Kitendo cha kusema mwanamke apigwe ila asivunjwe mifupa hiyo sio sheria au taratibu ya kiislamu,kwasababu hapo kuna kipigo kikubwa kinyume na mafundisho ya kiislamu,ambayo yanaelekeza kumwadhibu kidogo pasina madhara makubwa kwenye mwili wake,na isiwe usoni,kwahiyo ifahamike kuna taratibu za kislamu na taratibu za hao wanaojifanya wanafuata Uislamu lakini nyuma yake wana agenda zao
Kwa sheria za kiislamu mwanamke once akiolewa anakuwa kwenye mamlaka ya mume,kwahiyo hata kwenda kwao inahitajika ruhusa ya mume,sio kujiendea tu, hata kama umefiwa unatakiwa upate ruhusa ya mume,kwahiyo wazazi ambao wanafahamu taratibu za dini hili kwao halina shida kabisa kwani wanafahamu I haki ya mume kutoa maamuzi,lakini haikusemwa kuwa akienda basi apigwe
Siku zote kupigwa ni hatua ya mwisho baada ya diplomasia kutumika na kushindwa kutoa matokeo chanya,baada ya mazungumzo ya mume na mkewe kushindwa,kutafuata mazungumzo ya mume na mkewe na ndugu wa panda zote mbili,hii yote ni kutafuta suluhu kwa njia ya amani kabisa