Tukiweka mihemko ya kidini pembeni hii sheria inahitajika sana Tanzania kuja kuirudisha jamii iliyopotea kwenye mstari.
Hawa jamaa tunawachukulia powa kwa sababu ya record zao mbaya sana lakini sheria kama hizi ni muhimu na nzuri sana.
Wazungu wameharibu dunia, yani mwanamke anapewa kipaumbele cha kwanza, halafu mtoto, anakuja mbwa then wewe Baba ni wa mwisho.
Hi mentality ya 50 kwa 50 ni upuuzi mtupu, ubatili na ukafiri.
Tusiangalie haya mambo kwa mlengo wa kidini, kama Waislamu wana sheria za kuionyoosha jamii kuirudisha kwenye mstari hivyo ndio vitu vya kuiga kutoka kwenye Uislamu.
Humu wengi ni mashahidi hata kifo cha member mwenzetu Le Mutuz kimechangiwa na mke wake na watoto wake mwenyewe kwa malezi ya hovyo ya Kikafiri Marekani.
Imagine mtoto wako wa kumzaa anakwambia "Kiss my di**" tena live kwenye mtandao utajisikiaje?
Hebu tuangalie Biblia inasema nini?
Mithali 13:24
Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.