Ngoja nianze kwa kusema.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
Kisha niongezee kwa kusema Andiko linaua bali Roho anahuisha.
Sasa hebu soma katika biblia upate kujua mzimu wa Samweli ulivyopandishwa.
11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.
1 Samweli 28:11
13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
1 Samweli 28:13
14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14
Je ! Saul alikutana na Samweli kwa yule mchawi?
Ili kupata picha ya karibu, lazima tuwe na hoja...
1 Mambo ya nyakati 10: 13- 14
1
3 Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,
14 asiulize kwa BWANA; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.
Hii habari inataja moja kwa moja kuwa Sauli alikosea kutaka msaada kwa Mchawi, hivyo Mungu akamuua.
1. Sauli ni mtu asie mtii Mungu, hivyo kama angejibiwa kupitia Mchawi, kiu yake ingetimia, kiu ya uasi juu ya Mungu.
Hata sasa wapo watu ambao kila wakimuomba Mungu, asipowajibu wanakimbilia kwa waganga au mizimu na andiko hili ndilo wanalishika.
2. Mungu amenyima watu wasiwaendeee waganga wala wachawi, hawezi vunja neno lake mwenyewe.
3. Taarifa za Samweli zinatia shaka, Samwel hakuwa Mtu wa kutaja laana kwa Sauli, ila Samweli alidumu katika kumuombea Sauli hadi Mungu alimuuliza, atadumu kumuombea Saul hadi lini? 1 samwel 16:1
4. Kutokana na Luka 16:18-31
Hakuna uwezekano wa mawasiliano kati ya wafu na watu walio hai...
Mtu akiwa hai anakuwa na uhuru wa kuchagua pa kwenda, ila akifa, habari yake imeisha, anaenda aliko chagua,... hakuna namna hata kwa maombi ya kumsaidia au kumuhamisha tena.
........26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu......