Tamaa, Usaliti na Matokeo Yake Wanaume na Wanawake Wengi Wanaharibu Familia Zao Wenyewe

ndugu wadau wa Jf katika jukwaa hile, naomba leo kutoa maoni yangu kwenye hoja hii mahususi mezani,
kwa kunukuu maneno machache tu kwenye wimbo wa kundi la Christ Saints wa Pale Rwanda, ambao unaitwa NDOA.

nanukuu,
"Ndoa ni mpango mtakatifu tangu mwanzo,
ujumbe mwema utokao kwa baba, yahitaji hekima kuitunza, hadi kifo kiwatenganishe,

Mke si kidude cha kujaribu miguu yako,
Mume si kipaza sauti cha kupigia kelele,
Mpendane, msichokozane,
Amani ya Bwana iwe ndani yenu,
Hiyo ni baraka yake Mungu amewakirimia"
Mwisho wa kunukuu.

Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu,
Mungu awabariki nyote.

Tuishi nao kwa akili 🐒
Ukituliza kicwa hua una hoja kwa mbaali🐒
 
Sintawahi✖

Sitawahi✔

Hua✖

Huwa✔

Hapo pia umekosea.
shukrani mwalimu wa fasihi kwa masahihisho mujarabu ya makosa ya kimuundo na silabi katika lugha adhimu sana ya Kiswahili.

mnafanya kazi nzuri sana ndugu walimu.
well done 👊
 
Kuna wanaume Mungu kawajalia familia nzuri sana mke mwema, anayejitunza, anayeheshimu ndoa yake, anayekutii na kusimama kwenye nafasi yake kama mke.

Pengine amekuzalia watoto na amekuwa nawe kipindi kigumu na chepesi.

Lakini kutokana na tamaa, unaanza kuchezea amani ya familia yako mwenyewe.
Unaingia kwenye umalaya wa wazi wazi bila hata kujificha, ukiwa na ego kubwa kwamba hakuna atakayekufanya chochote

Sasa hapo mwanamke kakufanyia nini mpaka umtendee hivyo?

Tatizo kubwa si tu kucheat
Tatizo ni dharau, maudhi na mabadiliko ya tabia baada ya kupata (nyama mpya)huko nje

Na unataka mke aendee kukuheshimu kama zamani wakati wewe mwenyewe umebadilika
Heshima haiji yenyewe, heshima inatengenezwa

Kama zamani ulikuwa unaheshimiwa, basi jiulize: nini kimebadilika?

Kwa nini leo unaonekana wa kawaida tu machoni mwa mke wako?
Huenda ni tabia zako mpya dharau, ukali, kiburi na kutothamini familia

Lakini pia nisieleweke vibaya sizungumzii wanawake wenye tabia mbaya, wenye matusi, visirani na gubu kupitiliza Hapana

. Nazungumzia mwanamke mwema ambaye anajitahidi kuijenga familia lakini bado anatendewa vibaya.
Wanasema mshahara wa dhambi ni mauti.

Na kuna kisa nilikishuhudia karibu kabisa kwenye familia
Kuna dada mmoja alikuwa na maisha ya kudanga sana Akapata mimba ya kwanza, mwanaume akamkimbia na kumuachia mtoto
Hakutulia, akapata mimba ya pili, akaolewa haraka haraka kuficha aibu ya ujauzito, lakini ndoa nayo haikudumu akaachika akiwa na mtoto mwingine
.
Bado hakutulia.
Akabeba mimba ya tatu. Siku moja akaja kwangu baada ya swala ya Magharibi. Akanambia:
Mdogo wangu, nimejifunga
Lakini hakuwa na furaha hata kidogo. Nilipomuuliza kulikoni, akasema hajui mimba ni ya nani kwa sababu alikuwa ametembea na wanaume wawili kwa nyakati zinazokaribiana

Tulivyohesabu tarehe, ikaonekana wazi mimba ni ya kijana mmoja wa kawaida anayejitafuta. Lakini yeye alitaka mimba ihesabike kwa mwanaume mwingine mume wa mtu mwenye pesa

Bahati mbaya kwake, yule mwanaume mwenye pesa alikataa na hata akatoa pesa mimba itolewe

Mimba haikutolewa
Mwisho wa siku yule kijana wa kawaida akaambiwa ndiyo mwenye ujauzito na akakubali

Lakini baadaye wakaja kuachana.
Cha kushangaza zaidi, mimba ile ile ikapewa mwanaume mwingine 🙌

ambaye hata hakuhusika kabisa kwenye huo mchezo
Na kwa sababu ya upendo au ujinga, akaikubali mpaka akaanza kuhangaika na majukumu ya mtoto ambaye si wake

Leo hii huyo mwanaume amemuoa kabisa last kama mke wa pili

Nilipomuangalia siku ya harusi nilihuzunika sana
Nikajiuliza
Kama huyu mwanaume angeweza kutuliza tamaa zake na kuwa makini, angejikuta kwenye hali hii kweli?

Kwa sababu wakati mwingine tamaa na uzembe vinaweza kukufanya ubebe majukumu ambayo si yako, huku ukiwaumiza watoto au familia yako halisi

Swali langu kwa wanaume ni hili:
Una uhakika huyo mtoto unayemhudumia ni wako?
Pima hata DNA 🤪

Na kabla hamjaharibu familia zenu kwa tamaa za nje, kumbukeni kuwa amani ya nyumba hujengwa kwa uaminifu, heshima na kujitambua si kwa starehe za muda mfupi

ShesRise_1 👋
Aiseee 🤔

Issue wife anafuatilia sana simu yangu..soma sana meseji na chats mbali mbali ana screen shot anabaki NAZO.

Now tumekua na mgogoro kiasi...ILA NAMPENDA WIFE SANAAAAAA.. Tumejaliwa watoto wa wili wazurii stili ni wadogo..

For sure nili cheat akanishika through SMS na mchepuko ikawa noma.

Leo asubuh naona anaongea na SIMU kwa kujibebisha pia kwenye profile ya simu kamuweka mkaka nisiye mfahamu namuuliza anajibu juu juu..

Natamani kurudisha mapenzi ya mwanzo upendo wake now naona umekua DISGUISED
 
*

Mimi sio mwalimu ,huo ni muundo wa herufi za darasa la tatu , kiufupi huko shule ulienda kusomea ujinga.
 
Aiseee 🤔

Issue wife anafuatilia sana simu yangu..soma sana meseji na chats mbali mbali ana screen shot anabaki NAZO.

Now tumekua na mgogoro kiasi...ILA NAMPENDA WIFE SANAAAAAA.. Tumejaliwa watoto wa wili wazurii stili ni wadogo..

For sure nili cheat akanishika through SMS na mchepuko ikawa noma.

Leo asubuh naona anaongea na SIMU kwa kujibebisha pia kwenye profile ya simu kamuweka mkaka nisiye mfahamu namuuliza anajibu juu juu..

Natamani kurudisha mapenzi ya mwanzo upendo wake now naona umekua DISGUISED
Kwahiyo wewe kuchati na mchepko ukafuta sms unashindwa ?
Mpka unafumaniwa ?
Huoni kama dharau hizo

Yaan mimi kuni cheat sio shida kubwa shida mpka nakufumania nahesabu ni dharau sana
 
*
Na kabla hamjaharibu familia zenu kwa tamaa za nje, kumbukeni kuwa amani ya nyumba hujengwa kwa uaminifu, heshima na kujitambua si kwa starehe za muda mfupi
Baba angu mzuri 😍 AKA Gen-Z
 
Tamaa na usaliti ni saratani ya kiroho inayomomonyoa misingi ya familia nyingi leo.

Maandiko matakatifu yanatubainishia wazi kuwa moyo wa mwanadamu ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, na usipolindwa, tamaa huingia na kuzaa dhambi.
Wakati wanandoa wanapoacha kutazama viapo vyao vya madhabahuni na kuanza kuendekeza macho na hisia nje ya ndoa, wanaruhusu adui aharibu kile ambacho Mungu amekiunganisha.

Huu si tu usaliti kwa mwenza wa maisha, bali ni uasi dhidi ya agano takatifu lililowekwa mbele za Mwenyezi Mungu.Matokeo ya usaliti huu ni laana inayofuta baraka, amani, na utulivu ndani ya nyumba. Biblia inatukumbusha kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti," na katika muktadha wa familia, mauti haya yanajidhihirisha kupitia kufa kwa uaminifu, upendo, na furaha. Watoto ndio wanaoumia zaidi kiroho na kisaikolojia, wakikua katika mazingira yasiyo na ulinzi wa kiungu kwa sababu ya ubinafsi wa wazazi wao.

Nyumba iliyokuwa madhabahu ya sifa inageuka kuwa uwanja wa vita vya kiroho, vifo vya mapema, magonjwa, na umaskini wa ghafla unaotokana na kupoteza kibali cha kiungu.Ili kunusuru jahazi hili linalozama, ni lazima wanandoa warudi kwenye toba ya kweli na magoti ya maombi.

Uponyaji wa familia hauji kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa kumwalika Roho Mtakatifu atawale mioyo na kuleta roho ya kusamehe. Kila mmoja anapaswa kulinda malango ya moyo wake kupitia neno la Mungu na kujenga kuta za uaminifu zinazozuia mishale ya adui.

Kuridhika na kile Mungu alichokubariki nacho na kuishi kwa hofu ya Mungu ndiyo ngao pekee itakayolinda ndoa yako dhidi ya dhoruba za tamaa za kidunia.
 
Back
Top Bottom