Rais wa Marekani, Donald J. Trump, ametoa onyo kali kwa Iran kupitia mtandao wa X akisema kwamba subira ya Marekani na washirika wake inapungua kuhusu hali ya usalama katika eneo la Mashariki ya Kati.
Trump amedai kuwa wana jinsi ya kufuatilia mahali aliko "Kiongozi Mkuu" wa Iran, Ayatollah Khamenei, na kwamba mahali amejificha ni lengo rahisi, lakini kwa sasa, bado hawajafikiria kumuangamiza.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa hawatakaa kimya iwapo makombora ya Iran yataendelea kuelekezwa kwa raia au wanajeshi wa Marekani.
Aidha, Trump amesema kuwa ndege za kivita za Israel sasa zinatawala anga za Iran, ikiwa ni dalili ya Iran kulemewa na kujizuia na kujikinda dhidi ya mashambulizi ya ya Israel.
Ripoti za BBC za Juni 16, 2025, zinaonyesha kuwa Trump alizuia wazo la Israel la kumuua Khamenei, akiitaja kuwa si wazo zuri.
https://bio-nutrabalance.com/click.php
Licha ya Trump kupinga Khameni asiangamizwe (kwa sasa), Marekani inasemekana kuwa imetoa ujasusi wa hali ya juu kwa Israel.
Wakazi wa Mashariki ya Kati wanaendelea kuishi katika hofu, huku wataalamu wakishauri mazungumzo ya amani kama njia ya kutatua mzozo huu wa hatari.
@newsfeed