Huu ujinga wa kwamba kuna taifa baba, mama, mtoto, mjomba na shangazi huwa mnajifunza wapi ??
Hata Sudan ya Kaskazini sio baba wa Sudan Kusini.
Kwa sababu Kuna Mataifa yenye nguvu kabisa duniani na maamuzi yao hayaingiliwi na Taifa linguine lolote(Total sovereignty)
Kama Marekani(USA), CHINA, RUSSIA , UINGEREZA.
Halafu Kuna vitaifa ambavyo ni Vassal state;
1)Mataifa yote yaliyopo kwenye muungano wa Nato, ambayo first command wao ni USA, second command wao ni Uingereza.
2)Mataifa yote yaliyopo kwenye kwenye Jumuiya ya Ulaya.
Wenye sauti ni Ujerumani na Ufaransa,
Bahati mbaya hapa Mataifa viongozi nayo yapo under influence ya USA, kutokana na NATO.
3)New emerging military cooperation AUKUS ambayo ni USA, UK, AUSTRALIA
4) Mataifa yenye Kambi za jeshi za kigeni hasa kutoka USA:
Japan, South Korea, Taiwan, Thailand, Kenya, Djibout, Senegal,Panama, Costa Ujerumani.
5)Mataifa yaliyopo kwenye Muungano wa CSTO unaongozwa na Urusi.
Kazakhstan, Armenia, Tajikistan, Uzbekistan, Belarus.
6)Non allignment Movement (NAM)
Mataifa yote yanayojifanya hayajachagua upande Tanzania tukiwemo, kiongozi wa hapa ni India, haya ndiyo Mataifa yanayoongozwa kwa unafiki duniani baada ya Mmarekani.
7)ASEAN COUNTRIES
Kuimarika kwa Uchina Kiuchumi na Kijeshi kunafanya kundi hili kuongozwa na Mchina na mwenyewe ndio mwenye sauti pamoja huyu anatumia zaidi mbinu ya kibiashara.
Hivyo ni kweli Kuna Taifa baba ,Mama, shangazi, mjomba,binamu, mpwa na jirani
Yote inaletwa na itikadi pamoja na masuala ya maslahi ya kitaifa iwe uchumi au ulinzi.