Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Eiwa vizuri, so unaamini kwa mfano tutoe kwa manzi/mtoto wa kike.. We unaweza ukapenda pua mwingine akapenda jicho mwingine wowowo mwingine rangi n.k

Kwa kifupi kila mtu na taste ake si ndivyo eeh?
Ndio ila tatizo la tamaa ya mwili ni sawa na njaa unapokuwa na njaa sana hata kile chakula ambacho kingekuwa reject kinakuwa first and only priority.
 
Ati! Hivi Nato wanavyohaha dhidi ya Russia alafu we unasema hawana uwezo wakupambana nao? Kwani hujiulizi kinachomfanga Nato ajitanue kuelekea mashariki ni nn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanatesti vifaru...vinalipuka kama moto wa korosho..
 
Kwanza nipende kushukuru kwa mchango wako, pili pengine hujanielewa nilichokiandika kutokana na nilivyokiwasilisha in general na siyo specific(point to point) au wewe ndo umetumia hisia kuelewa ndo maana ukajikita kuongelea hisia na assumption, sad enough muda wangu huwa ni limited sana ningekuwa active kivile nadhani tungebadilishana zaidi mawili matatu kiundan zaidi.

Ok ngoja nirudi kwenye mada: umezungumzia mambo mengi ambayo maudhui yake yote yanaonesha kuwa nimeibebesha Urusi mambo yasiyo sahihi, kitu ambacho haikuwa maana yangu na sijamaanisha hivo(nadhan hukujipa muda wa kunielewa vizuri maana yangu kabla ya kujibu), hakuna sehemu niliyokusudia kumaanisha kuwa biolabs, Azov battalion, ushirikiano wa kijeshi kati ya Ukraine na USA&NATO na mengine mengi uliyo yataja kwamba ni mipango ya putin kuja kuivamia Ukraine (nadhani ulitumia hisia kujaji) hivyo vyote ulivyovitaja ni mipango ya USA&NATO kutishia usalama wa Russia, "EU" kaongezeka kwenye hiyo combination kutishia usalama wa uchumi wa Russia hivo basi kwasasa Urusi haipo kwenye cold war na USA&NATO tu bali ni cold war ya RUSSIA vs USA&NATO+EU na wote wanataftana kwenye weak point, na ikitokea nchi yako ndo ikawa weak point basi tegemea kuona miamba hao wakitunishiana misuli nchini mwako kwasababu za kusadikika na siyo za kutimiza malengo yao, Mfano angalia sababu zilizotolewa na USA&NATO kuivamia Libya, Iraq, Yugoslavia na n.k kama ndo sababu halisi zilizokuwa nyuma ya pazia.
Angalia Sababu zilizotolewa na Urusi kumkingia kifua Asad wa Syria na zile zilizotolewa na USA&NATO kumuondoa Asad kama ndo sababu halisi (naamini kwa hayo mtukio ya nyuma baadhi ya sababu halisi dunia ishazijua na siyo zile zilizo tangazwa wakati wa tukio)
 
KUHUSU UKRAINE kutumika kama prox wa USA na wake zake vs Russia
Ukraine: tangu kutokea mgogoro wa Cremia 2014, USA&NATO walipata upenyo wa kuitumia Ukraine kui threat Russia ndo uanzishwaji wa hizo biolabs, neo-naz battalions, mafunzo ya kijeshi na usambazaji wa silaha zao Ukraine. Na hapo ndo imani ya mrusi kwa Ukraine ilivyoanza kubadilika nakuanza kumuona kama ndugu asie aminika, hivo basi ikamlazimu nae kuanza kusuka mipango ya kukabiliana na hao adui zake japo by that time hakuwa na sababu yenye mashiko juu ya kuingia Ukraine kupambana na hiyo mipango ovu ya USA&NATO.

EU kaingizwa na USA kwenye Cold war na Russia ili apambane nae kiuchumi akiwa kama mteja wake mkubwa wa gas, oil, chakula na n.k.
USA yupo tayari kuona raia wa EU wanakufa kwa baridi na njaa nasiyo kuona EU wakiendelea kufanya biashara na Russia, yupo tayari kuona Raia wa Ukraine wanakufa kupitia NATO ili kuendelea kuichosha Urusi kijeshi, USA yupo tayari kuishinikiza EU kumuwekea vikwazo vingi Russia hata kama wanaumia EU ili kuendelea kuharibu uchumi wa Urusi.

Russia nae anatumia mbinu hizo japo kinyume chake kuhakikisha anakwepa makombora yote ya USA kuhusu kudhoofisha nguvu ya jeshi lake na uchumi wa nchi yake, na ndo maana ukiangalia kinachoendelea Ukraine kuna Operation ya kijeshi iliyojikita zaidi kuharibu miundo mbinu ya kijeshi ya Ukraine kupitia mgongo wa USA&NATO at the sametime ipo kwenye vita ya uchumi na EU kwa kulenga kuthibiti maeneo mhimu ya kiuchumi Ukraine ambayo yanatumika kama feedbreath kwa EU mfano kuthibiti black sea ports, kuthibiti key economic points za Ukraine ambazo anaweza kuja kuzitumia kama threaten points za kuifanya Ukraine ibadili mlengo wake wa siasa.

Tujiulize haya maswali naamini tunaweza pata mwanga
1. Ukraine ilitangaza tu nia ya kujiunga ikavamiwa, lakini Fin na Swiz zimekusanya hadi maombi ila amani ipo?
2. Kwanini hapo awali Urusi iliikubalia Ukraine kujiunga EU ila baadae ikabadili sera na kukataa?
3. Kwanini EU, USA na G7 hawalali na wanaumiza kichwa kisa Ukraine?
4.kwanini EU wameamua hadi kutesa raia wao kisa Ukraine?
5.kwanini rais zelensky kaamua kubet maisha ya raia wake kwa USA na EU? Je nikweli alivyo tangaza vita na Mrusi aliamua yeye na nchi yake au waliamua wengine yeye akapewa tu kazi ya kutangaza na kupitisha sheria?
6. Kwanini USA na washirika wake waliamua kuwatambua neo-naz wa Ukraine hadi kuwapatia battalions na mafunzo ya kijeshi? Ngoja niishie hapo

I hope siku nikipata muda mzuri nitachambua kiundani zaidi ila naomba nieleweke ni rahisi sana Russia kuwafanya EU waendelee kumtegemea kupitia Ukraine na nivigumu EU kuepukana na Mrusi kupitia mgongo wa operation yake ya Ukraine na ukweli usio pingika kuwa USA kufanikiwa kwa %kubwa kuziingiza kwenye mgogoro wa kiuchumi Russia na EU kupitia hii operation(USA hana Rafiki wala adui, rafiki yake niyule anae pambania masilahi yake na adui yake ni yule anaepingana na masilahi yake) pia USA imeshindwa vibaya mno kuidhoofisha Urusi kijeshi kupitia operation yake hasa baada ya hao panya wake iliyo watrain kwa miaka mingi kujisalimisha kama migambo wa buza.
 
Ni kweli, Ukraine imezidiwa kila kitu na Urusi hivyo haiwezi kushinda kijeshi.

Ila msaada walioupata na wanaoupata mpaka Sasa umewasaidia mno kuchelewesha ushindi wa Urusi na kuwatia hasara kubwa.
T14 Armata Tsh
Sasa jiulize:
USA,UK na some NATO walikua wakiifundisha Jeshi la Ukraine miaka zaidi ya 8.

Wamewajengea miundombinu ya kijeshi miaka zaidi ya 8.

Wametoa michango ya fedha na silaha,

Urusi imefanya OP yake Huku ikiwa imewekewa vikwazo vingi mno ambavyo havijawahi kuwekwa kwa nchi yoyote duniani toka Dunia ianze.

Vikwazo ambavyo maumivu yake yanapiga nusu Urusi nusu WENATO
Unajua NATO Ina nchi takeiban 30,
Zimetoa silaha,fedha na taarifa za Kijasusi.
Japan sio NATO lakini katoa fedha isaidie kumshinda Russia.

Australia sio NATO katoa silaha na fedha,

Finland Sweden sio NATO lakini walishiriki kuweka vikwazo,vikwazo NAIA yake ni I kudhoofisha uchumi ili nchi ishindwe kuwndesha vita,Kisha ipigwe.

NATO wanaweza kupeleka majeshi hata kwa nchi isiyo mwanachama.
Mfano Yugoslavia,kuiokoa Kosovo dhidi ya Serbia.
Vita hii ilipelekea Slobodani Milosevic kukamatwa na kufungwa,Kisha akafua gerezani.

Hata kama sio NATO lakini baadhi ya nchi ambazo ni Wanachama wa NATO waliishirikiana na Marekani huko Iraq, Afghanistan,Syria na Libya .

USA na NATO waliogopa kuingia mazima.
Maneno ya Biden yapo humu.
" We are dealing with the biggest army in the world,not terrorist organization."
Kulikua Kuna haja Gani ya kupeleka silaha dhaifu dhidi ya might Russia kama sio kuwaponza wa Ukraine TU.

Sasa kama unavyosema USA anampa Israel sophisticated weapons.wakati Israel ana pigana na Adui dhaifu sana asie wala na Kambi za majeshi (Palestina).
Ama nchi dhaifu kama Iran na Syria?

Sasa kwa nini Badala ya kumpa Ukraine silaha Kali kwa sababu anapigana na nchi kubwa Urusi, yeye
USA anakwenda kumpa Israel silaha kali anaepigana na maadui dhaifu?

Mbona anapeleka silaha Kali kabisa Taiwan bila kujua atamudu vipi kuzitumia?

Kumbuka USA na UK na NATO wengine walikuwepo ndani ya Ukraine wakiwafundisha majeshi ya Ukraine,kwa Nini hawakuwafundisha kutumia silaha za USA na NATO?

Urusi imeonesha udhaifu Gani,kupigwa inaweza kupigwa,lakini kwa hapa haijapigwa.
Na wala hakuna udhaifu wowote ni propaganda TU za west.wametuamia media zao kupotosha sana.

Kama wastaafu ma Gen wa USA,German na huyo wa Bulgaria wanasema Ukraine Hatashinda Mimi ni nani?

Tena kwa kukumbusha TU ni kwamba, hii ni tabia ya NATO. Urusi akipigana na nchi nyingine humpa nchi hiyo silaha.ilitokea hivihivi huko Afhanistan dhidi ya USSR
Sasa safari hii vita/ OP imepiganwa mpakani kabisa na west ambapo ndio nyumbani kwa NATO tofauti na wakati ule kule Afghanistan.
Lakini hamna kitu Cha maana wamemfanya mrushi ashindwe kuiadhibu Ukraine .
 
Wanapigana na Mataifa 40, Nato, plus USA and others.
 
Kuna boss wangu mmoja alikuwa ni mchambuzi kama hivi. Anaamini anajua kuliko wenye tukio. Hii personality huwa inazalilisha sana watu wakishakuzoea kuwa wewe ni mr I know more.
 
Russia bado hajatwaa yale majimbo anayowania ya Donetsk na Luhanskh lakini Mujahedeen humu wanaleta porojo kibau wakati vita ambavyo watu walidanganya eti ni vya siku tatu sasa vinaingia mwezi wa nne.

Hivi vita bado sana na hata Russia wakiteka hayo majimbo haitakuwa mwisho wa vita ndio sasa wataingia kwenye "Guerrilla Warfare" ambayo Russia haiwezi kushinda kamwe.
 
Yeye hajui ila ndugu Imeloa unajua heheheee
Inaonekana unayajua mengi sna pale KREMLIN
Ila nakushauri kaeni kwakutulia mpaka jamaa wapite na ODESSA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@T14 Armata

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Turkey hana tofauti na malaya wa buguruni pale.
 
Haaa! Ktk Vita Hasara haiepukiki.
Vifo vya askari ni kawaida na ulipuwaji dhana ni kawaida pia.
Hakuna mahali popote Urusi ilitoa muda wa operation.
Tazama maelfu ya Wapiganaji wamejisalimisha na bandali imetetwaliwa mbali na climea.
Luhansinky na Donenky wanajitenga.
Bandari ya Ok Odesa imefungwa.
Waukraine wamekuwa wakimbizi.
Miundombinu ya Kijeshi imekufa.
Naweza sema walioko krk mapambano ni Mataifa 40 dhidi ya Moscow.
Njaa na mifumko ya bei Ulaya imekidhili bora Africa.
Putin sarafu yake imepanda na Vita inaendelea.
 
Rudia kusoma hiyo historia yako.......hakuna mmarekani aliyemkata babu yako mikono......Soma vizuri hiyo history 2.....
ila daah Kuna watu mnamavichwa magumu aisee mzungu anaishi marekani sindio huyo huyo ndio mzungu wawingereza ama ugerman au haujui kua waingereza waliokua wakiishi marekani huku wakifanya shughuli za kilimo na viwanda huku wakimuweka mwafrika Kama mtumwa kwa viwanda vyao ndio hao hao walidai Uhuru na kujiita USA
 
Ndio ila tatizo la tamaa ya mwili ni sawa na njaa unapokuwa na njaa sana hata kile chakula ambacho kingekuwa reject kinakuwa first and only priority.
Eiwaa taratibu unakuja kwenye point yangu.

Awam hii ngoja nirefushe maelezo nimalizie maana hapa kope zishaanza kupendana. 😴😴😴😴😴

Naweza nikasema zaidi ya 90% ya binadam wa kileo hatuna uwezo wa kucontrol fikra zetu. Ni wachache mno waliobarikiwa hilo jambo.

Mind zetu zinanjaa ya Perfection, tuko makini sana kutafuta kasoro kuliko lile zuri lililopo mbele.

Mbaya zaidi fikra zetu zimetawaliwa na hisia zaidi kuliko kuuruhusu ubongo kufanya kazi yake.

Leo hii mtu akipenda (mahaba yakiwa juu) anafunika kila udhaifu ulio mbele yake. Na hii aina binafsi huwa siioni kama ni mahaba bali upumbavu. Mahaba sio kukana udhaifu bali kuuona udhaifu kisha kuuridhia kwa kuamini hakuna kilicho timilifu.

Vile vile leo hii mtu akichukia nukta katika wewe, basi unakosa zuri kwake. Lolote utakalofanya atakuwa anatafuta kasoro. Huyu naye anakuwa anaendeshwa na hisia zaidi kuliko kuupa uhuru ubongo wake ufanye maamuzi. Nayo hii ni aina nyingine ya upumbavu vile vile.

Hapa kwenye huu uzi mainly ziko team mbili. 😂 Team NATO na Team Russia (na mie nikiwemo). Katika hizi team mbili kote kote kuna watu wanajielewa na kuna watu ndio vile tena tafran 🤗

Kuna watu katika makundi hayo mawili wana mahaba sana, na kuna wengine wana chuki sana. Mwenye mahaba hata ukimletea taarifa ya Uongo maadam inamfurahisha haipingi wala kujiuliza uhalisia wa kilichozungumzwa 🤣.

Na yule mwenye chuki nae akifikishiwa taarifa hupinga pia hata kama ni ya kweli maadam haimpendezi hatoikubali.

Me naamini sio kila msemo wa kiswahili lazima utimie 🤔, hivo unaweza kupenda boga ukachukia majani yake. Mfano mie binafsi naweza kujieleza kua katika maisha kuna aspects nyingi tu za mwanadam.

Kuanzia maisha yake ya ndani binafsi ye na familia, ya kijamii, kiuchumi, kibiashara na kisiasa.

Naweza kusema katika aspects hizo za maisha baadhi yake kama Kisiasa na kijamii sizipendi zote zitokazo west.

Kwasababu Siasa zao za kibabe zilizopambwa kwa jina la democracy na issue za kijamii ambazo zikitajwa hapa we mwamba huwa unapiga kelele ukidai zinakutia kichefuuuu kama ushoga na mengineyo. Ila haina maana ya kusema ninawachukia kwa kila kitu.

Na ni vitu hivyo hivyo ambavyo binafsi nimeviona na sivipendi lakini kuna mtu anavipenda na kuvihusudu kwa kuvifanya sehem ya maisha yake 😂

Kwa kua kila mtu na taste ake basi tupeane uhuru kila mmoja amtulie na lake kiroho safi 🤗. Na atakaye amua kutaka ku'challange kile anachokiamini mwenzie basi akichallenge with facts ambazo sio double standard.

Kwenye nyeusi iitwe nyeusi na nyeupe iitwe nyeupe. Sio kugeuza geuza mambo kingese kisa flan au kundi flani limesema au kufanya na hii tabia anayo sana mzee flan na toto flan hivi 😂😂😂

Tuishie hapo point angu imejificha ila naamini una akili timamu kuifichua 👊

Kwaherini kwa leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…