Siyo kweli kwamba wanawake tunapenda sana pesa, hatupendi umasikini

Siyo kweli kwamba wanawake tunapenda sana pesa, hatupendi umasikini

Kweli kabisa, mimi nauchukia sana umaskini ndio maana nafanya kazi kwa bidii ili kuhudumia wanao nitegemea ili na wao waweze kujitegemea. Hela ya mtu hapana aisee ,naridhika na ninachokipata. Wanawake tuache kuombaomba, tutafute hata kidogo cha kwetu, ikitokea umepawa hewala , lakini isiwe ni ada
Sasa wenzio wanataka iwe ada yani mwanaume hata akisema amsalimie kwa simu tu tayari😂 mizinga inaanza. Anakomaa kabisa umgee hela ukifeli inakuwa balaa.
 
Habari zenu wana nzengo?
  • Wanaume wa leo wanatimiza miaka 50 wanakaa kwa baba na mama
  • Wanaume wa leo hawatunzi wazee wao, wazee wanatunzwa na mabinti
  • Wanaume wa leo hawatunzi nyumba zao, badala yake wako busy na kuhudumia michepuko.
  • Wanaume wa leo wengi hawasomeshi watoto, watoto wanasomeshwa na mama zao.
  • Wanaume wa leo wanajua ulevi na uzinzi na sio kuwekeza ndio maana wanawake wengi sasa ndio wafanyabiashara na wajasiriamali.
  • Wanaume wengi wa leo wanatunzwa na wanawake
Siko hapa kuleta ugomvi, niko hapa kuweka mambo sawa na kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa wanaume wengi sana hapa bongo, dhana hiyo ni potovu, ovu na iliyopitwa na wakati.

Wanaume wamekuwa wakiona wanawake kama ni watu wasio na upendo wa kweli, watu wenye kupenda pesa na wasio na utu.

Ndugu zangu, sisi hatupendi pesa, ila tunauchukia umasikini. Tukipata hela kutoka kwenu tunasomesha watoto wetu, tunawalisha, tunawatunza wazee wetu, tunapunguza umasikini wa familia.

Wanaume wanautafuta umasikini kwa udi na uvumba. Mshahara laki tano, huo huo uhonge, ujimwambafai kwa washikaji, uwanunulie ma bar maid bia yaani mnatafuta sifa za kijinga sana.
Kwa kweli wanawake na pesa ni sawa tu na mgonjwa na uji! Yaani hamuwezi kutenganishwa.

Ni sawa tu na wanaume kupenda wanawake wengi (kuwaka tamaa)! Huo ndiyo ugonjwa wetu mkubwa! Ukiona mwanaume ameridhika na mwanamke mmoja pekee, basi utambue fika huyo hajakamilika.
 
Kweli kabisa, mimi nauchukia sana umaskini ndio maana nafanya kazi kwa bidii ili kuhudumia wanao nitegemea ili na wao waweze kujitegemea. Hela ya mtu hapana aisee ,naridhika na ninachokipata. Wanawake tuache kuombaomba, tutafute hata kidogo cha kwetu, ikitokea umepawa hewala , lakini isiwe ni ada
Wewe unaonesha umefundwa ebu wape elimu hawa wadogo zako kama mtoa mada
 
Wanaume mnapenda personal attacks mmeenda kufukua madam zake zingine
Kutwa mnatukana wadada humu mbona hamshambuliwi kaahhh
Huzuni sana
 
Kweli kabisa, mimi nauchukia sana umaskini ndio maana nafanya kazi kwa bidii ili kuhudumia wanao nitegemea ili na wao waweze kujitegemea. Hela ya mtu hapana aisee ,naridhika na ninachokipata. Wanawake tuache kuombaomba, tutafute hata kidogo cha kwetu, ikitokea umepawa hewala , lakini isiwe ni ada
Na tunachambwa balaa yaani kuanzia redion vituo vy television had kwenye mitandao ya kijamii sema ndo Ivo
 
Hiyo kazi yako ndio inajutia kiburi,sema unavyi weza Ila IPO siku utamng'ang'abia shamba boy na hauta kumbuka yote haya
 
Back
Top Bottom