TANESCO wapata hitilafu katika mfumo wa kununua umeme wa LUKU
.keshaliwa kichwa MTU huku
FB_IMG_1621424196478.jpg
 
Umeme huku kijini Kimokela, hakipatikani tokea Jumapili, na sasa hakuna hata nyumba moja iliyo na umeme, kumekuwa kiza.

Maisha haya hatujawahi kuyaona, biashara zimelala, wale wa juice wanamwaga zimechacha, wamiliki wa saloon nao wamelala tu, mashine za kukoboa na kusaga zimezima shida huduma ya luku haipatikani, mitandao yote holaa!

Kutokea kijijini kwetu kwenda (W) kufuata huduma hii ni kilomita kadhaa na ni gharama.

Leo ilikuwa ni fursa nzuri Kwa Mheshimiwa kulikemea hili Wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa na kuagiza lifanyiwe kazi mara moja na huduma hii irudi ndani ya masaa kadhaa, wabongo sio wa kubembeleza Mh Rais.

Unajua, ukiwa na watoto, au mke, kuna vitu ambavyo huwa wanataka wakujaribu kama baba ili kuona unaudhafu gani na baada ya hapo watakuwa wakifanya mambo Yao bila wasi Kwa sababu walishaona udhaifu wako.

Na ndicho kinachofanyika Kwa Baadhi ya watumishi hawa, na hivi vitu visipokemewa, baada tu ya muda utasikia mtambo Fulani wa kuzalisha/kupozea umeme umebasti, kumbe, kunachezwa madili, siku si nyingi Karikoo Majenereta yataenea.

Ukifanya kazi na wabongo, wengi wao ni wa kuburuta Kwa nguvu Kwa maana wanapenda bata zaidi kuliko kazi.

Wasaidizi wa Mh Rais wawe wanamkumbusha mambo hayo ili ayakemee, maana kwake kusahau ni kawaida Kwa Sababu ya majukumu Mengi.
 
Tatizo la umeme limenifanya nimkumbuke mzee baba, kweli atakumbukwa kwa mengi
 
Hata wilayani makao makuu ya Tanesco hakuna huduma...usihangaike kwenda mkuu!
 
Foleni ya kununua umeme na bado watu wanamiminika
20210519_164927.jpg
 
Back
Top Bottom