Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Sawa bosi.
Akili yako inakutuma kwamba kila anayeomba LIFTI au msaada basi ANA SHIDA???
Kwako wewe ukiwa na gari huhitaji ushirikiano na watu wengine?
Msongamano upo kwenye gari tu? Nyumba za iibada je? Kila mtu awe na yake ili kuonesha hawana shida?
 
Mimi ni muwazi naongea as joking lakin namaanisha ningewaambia
Tatizo letu ni ujamaa, tunatamani kuishi kijamaa lakini dunia inatuendesha kibepari.

Kila mtu anataka ku-save pesa yake, ndio maana anakuja kuomba lift na kupata urahisi wa kufika anakoenda. Ila kiuhalisia kabisa ukipewa lift jiongeze, hata mgeni akija home utaishi nae kwa muda fulani, baada ya kipindi kirefu kupita utauliza vipi upo hapa kwa muda gani.
 
Kila mtu ni mnafique tu, watoa lift wanafiki...wanachekacheka ila moyoni hawana furaha, wapewa lift nao wanafique...anachekacheka ili mwenye gari yake awe huru.
 
We jamaa bana.
Tofautisha shida ya siku moja na watu kufanya mazoea. Yaani watu wafanye mazoea kuomba lifti nione sawa kwasababu nahitaji ushirikiano? Haipo hivyo ..shirikiana na mtu anayetaka ushirikiano na wewe, na utagundua kwamba kila mtu ana levels zake. Ni muda sasa umefika waomba lifti muanze kushirikiana mkusanyike pamoja kuelekea kwenye kituo cha daladala.
Au mnaonaje mkishirikiana mchange ili mrequest bolt?

Kanisani mtu unaenda bila kulazimishwa na mtu, kama mtu ataona hapendi msongamamo wa kanisani abaki nyumbani, haijawahi kuwa lazima.
 
Najua, haihusiani na hii mada.
Hao ninaowapa lift baadhi Wana uwezo kunizidi
Leo una gari lakini kesho unaweza usiwe nayo. Lakini hao unaotaka kuwanyima lift leo wanaweza wakawa na magari yao kesho. Unataka nao wakunyanyapae kama unavyotaka kuwafanyia?
 
Kwani nyie msio na magari hamuanguki huko maofisini?
Mkianguka mnasaidiwaje hadi huyo mwenye gari umwambie akianguka atasaidiwaje?
Acha ushamba kung'ang'ania gari kwa vitisho eti akianguka hamtamsaidia.
Unajua tukiwa wazima huwa tunakuwa wajuaji na wenye kujivuna sn, ila Mungu akikupa mtihani ndo utaona mali zote ulizonazo ni takataka tu, hata hilo gari wakikuambia uuze 1,000 km hauna namna utauza ili kuokoa uhai. Muhimu omba uwe mzima majigambo, fitina, starehe nk ni vitu vya muda tu.
 
Wewe utakuwa na roho mbaya mkuu. Huku Afrika siyo ulaya huwa tunashirikiana.
Mfano unatoka posta unaenda mbweni ukimpa lift mtu ukamuacha mwenge unapungukiwa nini hapo?
Mshamba na Limbukeni huyo.
Halafu unaweza kukuta ni mvivu wa kazi baadhi ya kazi anasaidiwa na wafanyakazi wenzie
 
Pole ukiwa na dharura au ishu nyingine mjibu huelekeo wako ni mwingine.

Kuazimana gari huo sio mchongo. Likiharibika utaambulia pole tu.
 
Unaogopa nini kuwaambia “HAPANA” wewe jilegeze tu wenzio wanakuona FALA TU . UJAMAA SHARI.
 
Aisee nibora ungetuchana ukwel tukiwa kazini kuliko kuja kutuanika huku hayo nimapigo ya kikee
 
Tena ingekuwa ni mara Moja,Sasa hivi wamegeuza utaratibu, utasikia "kaka twende ukaniache palepale pa Jana"
Na ukiwa na kazi zako ofisini usiombe usaidiwe hata kama umesafiri utazifanya mwenyewe acha ubinafsi gari lenyewe la mkopo, nani kakwambia ununue gari kwa mkopo? matokeo yake unakuja na makasiriko dhidi ya wafanyakazi wenzio
 
Yeah ni kuchangamsha maongezi tu hawa malimbukeni wanaomiliki magari ya mikopo wanasumbua sana
 
Hayo ndo madhara ya siasa za ujamaa kuomba omba kama masikini kwanini unataka mimi ni share "your poverty" kwa kunishirikisha umasikini wako.
Introduction of ujamaa village (ARUSHA DECLARATION) hapa ndipo shida ilipo anzia..

Ujamaa ni mbaya Sanaa.
 
Wewe utakuwa na roho mbaya mkuu. Huku Afrika siyo ulaya huwa tunashirikiana.
Mfano unatoka posta unaenda mbweni ukimpa lift mtu ukamuacha mwenge unapungukiwa nini hapo?
Wewe hauna gari ndio maana hauoni tatizo alilo wasilisha mtoa mada.....hizo tabia zinakera vibaya , kuna watu wamenunua private car sababu ya kulinda privacy zao nmk......kwahy naww kama unatabia kama hiyo nakusihi sana uache bora iwe inayokea mala moja moja mtu kakukuta njian na sio kumsubiri utadhan wewe haupokei mshahara
 
Yaani ulivyo boya unaona sawa tu, wafanyakazi wenzio kukujua kwamba ni mchoyo wa lifti,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…