Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Huyu jamaa alie kuandikisha mama yake ni dume la mbegu ikitokea akafa mamake alithi mali na ndugu zake bora kuliko mali yake kuliwa na huyo kahaba angeishia kuhonga tu
hapana, wanaandikishana mamaake akifa yeye anamilikishwa hivyo zinakuwa mali za urithi, nazo hazigawanywi pasu pasu 😅😅😋😋
 
Wewe ndio hujui sheria ya ndoa, sheria ya ndoa imesema kuwa mahakama ' inaweza ' kutoa amri ya matunzo Kwa mke au kwa mke wa zamani, Wakati wa kesi ya ndoa na baada ya kutolewa talaka hiyo, hiyo Sheria ya Ndoa imesema kuwa mahakama inaweza kutoa amri ya matunzo, sio Lazima yani inaweza kutoa au isitoe amri ya matunzo kwa mke au mke wa zamani, kasome kifungu Cha 115 Cha sheria ya Ndoa
Duh

Ova
 
Ndio maana nikakuambia ungekuwa Wakili ungepoteza kesi nyingi.
Kutoa istilahi Fulani haimaanishi unajua Jambo Fulani.
Hizo Kanuni za kutafsiri sheria "Principles of Statutory interpretation" wewe ndio umezileta hapa. Sasa ni jukumu lako kuzitaja na kuzifafanua.
Hapo ndio itajulikana kuwa kuna sheria ya kumfanya Mtalaka ahudumiwe au asihudumiwe.
Mwisho itajulikana Wakili msomi um epoteza kesi au vipi.

Nakukumbusha swali langu unajua maana ya busara Kutumika katika sheria? Alafu Kwa vile hujui Lugha najua unaniuliza tena Discretion ni kitu gani😀😀
Nafikiri jibu la swali hili litajikita kwenye moja ya hizo principles za kutafsiri sheria.

Nakukumbusha Mimi ni mtaalamu wa Lugha hivyo uwe Makini.

Nakusubiri.

Mjadlaa huu Watu wanajifunza so twende
  • kutoa istilahi kwenye sheria ni kiashiria kuwa unajua sheria, na ukikosea tu neno Moja kulitafsiri hapo unakuwa unapoteza maana halisi ya kifungu Cha sheria, ndiyo maana hapo awali nikakwambia maneno 'The Court may' maana yake hiyo ni hiyari au ni Mapenzi ya Mahakama, ingesema 'the court shall' maana yake Hilo jambo ni Lazima, na nikakupa na Sheria kabisa inaitwa The statutory interpretation Act, ukiingia huko ndiyo utakuta maana ya hayo maneno madogo madogo ambayo wewe unataka kuyapuuza wakati yana Umuhimu mkubwa kwenye statutory interpretation, ni Mimi ndiye nimekufundisha maana ya hayo maneno ulikuwa hujui, kama Mimi nitapoteza Kesi basi wewe hoja zako zote hazitaingizwa kwenye kumbukumbu za mahakama kabisa, Kwa sababu hazina authority i.e kifungu Cha sheria au Kitabu chochote Cha Kisheria i.e book of authority,
  • kumbe Hata principles za statutory interpretation huzijui, umeonyesha hujui hata unachosimamia Ili utafsiri sheria huwa zinatumika principles, Intention of the legislature nk, itabidi ujiulize kuwa Kwa Nini Bunge limesema hivi when granting or subsequent to the grant of a decree of divorce Kwa Nini Bunge litunge hiki kifungu Cha sheria i e s.115 of sheria ya Ndoa, hiyo inaitwa intention of the legislature, kumbe hata principles of statutory interpretation huzijui,na ndio maana huelewi unachoambiwa, ukiongeza na kutokujua Lugha ya Kisheria.
  • kama wewe ni mtaalam wa Lugha mbona haya maneno yamekushinda _ when granting or subsequent to the grant of a decree of divorce_ ? Nimekuuliza zaidi ya Mara tatu, lakini umeshindwa Kujibu na umekubali kule juu.
-
 
...Naona Wanaume wamelishikia Bango Kumpongeza Mwanaume Mwenzetu bila Kufikiri!
Kitakachotokea Sasa... Jamaa Bado Ataktakiwa kutoa matunzo Kwa ajili Mtoto/Watoto wake, atajua Mwenyewe wapi atakozitoa Mwenyewe! SI anacheza mpira na analipwa Hela nzuri TU?
Tusubiri tuone Hakimu atampangia atoe Shilingi ngapi za matunzo...ama aende Jela!
Tusubiri pia Mke wake apate Wakili Mzuri wakati Dunia' nzima inajua Hela zake Hakimu 'amezificha' Kwa kumpa Mama yake!
Tungoje tuone SHERIA za huko kuhusu Watoto zinavyofanya Kazi....Sio SHERIA za Wizara yetu ya Ustawi wa Jamii ! [emoji1][emoji1]
kwani kabla hawajaachana ni nani alikuwa anawatunza hao watoto..?...France jukumu la kutunza watoto ni jukumu la wazazi wote wawili na pia hakimu hakupangii umpatie nini na nini mtoto ila kuna masuala kama elimu,chakula,malazi, mavazi na uangalizi wa wazazi ni lazima , sasa atatoa wapi pesa ni jukumu lake hilo
 
Power of court to order maintenance for spouse (1) The court may order a man to pay maintenance to his wife or former wife– (a) (b) (c) (d) (e) (f) (g)
  • if he has refused or neglected to provide for her as required by section 63;
  • if he has deserted her, for so long as the desertion continues;
-during the course of any matrimonial proceedings;
-when granting or subsequent to the grant of a decree of separation; -when granting or sebsequent to the grant of a decree of divorce
Ukiisoma utaona kuwa mwanaume atatoa matunzo kwa mkewe wakati suala lao la taraka bado linafuatiliwa au lipo kwenye mchakato (inamaana bado ni bwana na bibi)
 
  • Wakili, umezungumzia Kuhusu kuandikisha Mali Kwa majina ya wengine eg Mama Ake Hakimi, na kusema kuwa Hana Mali yoyote (Hakimi), hiyo mahakama iliyoamua Hilo shauri ilitakiwa ijiulize inawezekana vipi mtu mwenye kipato Cha zaidi ya Bilioni 2 asiwe na Mali yoyote? Tuseme alikuwa anatumia zote? Mahakama ilitakiwa ijiulize Mama Hakimi ameweza vipi kumiliki ukwasi wa kutisha i.e hizo Mali kama Nyumba? , Mama Hakimi analipwa Bilioni ngapi , Hadi aweze kumiliki hizo Mali?, Mahakama ilitakiwa itoe amri kwa Hakimi atoe matunzo Kwa mke wake
  • Hapo Hakimi ametumia false pretense.
Sio kosa kisheria kumrithisha mtu mwingine mali. Ndio hapo msingi wa Hakim na watu wake walipowapiga katafunua wapinzani wao.
 
Sasa ukikataa ndoa,maana yake uzini ovyo !Sio poa ni upumbavu huo wa Kataa ndoa!inaonyesha ulilelewa ama baba,mama peke yake!
Wanaosema kataa ndoa wengi washatoboka spika wengi washika bendera za rangi rangi
 
Hata sheria za Tanzania wewe leo unakofanya kazi ijulikane mwisho wa mwezi unakunja cash Tsh 5mill mkeo aombe talaka atake kugawana mali kisha uonekane huna hata cent lakini mama yako aonekane ana hela na matunzo anakupa wewe hakuna wa kulibadilisha hilo.

Shida msingi wa mahakama zetu za Tanzania zinaamini bado ktk kum-favor mwanamke kwamba ni kiumbe dhaifu so lazima asaidiwe wenzetu hatua hiyo wameshaivuka wapo ktk kuitendea haki ile wanaita 50/50 ndiyo maana huko jamaa nae kaenda kufungua shauri wagawane mali za huyo mwanamke na kesi imeshafunguliwa.

Na kama point ni mali za wanandoa,inaweza kuwa nyumba tena moja nayo ukaitoa zawadi kwa watoto lakini kile kipato unachokiingiza kwenye shughuli zako na mali zako nyengine unaweza kukiamulia mwenyewe.

Hapana, sema watz wengi hawakuwa wanalifahamu ili na waliolifahamu hawawaamini wazazi wao, ila ili kujiepusha na vifo vya magonjwa ya kushtukiza, hebu jaribu njia hii ni salama na mimi naitumia ni muda sasa ili kulinda jasho langu
 
  • kutoa istilahi kwenye sheria ni kiashiria kuwa unajua sheria, na ukikosea tu neno Moja kulitafsiri hapo unakuwa unapoteza maana halisi ya kifungu Cha sheria, ndiyo maana hapo awali nikakwambia maneno 'The Court may' maana yake hiyo ni hiyari au ni Mapenzi ya Mahakama, ingesema 'the court shall' maana yake Hilo jambo ni Lazima, na nikakupa na Sheria kabisa inaitwa The statutory interpretation Act, ukiingia huko ndiyo utakuta maana ya hayo maneno madogo madogo ambayo wewe unataka kuyapuuza wakati yana Umuhimu mkubwa kwenye statutory interpretation, ni Mimi ndiye nimekufundisha maana ya hayo maneno ulikuwa hujui, kama Mimi nitapoteza Kesi basi wewe hoja zako zote hazitaingizwa kwenye kumbukumbu za mahakama kabisa, Kwa sababu hazina authority i.e kifungu Cha sheria au Kitabu chochote Cha Kisheria i.e book of authority,
  • kumbe Hata principles za statutory interpretation huzijui, umeonyesha hujui hata unachosimamia Ili utafsiri sheria huwa zinatumika principles, Intention of the legislature nk, itabidi ujiulize kuwa Kwa Nini Bunge limesema hivi when granting or subsequent to the grant of a decree of divorce Kwa Nini Bunge litunge hiki kifungu Cha sheria i e s.115 of sheria ya Ndoa, hiyo inaitwa intention of the legislature, kumbe hata principles of statutory interpretation huzijui,na ndio maana huelewi unachoambiwa, ukiongeza na kutokujua Lugha ya Kisheria.
  • kama wewe ni mtaalam wa Lugha mbona haya maneno yamekushinda _ when granting or subsequent to the grant of a decree of divorce_ ? Nimekuuliza zaidi ya Mara tatu, lakini umeshindwa Kujibu na umekubali kule juu.
-

Sheria huzijui,
Huwezi mhudumia Mtalaka (, Mwanamke au Mwanaume) uliyewahi kuwa naye kwenye Ndoa Kwa Sababu, Watu wengi kwenye jamii yetu hawezi kuishi peke Yao bila mahusiano.

Yaani kitendo cha kuachana Leo hii, ndani ya mwezi muda mfupi waliopeana talaka wapo kwenye mahusiano mengine.
Na hapo ndio inakuja hoja ya kuwa Mtalaka hahudumiwi.
Na sheria hiyohiyo inaeleza Jambo hilo.
Kasome sheria vizuri,
Anzia Vifungu vya 63, 118, 120- 130 utaona minachokieleza

Elewa kuwa zipo sababu za Mtu kupewa talaka ambazo zitaifanya Mahakama isimuamuru Mwanaume au Mwanamke kumhudumia Mwenza waliotengana, na sababu kubwa ni uasherati.

Mahakama Kutumia neno May ingetosha kukufungua macho kuwa Jambo hilo linategemea zaidi Mischief Rules.
 
  • Wakili, umezungumzia Kuhusu kuandikisha Mali Kwa majina ya wengine eg Mama Ake Hakimi, na kusema kuwa Hana Mali yoyote (Hakimi), hiyo mahakama iliyoamua Hilo shauri ilitakiwa ijiulize inawezekana vipi mtu mwenye kipato Cha zaidi ya Bilioni 2 asiwe na Mali yoyote? Tuseme alikuwa anatumia zote? Mahakama ilitakiwa ijiulize Mama Hakimi ameweza vipi kumiliki ukwasi wa kutisha i.e hizo Mali kama Nyumba? , Mama Hakimi analipwa Bilioni ngapi , Hadi aweze kumiliki hizo Mali?, Mahakama ilitakiwa itoe amri kwa Hakimi atoe matunzo Kwa mke wake
  • Hapo Hakimi ametumia false pretense.

Kwani mshara wako/mapato yako huwa unatumiaje? Kama hakuna ufuatiliaji wa mwenza ni ngumu sana, maana hata kumbukumbu za malalamiko kuwa hutunzwi hayapo. Na huko mbele ukute kila mtu anakula kwa jasho lake

Kama huwa unamgawia mkeo/mmeo kila kitu sawa naye ndo akapanga matumizi sawa.
Wengine wanalewea na kuhonga huko. Sasa kama hukuweza kujua mapato ya mwenza wako yanatumikaje huo ni uzembe wako.
 
Hizo mali zenyewe watu wanazo mtu ana familia ya mke na watoto watatu anaishi nyumba ya kupanga chumba 30k unatarajia kuna cha kugawa hapo labda agawe umeme kama tanesco
Watu wanagawana ndooo za maji,makochi,sahani vijiko mzee

Ova
 
Watu wanagawana ndooo za maji,makochi,sahani vijiko mzee

Ova
Dah sio mchezo nipo na wife nimempa asome hii comment kacheka sana. Hivo kuliko kugawana bora mmoja wenu amuachie mwenzake😂😂😂😂😂
 
Wewe ndio hujui sheria ya ndoa, sheria ya ndoa imesema kuwa mahakama ' inaweza ' kutoa amri ya matunzo Kwa mke au kwa mke wa zamani, Wakati wa kesi ya ndoa na baada ya kutolewa talaka hiyo, hiyo Sheria ya Ndoa imesema kuwa mahakama inaweza kutoa amri ya matunzo, sio Lazima yani inaweza kutoa au isitoe amri ya matunzo kwa mke au mke wa zamani, kasome kifungu Cha 115 Cha sheria ya Ndoa

Nilikuwa nakupima kuona kiwango chako cha Haki na Uelewa.
Kwa upande wa Haki umefeli Kwa sababu hizo sheria unazozinukuu unachagua Vifungu vinavyokupendeza na kupendelea Mwanamke ilihali ukisoma Vifungu vinavyofuata vinaeleza pia kuwa hata mwanamke anaweza kuambiwa amhudumie mwanaume aliyeachana naye.

Hii hoja nimeipinga na vipo Vifungu vinasapoti hoja yangu Kwa sababu mazingira ya Kitanzania Mtalaka hawezi kuishi mwenyewe Kwa hata miezi sita bila Kupata mpenzi anayemgegeda au wanayegegedana,

Pili, uelewa wako kuhusu Lugha ni mdogo ndio maana unafikiri Lugha ni vile MTU anavyoongea au kuandika bila kujua kuwa Lugha ni utamaduni, hivyo unapomzungumza kiingereza kuna sehemu tuu utapishana na tafsiri za Kiswahili kutokana na tofauti za kiutamaduni.

Ndio maana nikakuambia tafsiri ya Former wife haiwezi kuwa MKE wa zamani katika utamaduni WA kiafrika, Mtalaka haiwezi kuwa na maana ya MKE wa zamani.

Ndio maana kwenye hiyo sheria imetumia Mischief Rules kuziba gap la kiutamaduni baina ya Uafrika na Ujio WA sheria hizi za kizungu, na Ipo tayari kupokea mabadiliko yoyote kulingana na utashi na busara za Mahakama. Hata hivyo sheria hiyo imelenga kumpendelea mmoja wa wanandoa ikiwa hapo Kabla kina sheria zilikiukwa licha ya kuwa wamepeana Talaka
 
Hapana, sema watz wengi hawakuwa wanalifahamu ili na waliolifahamu hawawaamini wazazi wao, ila ili kujiepusha na vifo vya magonjwa ya kushtukiza, hebu jaribu njia hii ni salama na mimi naitumia ni muda sasa ili kulinda jasho langu
Unaweza muhamishia Mali,pesa zako kwa mama yako na akakuangusha
Hii inatokeaga na mimi nishaona,ilimkuta baharia mwenzangu ....mama yake alimyoosha kwelikweli

Ova
 
Kwetu Kenya Sheria ya urithi ilibadilishwa,kwamba kila mmoja atakuchukua kile alichochangia,kwa hiyo Hakuna Sheria ya pasu kwa pasu

Ije Na bongo ili watu waache kuvizia mali za wenzi wao!

Imeandikwa: kila mtu atakula kwa jasho lake!
 
Back
Top Bottom