Toka niache kwenda kanisani, maisha yangu yamekuwa bora sana

Toka niache kwenda kanisani, maisha yangu yamekuwa bora sana

Na ndicho kinacho nifanya nione dini ni utapeli wa hali ya juu. Bora wa kina Elon musk wa najifurahisha kutengeneza gari zinazo paa kuliko wanaokesha kulia lia makanisani
Wakina Mwamposa wana sadaka za kila namna mpaka za kujimaliza plus kuwauzia watu udongo, maji n.k! Atleast mimi uwa natoa kwenye semina za Mwl Mwakasege cuz zinaenda kusaidia kuandaa semina ijayo pahala pengine na sio kwenye account binafsi ya mtu.
 
Ni najua kuhusu nilicho kiandika.
Imeenda straight forward kuonesha kuwa wanakwenda kanisani wanakwenda kupoteza muda kulilia kitu kisicho kuwepo
Kwa hiyo wewe kufanikiwa baada ya kuacha kwenda kanisana kunathibitisha Mungu hayupo? Na labda nikuulize, unaweza kuweka ushahidi kuwa kwenda kanisani ndio ilikuwa inakuzuia kufanikiwa?

Kuna wapagani au baadhi ya watu wa Asia huko hawaamini katika Mungu na wanafanikiwa, au wazee wetu kabla ya dini kuja walifanikiwa pia kwenye shughuli zao hii utaileza vipi?

Kuna ya kujifunza kuwa tararibu za utafutaji mali zinajulikana, na zinaweza zisiwe na uhusiano wowote na dini na ndio maana viongozi wa dini hupata mapato kutoka kwa wafuasi wao.

Hivyo, ni vizuri kujua vizuri mawanda ya dini na suala la upatikanaji mali. Suala la pili na muhimu ni kuweza kutofautisha kwenda kwenye nyumba za ibada (religious) na ile hali ya kumtafuta Mungu ndani ya moyo wako na popote ulipo (spirituality). Mtu anaweza asiende kwenye nyumba za ibada na bado akawa na uhusiano mzuri na Mungu wake.
 
Mara ya mwisho kwenda kanisani ilikua siku napata kipaimara. Baada ya pale sijawahi kwenda tena. Ilikua 2006.

Am I proud of it? No.

Am I at peace with my life? Yes.

Is it because I don't go to church? No.

Do I believe in God? Yes.

Do I believe in church? No.

In any other religion? No.
 
Hii ni miongoni mwa best qoutes ninayoitumia katika kufanya maamuzi yangu .

Kuna wakati mambo ya shule walimu Fulani walikuwa jau na kunifanya nichukie masomo Yao na shule , ila nikakaa kujiuliza nikifanya maamuzi ya kuchukia hayo masomo na shule yatakuwa maamuzi kwa ajili ya nani na madhara yatarudi kwa nani ? jibu nikapata Mimi ndio muathirika namba Moja wa kila uamuzi nitakaochukua kuhusu Mimi , hapo nikatuliza akili na kuchanga karata zangu vyema .

Hadi kwenye maisha sometimes nilitaka kukata tamaa kwenye jambo Fulani zuri , nikajiuliza swali Moja hayo ni kwa ajili ya nani na nani muathirika namba Moja ? jibu likaja ni Mimi , hapo nikafunga mkanda na kusonga mbele
Safi sana
 
Yesu mwana wa Mungu, kabla ya kusurubiwa na wayahudi msarabani alilia na kuomba ikimpendeza Mungu kikombe cha mateso kimuepuke,

Kwani Mungubalimkubalia? Alimtuma malaika aje amtie Nguvu/Moyo lkn mateso ni lazima ayapitie, maana kaandikiwa yeye na sio mwingine.

Sasa wewe kama unafikiri Mungu anakupenda kuliko mwanae, endelea kuomba shida zikuepuke badala ya kuomba neema/Ujasiri wa kuzikabiri 😅
 
Ni najua kuhusu nilicho kiandika.
Imeenda straight forward kuonesha kuwa wanakwenda kanisani wanakwenda kupoteza muda kulilia kitu kisicho kuwepo
Nani anapoteza muda?. Na inakuwaje kwamba wanaye Muomba hayupo?
 
Back
Top Bottom