Kweli mkuu
 
Tunaomba namba yako ya simu kwa ufatiliaji na hatua zaidi
Kwanza, Naomba niwapongeze TANESCO kwa ushirikiano mkubwa ambao mmekuwa mkiutoa katika Jukwaa hili.

Pili niliuliza suala la TANESCO ambayo IMETWAA NA KUZUIA uendelezaji wa maeneo ya watu wa MSALATO bila kuwalipa FIDIA TANGU 2018. (#6802)

Jibu nililopewa nimeambatanisha katika ujumbe huu.

Kumekuwa na Danadana na kutupiana mpira Kati ya JIJI LA DODOMA na TANESCO DODOMA.

Kwa ajili ya ufuatiliaji naomba niweke namba za wahusika wakuu.

KUTOKA JIJI LA DODOMA: STEVEN MWAKASITU - 0714 223 159

KUTOKA TANESCO DODOMA: NDUGU TABU - 0789 383 199

NAAMINI SUALA HILI LITAFUATILIWA.


AHSANTENI.



Sent using Jamii Forums mobile app
 


Kwann Mameneja wa Tanesco wilaya wana kiuka kauli ya waziri wa Nishati na Umeme. Waziri anasema nguzo za umeme ni bure lakini mameneja wanatoza gharama za awali. Nimeomba umeme tangu last year mpaka leo napigwa dana dana tu. Mara kwa sasa tumesitisha huduma mpaka kauli ya serikali. Sasa sijajua ni kauli gani ya serikali zinatakiwa.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wanabodi Salaam!

Juzi nilisikia kiongozi mmoja wa serikali akijimwambafai kwamba watakao uza nguzo za TANESCO wachukuliwe hatua mara moja. Sasa tunakuja na Case study ya Halmashauri ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma ili sasa tujiridhishe tatizo ni TANESCO , au SERIKALI au wafanya kazi wa Tanesco.

Kwa sasa hivi ukifika ofisi hii ya TANESCO mara baada ya kufanya wiring na kuomba wakuwekee umeme, utakutana na options mbili na kuombwa uchague moja kwa hiari yako.
1. Lipia nguzo kwa utaratibu wa awali au
2. Usubiri utaratibu wa nguzo za bure mpaka utakapo tangazwa uje.

Ndugu zangu katika muktadha huo, unaambiwa kabisa kwamba nguzo ni bure ila nao wanasubiria waraka au tamko rasmi, hivyo kama una haraka, basi lipia nguzo ufungiwe mapema.

Sasa naomba majibu haya kutoka TANESCO , Wizara ya Nishati na Madini dr medard Mapogolo Kalemani na Serikali yetu pendwa ya CCM.

Je,
1. Ni kweli mpaka sasa sera yenu ya Umeme bado haijatamka wazi kuwa nguzo ni bure na watu wapewe katika ofisi za wilaya?
2. TANESCO mnajua kwamba nguzo bado zinauzwa kwa sababu ofisi zinasubiri maelekezo yenu ya nguzo za bure?
3. Serikali haina vijana wa Usalama wa Taifa au TAKUKURU kwenye ofisi za Tanesco ili kuthibitisha hili na kuondoa Urasimu?
Nimeongea hili ili KUONDOA LAWAMA kwa watumishi wa Tanesco huko ofisini maana wananchi wanaishia kuwalaumu wafanya kazi wale wakati pengine tatizo lipo kwenye uongozi wa juu.

Kama hili halitatatuliwa mapema, tutaendelea kuwatwisha mzigo mzito wa lawama hawa watumishi kwamba ni wezi na wababaishaji kwa maana mpaka sasa inaonekana matamshi ya wanasiasa yanaenda tofauti na uhalisia kule maofisini.

Sasa, je ni nani Muongo kuhusu utaratibu kati ya TANESCO na SERIKALI?
Wasalaam
Kidudu.
 
Naomba mwongozo wa viwango vya yuniti za luku maana nimebadirishiwa mita na bei za yuniti zimekuwa juu sana wakati matumizi yangu yalikuwa chini ya 10000 kwa mwezi
 
Tatizo la umeme mkoa wa Morogoro Kata ya Mkundi Mtaa wa Mlimani shida ipo wapi kutuletea umeme tuna shida ya umeme sana kila mwaka mnatudanganya mnaleta nguzo lakini ni uongo mtupu. Mnakwama wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
E eneo lako, wilaya na mkoa wako. Pia tutashukuru kupata namba ya simu yako..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umekua kama mchezo sasa kwa tanesco mkoa wa Arusha kukata umeme kila siku kuanzia SAA 1 usiku na kuurudisha SAA tatu usiku.

Jambo hili limekua ni kero.sasa.nakupelekea usumbufu mkubwa kwa wananchi na wakazi wa maeneo ya.kwamrefu. mpaka tengeru naomba Ndugu waziri ufatilie jambo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco imekua jipu kila mahali nchini kuna malalamiko wakati hata mabwawa yanataka kupasuka sijui wana shida gani nafikiri Mheshimiwa Rais afumue tena wizara na menejiment ya Tanesco wamejisahau mno, na hata wakilalamikiwa vipi hata kujibu tu malalamiko hakuna, kiufupi hawajali
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama atasikia kilio chako kuhusu Arusha basi akumbuke kwenda Kisarawe maana maeneo ya Chanika yanayohudumiwa na TANESCO Kisarawe hukosa umeme kila siku iendayo kwa Mungu... Narudia tena kila siku hao jamaa wanatuingiza hasara pamoja na kupokea malipo kwa wakati.
 
Mimi nimewekewa umeme tar 26/1/2020 nikaambiwa mita yangu itakuwa tayari kununua umeme baada ya kama siku 3 hivi tena wala sina haja ya kufika Ofisi za Tanesco! lakini sasa ni wiki ya 3 hii siwezi kununua umeme, nimekwenda ofisini mara ya kwanza wakanambia file langu halionekani lkn wanashughulikia same day itafunguliwa! lkn hawaikufungua, nimeenda tena leo nimeambiwa hivyohivyo kuwa leo nitaweza kununua umeme lkn hola! sasa naomba mnifungulie mita yangu ni 37216217952 nipo Tanga mjini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO mimi niko umbali wa kilomita 3.5 kutoka centre ya umeme nahitaji kuunganishiwa umeme.
Nifungue karakana ya mbao na Mashine ya kusaga.

Je naweza kupata hii huduma au kwa umbali huo siwezi kuunganishwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…