Hapo juu si unamkosoa Ayatollah ili mtu abaki katika nafasi yake si lazima amsikilize yeye ata Rais wa Iran? Sasa niambie huyo Waziri wa Ulinzi wa Israel kilichokamtoa nini kama wakisikilizana na Netanyahu? Au Rabin aliuawa sababu gani hapo Israel?
Sasa huoni tofauti ya Netanyahu na Ayatollah kwenye hilo.
Ayatollah hafukuzi mtu mwenye performance mbaya, yeye uwe chawa hilo tu. Netanyahu anafukuza kwa sababu na zina matokeo ya muda mrefu.
Netanyahu alimuondoa Defense Minister Gallant kwa sababu kadhaa ikiwemo tofauti zao za approach ya Operation. Gallant alikuwa anataka upole na unyenyekevu dhidi ya Hamas sababu wana mateka, Netanyahu ashapiga hesabu zake ameamua anawanyuka Hamas ili amalizane nao awashike Hezbollah ili amalizane na proxies za Iran kisha aje kwa Iran yenyewe jambo unaloona sasa.
Yohav Gallant yeye alikuwa anataka upole ili mateka warejeshwe kwa kusikiliza hoja za Hamas. Ambapo asingeweza fikia hatua ya sasa ya kudeal na Iran.
Wakati Netanyahu alitumia mateka kama kigezo, kwanza alihakikisha anawatafuta kwa jeshi sio kuwaomba magaidi na kusikiliza masharti yoyote.
Pia serikali ya Israel kwa sasa ni ya muungano, hata ya Lapid iliyopokezana na Netanyahu. Wanasiasa wenye msimamo mkali hawakumtaka Gallant walitaka mkono wa chuma gaidi akifyatua roketi fata appartment aliyotumia bomoa, mpaka wamenyoosha mikono.
Hamna cha sijui alifyatua akiwa hospitali, ilimradi kafyatua we fuata chanzo, hao wenye hospitali siku nyingine wajue madhara ya kukaa na silaha eneo la kiraia. Gallant alikuwa anaingia mtego wa Hamas na Hezbollah.
Baada ya Gallant kuondoka, tactics za Netanyahu unaziona. Baada ya Hamas, Hezbollah, humo katikati wakajichanganya Houthi. Baada yao kubwa la maadui Iran. Angekuwepo Gallant na sera zake hadi sasa tungekuwa tunabembelezana na Hamas kuachia mateka huku kina Haniyeh na Nasrallah wanakunywa alkasus na mikwara juu.
Mkuu wa Usalama wa Israel alijiuzuru kama wajibu wa Hamas kushtukiza October 7. Irab wana failures nyingi umeona Ayatollah anabadilisha mtu, au kuna anayejiuzuru miaka hii miwili?