Hii namna ya kukata elfu moja kila mwezi nyie Tanesco kwani mmebadilisha utaratibu? Inakuaje nanunua umeme mnanikata elfu tano badala ya elfu moja naomba ufafanuzi kama kuna mabadiliko yoyote mana sielewi.
 
NEW CONNECTION, MKOA WA DAR ES SALAAM
Naomba kufahamu bei halisi ya ufungaji wa umeme kwa mteja mpya ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
 
...Ninasikitika Sana kwamba Jana Jumapili nimenunua Umeme wa Shilingi Alfu SITA (6,000/=) hapa Mombo, Korogwe ili kuweka katika Luku yangu ambazo ni zile za Kimashine Cha Mkononi lakini kimekataa kuingiza umeme huo.
Nimehangaika kutoka saa 10 alasiri Kwa kupiga Namba Zote Tatu za Dharura za Mkoa wa Tanga ambazo mmeziweka humu JF.
Mbili zimefungwa na Moja ilikuwa Bize saa Zote. Nikajiuliza Sana hizo mbili mmeziweka za Nini, wakati hamjazilipia na zimekatwa !

Hio Moja iliyokuwa Bize saa zote kwenye saa Mbili Usiku na pamoja na kukuambia aliyenijibu kuwa Niko tayari kuleta token zangu Ofini ili aniwekee maana nilikuwa na Mgonjwa na isingekuwa jambo Zuri kulala na Giza, Nikashangaa Sana Mhusika aliponiambia Kituo Cha Mombo Siku za Jumapili kinafungwa saa Moja Usiku na sitapata Huduma yoyote Hadi Jumatatu.

Kwa hiyo nikiwa Hatua chache TU kutoka Ofisi yenu ya Tanesco Mombo, nimelala Giza na Tanesco imeshindwa Kunipa Msaada pamoja na Kuwa na Token! !
Mpaka saa TISA NA ROBO HII USIKU NIANDIKAPO UJUMBE HUU NIKO GIZANI I NA MGONJWA WANGU ANASUMBULIWA NA MWANGA HAFIFU WA MISHUMAA AMBAO NIMELAZIMIKA KUINUNUA TOKA JANA USIKU, UNAMUADHIRI MGONJWA WANGU.

NAULIZA TANESCO, IMEKAAJE HII ???

Namba yangu ni Vodacom 0754 340606
 
Ni Siku ya Pili Sasa Ninalala Giza na Kituo Cha Tanesco Mombo hakuna Wafanyakazi wa Emergency.....!
 
Ni Siku ya Pili Sasa Ninalala Giza na Kituo Cha Tanesco Mombo hakuna Wafanyakazi wa Emergency.....!
3o64528 Imenibidi Michele TU Kwa Uchungu.
Tatizo langu la kukosa Umeme kutoka a na Luku yenunkuwa Mbovu niliripoti saa 11 na Moja Jioni na kupewa namba 3064528 ya Tatizo langu.

Cha Ajabu Sana mmlinitumia Ujumbe saa Moja na Robo usiku kuwa Tatizo langu namba 3064528 limeishanyiwa Kazi na mkanitumia Link mbovu niijaze kupima Utendaji Wenu, nikiwa Bado Niko GIZANI Mpaka Sasa Hivi Jumatatu saa 3.00 asubuhi NIANDIKAPO UJUMBE Huu!

Tatizo limeishanyiwa Kazi wakati Niko GIZANI ??
Ina maana mmewasiliana na fundi Wenu wa TANESCO Mombo na akawakikishia kwamba ameishalifanyia Kazi wakati Sijaona Fundi hapa na Bado Niko GIZANI ?

Yaani token ninunue Mwenyewe, Luku yenu ishindwe Kupokea Token yangu halafu fundi aseme kuwa ameishalifanyia Kazi ??

Je ndio namna Mafundi Wenu wanavyotaka Rushwa Kwa WATEJA Wenu ?
Tafadhali zungumzieni na Mafundi Wenu wa TANESCO Mombo nipate Umeme Leo.
Sio Hisani. Ni w Wajibu Wao, nimelipia.
 
Nyie TANESCO mtaendelea kukata umeme mpaka mwaka gani?

Kil siku ni kukata umeme tu tokea awamu ya 2 ya Mzee Mwinyi.
 
NYUMBA MOJA KUWA NA MITA ZA UMEME ZAIDI YA MOJA.

.Kwenye media inazungumzwa kuwa nyumba ikiwa na mita zaidi ya moja basi mteja afike TRA kuomba kuondosha kodi ya pango ya kila mwezi na kubakisha kwenye mita moja. Lakini tukienda tra kuomba kuondoshewa wanakataza.
 
Kwa nini hizo nguzo zenu za concrete mlizikubali ili hali hazina nondo kwa hiyo kwenye tension zinafeli na kupelekea kuvunjika hovyo je wahandisi wenu wamechukua hatua gani
 
Habari TANESCO. Kita mpya inagoma kununua LUKU. Shida inaweza kuwa nini? Tumejaribu kwa voda na tigo imekataa
 
Hbr, tng jana nikiwasha kile kidude cha kuingiza luku inajiandika 888888888888. Sa sijui itakua na shida gn jmn
 
Kiukweli tanesco mmekuwa ni moja ya shirika ambalo linawafanya baadhi ya watanzania kuishi kwa maumivu na uchonganishi baina ya jirani na jirani.

Kwa mfano mtu anahitaji huduma ya umeme halafu labda nguzo zipo mbali na jengo lake itahitajika anunue nguzo kutoka tanesco kuanzia moja hadi mbili. Kumbuka huyu mteja atatoa kiasi hicho cha pesa ili apate huduma labda eneo hilo bado kuna wengine hawajafikia hatua ya kuweka umeme. Na huwezi kumwambia jirani achangie nguzo na wakati wa yeye bado hajajipanga kutoa hiyo pesa. Sasa mteja analipia kiasi alichoambia then analetewa huduma.

Sasa tatizo linaanza hapa. Hawa ambao hawachangia chochote kwenye hizo nguzo utashangaa wanaonganishiwa bila gharama yeyote ya nguzo. Na cha kushangaza zaidi ukiuliza unaambiwa nguzo ni mali ya tanesco, kiukweli hili ni tatizo.

Kwa ushauri wangu mdogo tu tanesco wngefanya ili kuondoa chuki na kuumizana baadhi jirni na jirani wangeteneza mfumo kuwa ili upewe huduma ya umeme kupitia nguzo ya jirani aliyochangia ni vyema uombe ridhaa ya barua kutoka kwa jirani yako aidha kwa kuchangia robo ya pesa aliyotoa jirani yako umpe jirani yako aliyotoa mpaka hiyo nguzo ikafika hapo.

Hii ingefanya watu wengi sana kuvuta umeme. Lakini utaratibu tanesco wanaoufanya si sahihi.....Yaani kila jirani anaetaka kuunganishiwa umeme alipe robo ya pesa ya nguzo moja apewe yule jirani aliweza kulipia nguzo zikafika au ikafika hapo.
 
Noted, Hui ni kweli kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…