Wanabodi Salaam!
Juzi nilisikia kiongozi mmoja wa serikali akijimwambafai kwamba watakao uza nguzo za TANESCO wachukuliwe hatua mara moja. Sasa tunakuja na Case study ya Halmashauri ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma ili sasa tujiridhishe tatizo ni
TANESCO , au SERIKALI au wafanya kazi wa Tanesco.
Kwa sasa hivi ukifika ofisi hii ya
TANESCO mara baada ya kufanya wiring na kuomba wakuwekee umeme, utakutana na options mbili na kuombwa uchague moja kwa hiari yako.
1. Lipia nguzo kwa utaratibu wa awali au
2. Usubiri utaratibu wa nguzo za bure mpaka utakapo tangazwa uje.
Ndugu zangu katika muktadha huo, unaambiwa kabisa kwamba nguzo ni bure ila nao wanasubiria waraka au tamko rasmi, hivyo kama una haraka, basi lipia nguzo ufungiwe mapema.
Sasa naomba majibu haya kutoka
TANESCO , Wizara ya Nishati na Madini
dr medard Mapogolo Kalemani na Serikali yetu pendwa ya CCM.
Je,
1. Ni kweli mpaka sasa sera yenu ya Umeme bado haijatamka wazi kuwa nguzo ni bure na watu wapewe katika ofisi za wilaya?
2.
TANESCO mnajua kwamba nguzo bado zinauzwa kwa sababu ofisi zinasubiri maelekezo yenu ya nguzo za bure?
3. Serikali haina vijana wa Usalama wa Taifa au TAKUKURU kwenye ofisi za Tanesco ili kuthibitisha hili na kuondoa Urasimu?
Nimeongea hili ili KUONDOA LAWAMA kwa watumishi wa Tanesco huko ofisini maana wananchi wanaishia kuwalaumu wafanya kazi wale wakati pengine tatizo lipo kwenye uongozi wa juu.
Kama hili halitatatuliwa mapema, tutaendelea kuwatwisha mzigo mzito wa lawama hawa watumishi kwamba ni wezi na wababaishaji kwa maana mpaka sasa inaonekana matamshi ya wanasiasa yanaenda tofauti na uhalisia kule maofisini.
Sasa, je ni nani Muongo kuhusu utaratibu kati ya
TANESCO na SERIKALI?
Wasalaam
Kidudu.