Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

2GB ilikua inauzwa Sh 2000 kwa sasa ni 1 GB kwa Sh 2000.
 
Nao wana mabadiliko hiyo tarehe?



Yeap, kesho wanatoa bando mpya... Stay tuned

Sent from my M2010J19CG using JamiiForums mobile app



Tigo tanzania baba la maajabu Wanafatilia comment zenu taratibu
Kabla ajaangusha BOM la atomic hapo kesho kutwa mapema

Kwa mujibu wa chini ya kapeti
Wapo kwenye kikao cha dharura na VODA
kabla hawajaja na maajabu yao ya vifurushi FUNGA KAZI
Ambapo tutalia na kusaga meno
 
Asilimia 50% ya maisha ya mwanadamu yanategemea mitandao: Mitandao ni kama chakula (Basic Commodity) hivyo hautakiwi kuwa wa gharama hata kidogo.

Pili, hili suala la sisi kununua vifurushi halafu wanatuwekea masaa ya kuvitumia na kupunguza kasi siyo sahihi na ni wizi wa nje-nje. Bando la mtandaoni ni mali yako binafsi kama mali nyingine, tofauti ni kwamba ile mali haishikiki (Intangible Property) kama mali nyingine. Kisheria naweza kuita hizi bando za mtandao INCORPOREAL PROPERTY, hivyo unavyolipia bando unafanya mabadiliko ya mali yako (Conversion of property from Corporeal to Incorporeal Property) ambayo ni pesa kwenda kwenye mali nyingine ambayo ni vifurushi vya mtandao.

Hili halikuondolei wewe umiliki, ila kinachofanyika ni kwamba hawa Internet Service Providers kama TiGO, Vodacom, Airtel, TTCL na Zantel wanafanya kazi ya kukuwezesha kutumia hiyo mali yako vizuri (They give you a platform in cyberspace). Bando siyo mali ya Internet Service Providers ni mali yako binafsi na wao kazi yao kubwa ni kukuwezesha wewe kutumia vizuri maana pia unalipa na VAT kwa ajili ya ile huduma.

Mfano unavyonunua HISA (Shares) kwenye kampuni, unalipia pesa ambayo hubadilishwa kuwa HISA, lakini zile HISA haziwi mali ya kampuni bali mali yako wewe unayelipia. Kwanini TCRA wanaacha sisi tunaporwa mali zetu kinyemela na hii mitandao ambayo wamiliki wake ni vigogo wakubwa ambao wengi hutoka CHAMA TAWALA ???

Kisheria tunasema They are in position of Trust, hivyo hawatakiwi kabisa kupunguza kasi ya mtandao, wala kubadilisha gharama zake bila kuwataarifu wateja au kuwawekea wenye mali muda wa matumizi usioeleweka (Unreasonable Time) maana bando siyo mali yao bali mali ya mteja. TCRA wapo tu, kazi yao kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya kwa miaka hii mitano iliyopita ni kuminya uhuru wa kujieleza na kufuatilia watu wanaokosoa serikali, lakini mambo ya msingi kama haya hawayafuatilii kabisa. SIJUI TATIZO LIKO WAPI !!!

Manunuzi ya vifurushi vya mitandaoni hayana tofauti na matumizi ya huduma za benki, ambapo mteja unaenda kuweka pesa zako kwao lakini haziwi za kwao bali za kwako. Wao kazi yao ni kuzitunza, kuzizungusha na kukupa wewe riba: Hawatakiwi kuzigusa wala kuzifanya chochote bila idhini yako. Hivi ndiyo ilitakiwa ifanyike kwenye vifurushi maana tunabadilisha pesa zetu kwa matumizi mengine na hatuwapi hawa Internet Service Providers.

THIS IS PURE EXTORTION AT IT'S BEST....................
 
Zantel kwa buku nilikuwa napata 1GB kwa siku 3 saivi imekua 450MB [emoji45] [emoji45] .natamani kuhama ila nasubiri kwanza.
Huku halotel nilikua napata 3GB kwa ef3 kwa week zima

Sahivi 1.3GB kwa ef3[emoji2297]
 
Vodacom wananitumia tangazo hapa ,kwamba kesho na wao wanapindua meza
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]washapindua mbona muda mrefu. Tangu 1 April Kaka. Hilo tangazo umechelewa kulipokea tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…