SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Ewaaa hayo ndyo mambo nipendayo kuyasikia
Piga bomu la atomic chapu vita iishe
 
Putin: Iran hawajaomba msaada wetu Bado wanaona wanajimudu. Wakiona wanatuhitaji watasema tuko tayari kuwasaidia. Hatukua na mkataba wa kusaidiana kiulizi wa anga kabla ya kuanza kushambuliana. Pamoja na hilo anasisitiza kuhusu Ukraine mpango ni kuichota yote, hatutabakiza jimbo hata moja.
 
Kama kweli Israel angekuwa kavimudu vita basi trump angekuwa hafikiri hata kuingia mzigoni
 
Kumsaidiaje huko kwa hasara Iran inayopata. Nuclear facillites zilizojengwa kwa miaka mingi na kwa gharama kubwa zinaharibiwa useme anamsaidia? Vinu vya kuzalishia mafuta vinapigwa vinaharibiwa wao hawaoni? Au mpaka ifikie kuwa kama gaza au Aleppo ndio aingie. USA na west na NATO wanamsaidia Ukraine tangu kombora la kwanza lilipopigwa pale kiev. Na hawafanyi siri. Wanatangaza kabisa na aina ya msaada anaotoa. Hata askari mamluki wanaopigana upande wa ukraine wao ndio wanawalipa. Kubali kataa. BRICS ni kwa ajili ya issue za uchumi sio kwenye issue za ulinzi na usalama.
 
Toka Febr 24,2022 mpaka leo June 19,2025 Miaka 3 mizima wakati Russia ni Supapawa kwa nini alishindwa kuichota yote kwa Masaa 72 aliyoyasema ???
 
Iran yashambulia Hospitali ya Soroka huko Israel

View: https://x.com/mossadil/status/1935556932062032139?s=61
Israel haijazuia raia wake kuchukua picha au video, imezuia zile zinazowaletea aibu na kuonyesha wanabondwa. Hizi za kutafuta huruma au kutoa uhalali wa kushambulia raia na wagonjwa zinasambazwa na mossad na Jeshi lenyewe ili wao wakijibu wapige popote. Ndio maana Kuna wengine wanasema Al aksa flood wakijua wapalestina wangekuja kuua raia wao wakapotezea, wakachelewa hata kuzuiq makusudi Hamas wasiendelee kuua raia ili baada ya hapo wapate uhalali wa kujiuliza wanavyotaka na ikiwezekana kuchukua Gaza yote au nusu moja KWA moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…