Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kwa maelezo ya mtandaoni, hii nakiri hii sijawahi kuisoma kwenye kitabu chochote Wala kufanya hesabu zake.

1) Benki kuu za Mataifa duniani
Tamaa ya kumiliki dhahabu nyingi ikiwa kama akiba ili itumike kipindi Cha dharura.

2) Uhitaji wa urembo wa gharama

3)Matumizi ya dhahabu katika vyombo vya kielectroniki hadi simu zetu.

4)kupungua kwa uzalishaji

Sababu hizo ndio hupeelekea dhahabu kupanda kwa thamani.
Vizuri kwa kujaribu ila kwa wingi wa dhahabu inayochimbwa hayo yaliyoandikwa katu hayawezi kua matumizi pekee. Ukiachana zile nadharia za baadhi ya watu kuhusu dhahabu.

Kilichopo kwenye dhahabu na cha muhim zaidi ni "Limited Supply"... Dhahabu duniani kote inapatikana at a "Limited Quantity"... "Limited Supply" kwenye "High demand" ndicho kinachopelekea "Rise in Value"...

That's why zinatunzwa hasa na Central banks za mataifa karibia yote dunian kama "Reserves" yao. Gold ni International standard ambayo thamani yake haiwi affected kwa zile sababu tulizoziona apo juu kuhusu Currencies...

Sasa kupitia maswali tunayojaribu kuulizana basi rejea kuitazama tema Dollar na mwenendo wake chini ya Biden [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1732][emoji1732][emoji1732]
 
Mwanangu una uchungu hatari [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hivi msululu wa ule wa magari ya kivita na vifaru kwa urefu wa maili 1.3 vimegeuzwa chuma chakavu vyote

Urusi kapigwa, kashindwa, kapoteza majenerali 4 na vifo vya askari wake wengi kwa muda mfupi zaidi rekodi ya juu zaidi

Askari wa Urusi wamewagomea wakuu wao kusogea mbele wakati huo Vifaa vya kisasa vinaingia kuwasaidia UKRAINE

ibaki tu wazi zama za ubabe na kupiga nchi nyingine sababu una nukes unatishia watu zimepitwa na wakati

Russia is no longer Super Power ila tu anabaki na nafasi with large arsenal of nukes
Bro msululu ulikua 64km. Yan nilivyouona ule msululu nilikua najiambia moyoni kwamba Ukraine ndo bhas tena lkn mpk Leo Kiev bado imeshindikana kutwaliwa.
Screenshot_2022-03-18-01-12-06-764_com.android.chrome.jpg
 
Colonel Sergei Vladimirovich Sukharev, commander #331pdp : "In August 2021, by order of the Defense Ministry, I was appointed to the post of regimental commander, which I am very proud of. And I assure you that we will continue the glorious traditions of this regiment." Great traditions, I think , keep it up

✊✊
 
kisiju pwani umekiona tulichokua tunakisema???
Bado ni speculation.
Ila nguvu ya Ushawishi wa west lazima iteteleke?
Mataifa mengi yataamka kwenye hili.
Wamarekani wamefaidika na huu mfumo kwa miaka mingi uanguke tu[/QUOTE][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] atari na nusu... Twendelee kuongeza maarifa uku

Link 1.

Link 2.
 
NI silaha gani Kali ambazo mpaka sasa haijatumia kwenye hii Vita?! Au unataka watumie nyuklia au chemical weapons?! Maana masilaha yake mazito mazito karibu yote kashatumia kuanzia thermobaric bombs,cluster bombs,iskander missiles,kalibr missiles, artillery shells,nk.
Ukweli usemwe tu kwamba kwenye Vita hii Urusi imeonyesha udhaifu mkubwa sana.
Right On the money 🔨🔨🔨
 
Hivi ww jamaa unajua unacho kiongea kweli au unaongea tu?
CIA wana sema hakuna bomu lenye uzito juu ya kilo 500 lililo tumika wewe mla mihogo kutoka sumbawanga inabisha?

Hivi unajua mlipuko wa bomu la tani 3 au unausikia? Wabongo tuna ujuaji wa kipuuzi kabisa.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Kwahiyo Iskander lina kilo mbili?! Si kuna jamaa kapost screenshot huko juu warheads zake NI kuanzia 500kg-700kg/800kg,hlf ww muuza kahawa kutoka mbande unabisha.
 
Ongea vitu vyenye maana, mtu akikosea basi eleza hoja sahihi ni ipi ili pia na yeye ajifunze kama kuna cha kujifunza. Hii ya kila jibu lako kusema jielimishe wakati hajaweza kushawishi watu na kile kidogo unachokijua ni jambo ambalo nalo linahitaji elimu.
Hapa utawatoa watu povu bure,unauliza mambo makubwa mno ambayo huwezi kupewa majibu sahihi.
 
Wakuu mwenye full story ya USSR kwa kiswahili basi anitumie nipate mwanga kidogo ya huu uzi..?
Maana umekaa kimkakati sana kama hujui historia vizuri juu ya hii Miamba.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
USSR ni umoja ulounda nchi za kijamaa yaani Union of Soviet Social Republics au umoja wa kisovieti Soviet republics.

Nchi zilounda umoja huu zilikuwa ni pamoja na Poland, Lithuania, Estonia, Latvia, Georgia, Ukraine, Belarus, Uzbekistan, Kazakhstan, Armenia na Moldova. Pia kuna nchi zingine ndogondogo kama vile Tajikistan, Krygzstan, Turkmenistan na Uzbekistan nazo ziliunda USSR.

Sehemu hii iliitwa Eurasia na ilitawala eneo hili kutokea Moscow huku majimbo makuu kama Kyiv, Leningrad na Minsks yakiwa ni majiji makuu.

Kiongozi wa kwanza wa USSR aliitwa Vladmir Lenin ambae mwaka 1917 akiwa na wenzake waloitwa Bolshevicks aliongoza mapinduzi ya kuiondoa serikali ya himaya ya Russia yaani Russian Empire na kuunda serikali ya kijamaa ya USSR ambayo ilifuata misingi ya kijamaa na hiyo ikiwa ni mwaka 1922 baada ya mapigano ya ndani kwa ndani kati ya wafuasi wa Lenin na wafuasi walokuwa wakiwapinga hawa Bolshevicks.

Lenin alifariki mwaka 1924 na akaja bwana Joseph Stalin ambae sera zake zilikuwa ni uchumi imara ambapo viwanda vingi vilijengwa na mashamba ya kulima kwa ujumla yalianzishwa na ilikuwa ni program ya miaka 5.

Hii ya kuanzisha mashamba ya ujumla iliitwa "collectivization" ni mwamba serikali ilianzisha mashamba makubwa ambayo watu walikwenda kulima kwa kutumia njia za kizamani ambapo akiba ya chakula ilitosheleza kulisha wakazi wa miji mikubwa, uwepo wa malighafi ya kutosha na kisha kukawepo na mazao mengi ya kusafirisha nje ya USSR.

Stalin alikuwa katili na hakutaka upinzani na kama alihisi kuwepo upinzani watu walifungwa au kupotezwa iwe wanajeshi, wanachama wenzake wa chama cha kikomunisti au wananchi wa kawaida.

Mwaka 1939 Stalin aliungana na Wanazi (mkataba ulotwa Nazi- Soviet Pact) kwa malengo ya kugawana Poland na kutogombania sehemu hiyo.

Lakini wakati wa vita ya kuu ya pili ya Dunia, Stalin akavamia sehemu ulokuwa ndo nchi za Estonia, Latvia, Lithuania na akaichukua mazima sehemu yote ya Poland. Mwaka 1941 zikapigwa vikali kati ya majeshi ya Lenin na wanazi na Ujerumani ikatekwa (upande wa mashariki ulokujaitwa Ujerumani Mashariki) na baadae mwaka 1945 Lenin akatangazwa mshindi.

Baada ya Lenin kuwa bingwa upande wa mashariki akiwa amechukua sehemu kubwa ilokujaitwa Estern Bloc baadae mwaka 1947 vita baridi au Cold War ikaanza na upande wa magharibi ikaitwa Western bloc ambayo ilikuja na wazo la kuanzisha umoja wa kujilinda dhidi ya Lenin na NATO ikazaliwa mwaka 1949.

Lenin alifariki mwaka 1953 na akaja bwana Nikita Khrushkev ambae alikuta mipango ya kuondoa sera za Lenin ila akapalilia na kihakikisha USSR inapaa kiuchumi na ndo ikaanzishwa satelite ya USSR ya kwanza pamoja na ndege ya kwenda angani au Spaceflight ambayo baadae mwaka 1979 ilitua kwenye sayari ya Venus.

Muda wote huo USSR na Marekani walikuwa wakizungumza na kushirikiana katika programs kama hizo za mwezini na kadhalika lakini uhusiano ukaingia shubiri mwaka 1980 pale USSR walipopeleka majeshi yake nchini Afghanstan na Marekani wao wakawa wanapeleka silaha kwa Mujaheeden ( ni kama leo wanawapelekea silaha wapiganaji walioko Ukraine).

Mwaka 1989 dunia ilianza kushuhudia kuvunjika kwa sehemu kubwa ya USSR ambapo nchi nyingi zilounda umoja huo zilianza kufanya chaguzi mbalimbali ambazo zilileta mabadiliko ya serikali na viongozi wapya.

Poland na Hungary ziliendesha chaguzi zao kistahamilivu lakini nchini Romania uchaguzi ulipelekea kutokea machafuko ambayo yalipelekea kuuawa kwa kiongozi wa nchi hiyo Nicolae Ceausescu na mke wake Elena. Baadae mwaka huohuo ukuta wa berlin Berlin Wall ukabomolewa na kudondoka na wajerumani wa Mashariki wakakutana uso kwa uso na Wajerumani wa Magharibi na vita baridi ikaishia hapo.

Mwaka 1990 ndo uloanzisha mgogoro wa leo ambapo kiongozi wa USSR Mikhail Gorbachev alidanganywa na waziri wa nchi wa Marekani James Baker kwamba NATO isingejipanua upande wa mashariki. Ni Gorbachev ambae kwa siri alikubaliana na raisi wa Marekani wa wakti huo George Bush (mkubwa) kwamba ilokuwa Ujerumani Mashariki iruhusiwe kujiunga na nchi za Magharibi lakini akasahau ( au kwa makusudi) alikuwa alifahamu kuwa muungano wa Ujerumani magharibi (ilokuwa mwanachama wa NATO) ungeiingiza moja kwa moja Ujerumani mashariki ndani ya NATO likiwa taifa moja la Ujerumani.

Boris Yeltsin nae ni kiongozi alieshiriki kinagaubaga kuivunja USSR, ambapo mwaka 1991 alizungumza na viongozi wa nchi zote ndogondogo zilosalia zikiongozwa na Belarus na kufikia makubaliano yaloitwa Alma-Ata Protocol ambapo mataifa yapatayo 11 yaliafiki kujitenga na kuwa huru.

Mataifa hayo huru baada ya ilokuwa USSR yalikuwa ni pamoja na Belarus, Russia, Ukraine, Moldova, Kazakhstan, Azerbaijan, Armenia, Tajikistan, Krygzstan, Turkmenistan na Uzbekistan. Georgia haikushiriki mchakato huo.

Vitendo vya Gorbachev na Yeltsin viliwaudhi sana mazee wa KGB akiwemo Vladmir Putin ambae wakti wote huo alikuwa akifanyia kazi Ujerumani Mashariki akichunguza wageni wa kutoka nchi za magharibi.

Nafikiri ntakuwa nimekupa mwanga kidogo.
 
Habari zenu wenzangu wanaJF.

Habari zao wenyewe wanaopigana zinaonyesha hii ni vita moja ambayo sheria walizotutungia dunia wamezitupilia mbali. Yaani nahisi ndo kipimo cha chuki kilipofikia. Vikwazo vimevunja hadi sheria ndani ya nchi inayotoa vikwazo...
Habari za majeshi ndani ya mahospitali nk yanatokea mara kadhaa... hii ni kutumia raia kama kinga.

Hii vita pia inapiganiwa mtandaoni na kwenye vyombo vya habari - lengo kuu kulazimisha dunia kumchukia mrusi na kuunga mkono wa magharibi. Uongo mwingi sana tunatupiwa, usipochunguza unafuata mkumbo haraka sana manake mavideo na mapicha makali. Tunasahau photoshop nk

Nimemsikia mmarekani akitangazia dunia mrusi anataka kutumia silaha za kibailojia zaidi ya mara moja. Sikuelewa kwa nini hadi nilipomsikia huyu mbunge wa zamani wa Marekani akiongelea mitambo inayolipiwa labda hata kumilikiwa na mmarekani ya kutafiti silaha za kibailojia - kwa hiyo zimejaa madudu ya kuundia silaha hizo. Kama historia yake mmagharibi - ana uwezo wa kutupa yeye mabomu akimsingizia mrusi. Pia putin alivowashtaki wanatengeneza mabomu, walimbishia na kumbeza .... michezo ile ile michafu ILI sisi duniani tuwashangilie, kisa tunameza taarifa zao za habari kuliko za putin

Kwa kweli hii vita wamagharibi wamekuja na hisia na ubaguzi kuliko maarifa na uungwana. Hawaonyeshi kujali athari za kiuchumi duniani zinazosababishwa na ubishani ILA wanaonyesha kujali sana kutoa taarifa wanazotaka wao na kuungwa mkono kwa nguvu. Tafakari marekani na ulaya vitu vinapanda bei kama urusi walikompa vikwazo, serikali hazijali hilo - macho yameiva mekundu ni kutoa pumzi kali na hela kibao vitani.

Hawawajali watu wao sembuse sisi? Waafrika hii ni vita, sawa ya kuicheki na kuichora, ila tutajisaidia sana tukiamka tukalima ngano nyingi na mazao ya kutulisha... kuna njaa itakuja

View attachment 2154549
Tulsi Gabbard labeled a "Russian asset" for pushing U.S. biolabs in Ukraine claim

View attachment 2154552

Cry More
 
Habari zenu wenzangu wanaJF.

Habari zao wenyewe wanaopigana zinaonyesha hii ni vita moja ambayo sheria walizotutungia dunia wamezitupilia mbali. Yaani nahisi ndo kipimo cha chuki kilipofikia. Vikwazo vimevunja hadi sheria ndani ya nchi inayotoa vikwazo...
Habari za majeshi ndani ya mahospitali nk yanatokea mara kadhaa... hii ni kutumia raia kama kinga.

Hii vita pia inapiganiwa mtandaoni na kwenye vyombo vya habari - lengo kuu kulazimisha dunia kumchukia mrusi na kuunga mkono wa magharibi. Uongo mwingi sana tunatupiwa, usipochunguza unafuata mkumbo haraka sana manake mavideo na mapicha makali. Tunasahau photoshop nk

Nimemsikia mmarekani akitangazia dunia mrusi anataka kutumia silaha za kibailojia zaidi ya mara moja. Sikuelewa kwa nini hadi nilipomsikia huyu mbunge wa zamani wa Marekani akiongelea mitambo inayolipiwa labda hata kumilikiwa na mmarekani ya kutafiti silaha za kibailojia - kwa hiyo zimejaa madudu ya kuundia silaha hizo. Kama historia yake mmagharibi - ana uwezo wa kutupa yeye mabomu akimsingizia mrusi. Pia putin alivowashtaki wanatengeneza mabomu, walimbishia na kumbeza .... michezo ile ile michafu ILI sisi duniani tuwashangilie, kisa tunameza taarifa zao za habari kuliko za putin

Kwa kweli hii vita wamagharibi wamekuja na hisia na ubaguzi kuliko maarifa na uungwana. Hawaonyeshi kujali athari za kiuchumi duniani zinazosababishwa na ubishani ILA wanaonyesha kujali sana kutoa taarifa wanazotaka wao na kuungwa mkono kwa nguvu. Tafakari marekani na ulaya vitu vinapanda bei kama urusi walikompa vikwazo, serikali hazijali hilo - macho yameiva mekundu ni kutoa pumzi kali na hela kibao vitani.

Hawawajali watu wao sembuse sisi? Waafrika hii ni vita, sawa ya kuicheki na kuichora, ila tutajisaidia sana tukiamka tukalima ngano nyingi na mazao ya kutulisha... kuna njaa itakuja

View attachment 2154549
Tulsi Gabbard labeled a "Russian asset" for pushing U.S. biolabs in Ukraine claim

View attachment 2154552
Acha kulialia,sogezeni majeshi kyiv mpate dawa yenu.
 
Leta ushahidi wa hizo silaha kutumika nchini Ukraine.

Mpaka sasa kwa mujibu wa takwimu za CIA mpaka sasa Urusi imerusha makombora 800 kati ya hayo hakuna hata kombora moja lenye mlipuko wa uzito angalau wa kilo 500 wakati Urusi ina makombora yenye uzito wa tani 3.

Haya niambie Urusi akija kuanza kutumia makombora yenye uzito hata wa tani moja siya takuwa maafa?

Leo shirika la kijasusi la Uingereza ambao ni maadui wa Urusi wamekili ya kwamba Urusi inatumia silaha za kizamani ww unapinga kama nani?

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
🙂🙂🙂
 
Back
Top Bottom