Tuache kumuita Rais Samia Suluhu Hassan 'Mama'

Tuache kumuita Rais Samia Suluhu Hassan 'Mama'

KooZito

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2020
Posts
397
Reaction score
1,377
Tumempata Rais mpya, anaitwa Samia Suluhu Hassan. Sidhani kama ni sahihi kumtambulisha kama Mama Samia Suluhu Hassan maana hata Magufuli alikuwa ni Baba kwa maana ya mzazi lakini kamwe hatukuwahi kuwaita Baba Jakaya, Baba Mkapa nk.

Kisaikolojia kutanguliza neno "mama" ni kutweza cheo Cha Amiri Jeshi na kulazimisha ujinsia usiokuwepo. Ni kumwondolea heshima stahiki maana hata yeye amesema mara kadhaa, "Umakamu wangu ni hapa ofisini nikirudi nyumbani ni mama kama Mama wengine". Kwa mantiki hiyo tumuone Rais SSH akiwa ofisini si nyumbani.

#FreedomIsBack!
 
Yeye ndo alisema tumuite hivyo, sasa kama wewe hutaki labda we ndo First gentlemen wetu, basi tutatii kwakuwa wewe ndo baba, vingivevyo wahi kesho kituoni kapime UKIMWI
 
Mwinyi tu na miaka yake 95 anamuita mama tena mbele ya hadhara Mimi na miaka yangu 20s naachaje kumuita mama?

Acheni kucomplicate mambo. Kiutamaduni kumuita Rais mama Samia it's honourable kuliko hata Rais Samia.
 
Wivu tu! nani aliekutuma uwaite wale vigagula mashangazi. Tuachie mama yetu.
 
Huo ni utamaduni wetu wa staha,hatumaanishi 'Mama' wa kutuzaa

Na Cheo hicho kikianza kupotea na badala yake ukianza kuona cheo cha Bi fulani kinatumika sana ujue kaanza kuboronga pahala.
 
Kuitwa mama sio dhambi ila inategemea matumizi hayo ni kwenye mazingira gani na nani pia. Usihangae akawa kwenye ziara za kikazi ukasikia anaitwa mama hadi na wazee aliowapita umri maana mama inaweza kuwa heshma kubwa sana kutokana na wanachoaddress

Kwenye masuala ya kazi ya kiofice ni Rais Samia Suluhu Hassan

#MamaWaTaifa
#HaijawahiTokea
 
mtu yeyote anayekuzidi kazi--------au hata kilimo, huyo ni MAMA.

Mzee mwinyi.

huijui nguvu iliyopo kwenye hilo jina mkuu,ukimwita hivyo mwanamke umemheshimu sana.
 
Wewe ni nani?

Nyerere aliacha kuitwa mwalimu?

Tuanzie hapo.

Yaani mataga kuna mabata mengi sana
 
Back
Top Bottom