Hali ikiendelea kama ilivyo Iran itaanza mashambulizi ya angani kwa kutumia ndege za kivita aina ya Sukhoi Su-35 ilozinunua kutoka Russia na kuzipokea miaka miwili ilopita.
View attachment 3369522
Ndege ya kivita ya Russia Sukhi Su35. Picha na AP
Ndege hizo zipo katika kituo kipya cha jeshi la anga la Iran liitwalo Eagle -44 na kituo hicho kipo katikati ya milima kusini mwa Iran katika jimbo la Hormozgan kilomita 100 kutoka katika mfereji wa Hormuz.
Manunuzi ya ndege hizo yamo katika mkataba maalum wa kistrategjia kati ya Iran na Russia ambapo Iran imekuwa ikipeleka Russia makombora yajulikanayo kama Shaheed ambayo Russia yatumia katika vita vyake na Ukraine.
View attachment 3369525
Marubani wa IRGC wakiwa na moja ya Su-35 chini ya ardhi katika kituo cha kijeshi cha Eagle 44. Picha na Jeshi la Iran.