Habari zenu wana nzengo?
- Wanaume wa leo wanatimiza miaka 50 wanakaa kwa baba na mama
- Wanaume wa leo hawatunzi wazee wao, wazee wanatunzwa na mabinti
- Wanaume wa leo hawatunzi nyumba zao, badala yake wako busy na kuhudumia michepuko.
- Wanaume wa leo wengi hawasomeshi watoto, watoto wanasomeshwa na mama zao.
- Wanaume wa leo wanajua ulevi na uzinzi na sio kuwekeza ndio maana wanawake wengi sasa ndio wafanyabiashara na wajasiriamali.
- Wanaume wengi wa leo wanatunzwa na wanawake
Siko hapa kuleta ugomvi, niko hapa kuweka mambo sawa na kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa wanaume wengi sana hapa bongo, dhana hiyo ni potovu, ovu na iliyopitwa na wakati.
Wanaume wamekuwa wakiona wanawake kama ni watu wasio na upendo wa kweli, watu wenye kupenda pesa na wasio na utu.
Ndugu zangu, sisi hatupendi pesa, ila tunauchukia umasikini. Tukipata hela kutoka kwenu tunasomesha watoto wetu, tunawalisha, tunawatunza wazee wetu, tunapunguza umasikini wa familia.
Wanaume wanautafuta umasikini kwa udi na uvumba. Mshahara laki tano, huo huo uhonge, ujimwambafai kwa washikaji, uwanunulie ma bar maid bia yaani mnatafuta sifa za kijinga sana.