Wewe ndio una imani potofu.!
habari za kitabu cha yesu ulisoma?
Unajua utabiri wa kuzaliwa yesu ilipita miaka mingapi utabiri huo utimie?
Unajua utabiri wa kuzaliwa na kufa kwa yesu vilitabiriwa Kwenye Biblia kabla hata yeye hajazaliwa?
Unajua hata kurudi kwake kulitabiriwa?
Mnachojua ni kukosoa kitu ambacho hamna hata ujuzi nacho.
Shida yenu na hii ni kwa watu wengi huwa mnasoma maandiko "literally" (mnatoa tafsiri za moja kwa moja) katika mandiko ambayo ni "metaphoricals" (maandiko yenye maana zinazohitaji ufafanuzi).
Kuhusu kuja (kushuka) kwa Yesu kutoka mbinguni, Yesu mwenyewe kisha tanzua huo mgogoro hapo kabla, kabla ya yeye mwenyewe leo kuhusishwa katika mgogoro wa aina hiyohiyo.
Wayahudi kabla ya yesu hajatokea waliamini kuwa Eliya (Elijah) alipaishwa na upepo wa kisulisuli (swirl wind) juu mbinguni na wakawa wakimsubiri ashuke kutoka huko kama jinsi wakristo wanavyomsubiri Yesu ashuke kutoka mbinguni.
Juu ya wayahudi kumsubiri Eliya ashuke soma (Malaki 4:5)
Na pia iliandikwa masihi Yesu hawezi kuja hadi Eliya ashuke kutoka mbinguni.
Yesu alipokuja na kusema kwamba yeye ndiye Masihi, wayahudi wakahoji yeye atakuaje ni masihi wakati Eliya bado hajashuka kutoka mbinguni??? Yesu akawajibu; Yohana (mbatizaji) ndiye Eliya mwenyewe aliysubiriwa kuja (kushuka) soma (Mathayo 11:14).
Sasa kwa mtu mwenye akili ya kujua maandiko ya kiroho ni kwamba; inaposemwa mtu fulani atashuka maana yake atakuja mtu mwingine mwenye mfanano wa kiroho na huyo anadhaniwa kwamba atashuka, kifupi ni kwanba mtu anayedhaniwa kwamba kapaa mbinguni sio kweli kwamba huwa amepaa bali hutokea sintofahamu kumuhusu huyo mtu, sintofahamu hiyo hupekewa kimakosa ukichukulia maanani kwamba maandiko yanayohusu kupaa kwao hayakuwa "protected over time".
Wayahudi waliamini/wanaamini Elijah yupo mbinguni na atashuka, Wakristo na Waislamu wanamini Yesu/Isa yupo juu mbinguni na atashuka siku za mwisho, Wahindu wanaamini Krishna atakuja kuokoa wahindu nk ilimuradi kila dini inaamini siku za mwisho atatokea mtu wao kuja kuongoza nk, dini zao.
Yesu alipokuja kuhubiri Injili kwa mayahudi (mathayo 15:24) alisema kuna kondoo si wa zizi hili nami yanipasa niwakusanye niwaweke chini ya mchungaji mmoja, swali je hao kondoo ambao sio wa zizi lile ni wepi???.
Yesu hakupaa mbinguni kidhahiri; ukisoma maandiko kipindi Yesu anaagana na wanafunzi wake baada ya kula naye samaki na wanafunzi walipothibitisha kwamba ni yeye kweli baada ya kuona majeraha yake ya kusulubiwa ndipo Yesu akaondoka kwenda nchi nyingine kwasababu mahali pale hapakuwa salama tena kwa maisha yake.
Kwanini imeandikwa alipaa mbinguni???----- sababu zipo mbili, 1-- ni kuficha ukweli kwamba Yesu alihama yeye na mama yake kwenda nchi nyingine lengo ni kuficha na kufanya wale maadui zake washindwe kumfuatilia. 2-- wanafunzi wake walitaka yesu aonekane kwamba mtu wa Mungu kama Eliya ambaye naye Wayahudi waliamini kimakosa kwamba yupo hai mbinguni. Ni katika mazingira hayo imani ya kupaa yesu ndipo ilipoingia ndani ya imani za wayahudi na kuendelea kuota mizizi hadi Injili zilipokuja kuandikwa miaka mingi baadaye na imani hiyo ikaingizwa katika baadhi ya injili hizi tulizonazo leo, Injili hizi ziliandikwa na watu mfano injili ya Luka ni waraka wa Luka kwa mfalme Theophile.
Historia ya Yesu katika injili inaishia pale "alipopaa" tu,
Historia ya Yesu inaanza upya pale alipohama yeye na mama yake kuelekea Kashmiri kuwafuata kondoo wengine wa Israeli ambao hawakuwa katika zizi lile la makabila ya Yudea na Benjamini, makabila mengine 10 ya Israeli yalikuwa yametapakaa huko Kashmiri, Afghanistan, na sehemu fulani za India.
Mama yake Yesu alifariki katika safari na akazikwa katika foot za milima ya Muree (milima hiyo imeitwa Muree kwa heshima ya huyo mama, Muree ni jina jingine la Maria au Mary).
Yesu aliendelea na safari hadi Kashmiri ambapo huko wanaishi waizrael na huko aliendelea kuhubiri injili hadi Mauti yalipomfika na kaburi lake lipo huko Srinagar mtaa wa khanyar, (read on Rozabal shrine). Wenyeji wa huko kashmiri ni 99.9% waisilamu kwasababu Yesu aliwahubiria wazee wao kuhusu ujio wa Mtume Muhammad (saw) na hivyo ilikuwa rahisi kwao kumtabua Nabii Muhammad (saw) alipotokea.
Kwa habari pana zaidi tafuta kitabu kiitwacho "Jesus in India".
By Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (as) of Qadian.
Yeye ndiye Yesu, Isa na masihi wa mfano. Yeye ndiye yesu anayesubiriwa kama jinsi Yohana mbatizaji alivyokuwa ni Eliya aliyekuwa akisubiriwa na Wayahudi.
Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (as) ni Muanzilishi wa jumuiya ya Waisilamu wa Ahmadiyya.