Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Mawazo ya mtu mfu yaan wewe ulimwengu unaenda kasi wewe unarudi nyuma. Kuna mtu ulikua unamnunulia bando kuchat ama kuingia kwenye mitandao kwa mtu kunakuhusu nn km sio roho mbaya tu sijui mitanzania km hii yenye roho mbaya imekuja km mikimbizi ......
 
Watanzania hatuna umoja Wala msimamo. Tuamue kutoweka bando kwa wiki nzima. Tanzania gharama za vifurush n kubwa sana
 
Kwl afanye hivyo tenha harak
 
wi-fi zinazo tumia maji au?
 
Angekuwepo Magufuli haya mambo ya bei ya bando kupanda yasingekuwepo.Lakini kwa kuwa mwendazake hayupo hakuna yeyote mwenye hofu na serikali.Inasikitisha sana.
 
Waziri ametuingiza mkenge mbaya.
#NDUGULILE OUT
 
Wewe ni Tahira.
 
Waziri ametuingiza mkenge mbaya.

#NDUGULILE OUT
kosa pesa ya kununua.

Wananchi wanaposikia watu wanakandamizwa na wenye mamlaka huwa wanajitenga kama haliwahusu, sasa leo hili la bundle limewahusu onyesheni kuwa nyie ndiyo wenye nchi.
[/QUOTE]
Iwe ya msingi au la hilo haliwahusu serikali. Ni swala binafsi na katika Technological age tuliopo sasa ka dunia ilipaswa internet iwe service ya lazima kama tulipavyo maji ama umeme tu. The internet infrastructers was supposed to be one of the key goals kuhakikisha wananchi wako updated in real time kwa gharama nafuu...

Badala yake serikali imegeuka wakala wa unyanyasaji wa kimtandao.
 
katika hili la kupandishwa kwa gharama za vifurushi wa kilaumiwa ni mwendazake na matamko yake.

mwendazake alikuwa hapendi kukosolewa, alionyesha chuki kwa watu waliokuwa wanamkosoa kupitia mitandao ya kijamii. akafika hatua ya kutamani malaika washuke wazime mitandao yote.

washauri wake kwa kutambua chuki ya boss wao kwa mitandao, wakaona bora wamfurahishe, wakaja na idea za kutumia vpn kwa upande wa twitter (japo haijasaidia) na kuongeza gharama za vifurushi.

matokea ya idea hizo ndio hii bei mpya ya kikatili ya vifurushi ambayo imekuwa gumzo siku ya leo.

ndungulile na team yake walisukumwa zaidi na utashi wa kisiasa kuliko utu ili wamfurahishe boss wao(mwendazake).

nina imani kubwa na mama samia. najua atafikishiwa malalamiko ya hii bei mpya ya vifurushi ambayo sio rafiki kwa mwananchi mwenye kipato cha chini. hapana shaka mama
atatoa amri ya kufutilia mbali.
 
Ndugulile sijui ndungulile alipotoa wazo la kuweka gharama kwenye WhatsApp call nilijua kinachofuata huyo jamaa ni mjima kinyama kwa zama hizi hatakiwi kuwa na matamko ya aina hiyo...
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Huenda wameona mawasiliano sio basic need!

Hivyo wanataka kubadili tabia, kutoka ktk kutumia rasimali zetu katika masuala yasiyo ya msingi.
Mkuu, sio basic need kivipi?πŸ™„

Kuna watu wanatumia mitandao kwa masomo, utafiti, biashara, ajira, kazi, nk nk..

Mtu anaweza kuwa Katavi huko, akawa anafanya kazi kwenye kampuni moja au kadhaa US au Europe na anaendesha maisha vizuri tu.

So, kwa sasa internet ni zaidi ya basic need kwa baadhi ya watu, tena wengi. Ukiminya huko unakuwa unanyonga watu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…