Tukio gani la kuchepuka lilikufanya upoteze imani kwenye taasisi ya ndoa?

Huu uzi nina usoma masaa hayo na niko safarini kikazi ila nilitoa maelekezo kitambo sana na anajua kuwa kuwa mimi kwenye kosa la namna hiyo sitoi hata kadi moja ya njano,ni kuzama ndani ya mfuko wa bukta tu na kumuonesha kadi nyekundu na hata kwenye kadi silazimiki kuandika chochote.
 
Mama la mama uyo Hana hata aibu mbele za watu Kwel
 
Duh! Vibamia kazi tunayo
 
Aiseee kweli huyo kiboko.
 
Ndoa sio kwa wajinga ili udumu na ndoa lazima uwe na akili haswa sio zile za G.P.A kubwa

USSR
Hao wenye akili wanaoingia ndoani ndio hawahawa wanaokuja kulialia humu JF kwamba ndoa zao zimewashinda.

Sasa kama wenye akili walioko ndoani wanataka kutoka huko, Nani ni mjinga kati ya waliopo ndoani na kataa ndoa?
 
Hujakomaa...kuna zaidi kwa mwanamke na mwanamume...ni zaidi ya kukutana kimwili

Kama ni kijana sawa...lakini kama ulikuwa una amini hili...yaani ufuska...umalaya na mambo machafu,asilani hutakaa na huwezi mambo ya ndoa...subiri kuona wenzako tukizeeka hali tukifurahia matunda na furaha nzuri ya ndoa

Kupanga ni kuchagua
 
Daaah, watu wanapitia misukosuko jamani 💔❤️‍🩹
Kabisa...maisha usipoyaendea kwa adabu,usipokuwa makini kutumia uhuru wako,lazima yawe na visa...

Utachukia ndoa...na visa vitakuandama...utafumaniwa na wake au wame za watu...ndio binadamu hajaumbwa kukaa peke yake...

Na ukizeeka utakuwa deserted,kama alietelekezwa...Huna familia ,hadi unakufa utakufa kwa aibu.

Mungu atujalie kumcha ili tuimudu dunia na vurugu zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…