Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

wakuu ila tukiacha ushabiki wa pro-max tukarudi kwenye uhalisia basi kwa pamoja tutasema Putin ni Kichwa haswaa. Kuendesha operation zote mbili(kijeshi na kiuchumi) kwa mpigo against nchi zaidi ya 30+ zenye nguvu na bado unazitoa jasho siyo jambo la kawaida. Sisi wengine kelele za wake zetu tu ndani huwa zinatuvuruga kichwa tunakimbia ndani na kwenda kushinda bar, vijiwen na n.k sembuse makelele ya USA, NATO na EU.

Mzee putin apewe heshima yake haijalishi wewe ni pro-Putin au pro-NATO penye ukweli tusimame pamoja.
 
Kama kaonya ni kuwa kaonya, kwa greater thinkers hapo anamaanisha umakini unahitajika yaani hata kama wameshinda sasaivi huko mbeleni wawe macho, watu wanaangalia future, sio mbaya kutoa mawazo yake, je tukiongea sasa hali ipoje? Tunasema operations zinaendelea kama zilivyopangwa
 
Naona kisu kimegusa mfupa ..... Utukivu unahitajika. Awali ilikuwa unajinasibu vizuri tu upo neutral ...Ila kwa moment umerudi na majibu unayotoa kaka pole vumilia tu ndio maisha haya .... Upande uliochagua una maumivu makali Sana mpaka na wewe kujionesha kimaandishi japo kwa kujifichaficha watambuzi tumetambua . Pole lakini
 
Kazi ipo kweli kweli... Nimesema hivi
Kwa kua kila mtu na taste ake basi tupeane uhuru kila mmoja atulie na lake kiroho safi 🤗.
Nikaongeza na hili...
 Na atakaye amua kutaka ku'challange kile anachokiamini mwenzie basi akichallenge with facts ambazo sio double standard

Hoja zenyewe sasa unazotoa mwamba...
Kwani tukiimba wote nyimbo za kumsifu na kumuabudu puttin nn kitabadilika? Haya si ni maandishi tu yanaishia hapa hapa?
Hapo si tumekubaliana kila mmoja abaki na lake kiroho safi au? Au au auuuu?😂
______________________________

Haya tukakubaliana kupeana challenge endapo mtu akitaka lakini iwe kwa facts zenye mashiko sio ushabiki wa sizitaki mbichi hizi... Facts zenyewe sasa ndio ka hizi 🤔
OKEY RUSSIA KASHINDA, THEN WHAT? UTARUDI KWAKO KUJISIFIA KWA MKEO KUWA MMESHINDA
Ase huo upande bado mna safari ndefu sana 👊
 
Chanzo,
Mmarekani toka Buza kwa Mpalange

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Hivi mgambo wa buza tumewakosea nn?
 
Ha ha ha ni kweli jomba ndio maana nikasema kila mtu kuna point anaielewa kulingana na kile alichonacho kichwani.

Kwa mfano mie na baadhi ya wengine tunaona Issue ya Putin kuwawahi ama kujiingiza mwenyewe kwenye mtego aliokuwa anatengenezewa moja wapo ni katika kuivunja unipolarity na kuiweka dunia kwenye multipolarity.

Na hii imekuwa ikitamkwa mara kwa mara na waziri wa mambo ya nje wa Taifa hilo Ladrov.

Na kwa kiasi kikubwa kafanikiwa how? Kama hivi...
1. Kuondoa Imani ya mataifa mengine dhidi ya hizi International community ambazo of course zimekuwa kama fimbo ya kuwanyoosha mataifa mengine.

2. Kawavua nguo mataifa haya ni kudhihilisha yaliyo vifuani mwao hasa kwenye swala la white supremacist. Hawa jamaa ni wabaguzi mno, migogoro mingine inayoendelea duniani wameifumbia macho ila kona ni Ukraine as if pale ndio kuna watu tu kwingine kuna mbuzi na bata.

3. Kuna issue zingine kama usemavyo ngumu kuzielewa mpaka zifanyike, mfano ISSUE ya RUBLE, Nani aliwazs hata kwa bahati mbaya kua Putin na team yake waliwaza kuibomoa dollar 😂 hawapo.

Nani aliwaza hiyo Currency ya Ruble itapewa nguvu na hao hao wanaojikuta viongozi wa dunia kwa kuiongezea demand sokoni? Kupitia basic needs kama nishati?

4. Kawapa Confidence mataifa mengine kua yanaweza kujitegemea na kuishi nje ya Unipolarity, kuishi nje ya WESTERN HEGEMONY. mfano wa hili angalia mataifa yalioanza kumvimbia US baada ya huu mgogoro 🤣

5. Hata US anajua, kwa kunukuu kauli za Biden, kua dunia inaenda kupata New World Order, akiwasisitiza wakurugenzi aliokuwa anazungumza nao kua they should take a lead... Hii inaleta tafsiri ipi... Ni ile ya mapigano kati ya Old World (Westerers) na New World (Easterners).

Na hapa ninaweza sema kua lengo la Westerners (kutokana na kile nachokiona nje, hapa nisinukuliwe as if ndio malengo ambayo yameandikwa kwenye nyaraka zao) lilikuwa lile ambalo limefail toka awali, mwanzo wa hii OP.

Wanajua hawawezi kupigana directly na Russia. Shida yao kwao ni Putin... Target yao kubwa ilikuwa kuuharibu uchumi wa Russia, ile kufumba na kufumbua kuzua migogoro ya ndani kwa ndani, wananchi wapate hasira waingie barabarani kumpindua Rais wao.

Hii irejee kwenye kauli zao hao viongozi kiaso cha dementia Joe alifikia hatua ya kuzungumza wazi kua PUTIN inabidi aondolewe madarakani. Na hilo pia la kutaka kufanya mapinduzi kupitia ubomoaji wa uchumi PUTIN alilisema mwenywe na akidai westerners wameshindwa katika hilo... 🤗

Na mengineyo zaidi commets isiwe ndefu ikakerrrra...
Tuko pamoja jemedari 👊

Hapo ndipo utaona power ya Uzalendo dadeki... Inabidi tuwape pongezi pia warusi wote (hapa nalenga Raia sio Sie ma Pro) kwa utulivu waliouonesha.

Nahisi hili ni jambo kubwa ambalo tunapaswa tulione pia... Wananchi wa Russia kipindi kama hiki wamejionesha wako pamoja than before, indicator ya kuthibitisha hii kauli angalia kwenye Approval rate ya Putin kabla na baada ya Special OP.

Trust juu yake imeongezeka, pembeni anazungukwa na team makini so mipango nayo yaja imenyooka. Kila kitu bam bam 🤣🤣🤣

Mwisho nimesahau, kuna Post zile za mwanzo kuna hoja kama maswali hivi uliyatoa jana nilikuwa na usingizi nikayapitia juu juu tu😂... Ukipata mda anzisha ule uzi unaosema af tutajadiliana huko taratibu moja baada ya lingine... Usisahau kututag tu.
 
Unalazimisha mambo kulifanya hili liwe jambo binafsi..
Habari za asubuhi, kumekucha napeleka watoto kanisani, j2 imeanza vizuri kwa upande wangu nipo na familia, vp ww umeamka na hali gani huko kwenye ushindi bwana mtoto wa nzi? Tujuliane kwanza hali😀
 
Ukijifunza gasho jammo shatonai NASA pou?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…