ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
- Thread starter
- #21
Ndoa sio watu wote ni kwa ajili wa aminifuNdoa nyingi matatizo yake makuu;
1. Kutokufanana.
Unaoa au kuolewa na mtu ambaye hamfanani kifikra, kimaono, kimaadili, kimaumbike n.k
2. Wanawake kuolewa kama Ajira, nitoke vipi
Ni wanawake wachache wameolewa na wanaume wa ndoto zao. Hilo linapelekea matatizo ya ndoa
3. Matarajio ya wanawake na tamaa ya mafanikio.
Wanawake wengi huolewa wakiwa na matarajio kwamba maisha yatabadilika kwa haraka. Wengi sio wavumilivu.
Mwanaume anamtia moyo mke wake kuwa mambo yatabadilika na kuwa mazuri.
Mwanamke kutwa kulalamika kwamba mumewe mzembe, anamuona Hana jitihada.
Mwanaume anachoka, na anaamua kupata tulizo la moyo nje au kuwa chapombe.
4. Wanawake kujizira na kuwa wachafu.
Kulakula hovyo na kunenepeana hovyo.
Kutovaa nguo za mvuto.
Unakuta mwanamke wa miaka 30 kama Mzee vile.
Wanaume hatupendi wanawake waliojichokea, wasiojijali
Wengi wanasingizia uzazi.
Lakini mimi nawajua wadada wanawatoto mpaka wanne lakini wanavutia balaa.
Mazoezi hutaki kufanya, unakulakula hovyo unadhani sifa.
Haya usafi zero. Hapana
5. Hakuna kusema umemzalia mwanaume.
Mtoto huyo NI wenu wote. Hakuna uliyemzalia. Ni wako pia.
Wanawake wengi hufikiri kuzaa na mwanaume kunamuongezea pointi fulani. Nope! Kila mwanamke unayemuona barabarani anauwezo wa kuzaa na mwanaume wako. Tena wako wanawake wenye uwezo wa kuzaa mpaka mapacha.
Kuzaa ni jukumu lenu wote.
Kauli ya kusema nimemzalia ni kauli ya vita vya kisaikolojia ambavyo wanawake wengi huitumia kumfanya mwanaume asiyejielewa ajione ana msalaba, deni kwa mwanamke.
6. Kuhusu Tamaa,
Wanawake pia wanatamaa. Tena Siku hizi wanawake wanatamaa zaidi kuliko wanaume.
Ukitaka upime hilo,
Ipitishwe kampeni ya Kila Kaya DNA ni lazima. Kisha tusubiri matokeo. Utagundua kuwa kusema wanaume pekee wanatamaa ni mbinu tuu za kimedani wanawake wanazitumia.
Ukweli ni kuwa Wote(mwanamke na mwanaume) wanatamaa.
Na nikikusaidia tuu.
Kwa sasa ni ngumu kumkuta Mwanaume mwenye wanawake kuanzia wawili.
Ila ni rahisi kukuta wanawake wenye wanaume zaidi ya watatu tena wengine mpaka watano.
Ndoa ni kwaajili ya watu waaminifu wenye kupendana
Hao wanawake wenye wanaume watano wanyongwe