Mpaka leo, kumbukumbu zilizopo, ni kwa Polisi kuua na kuwatesa mara kadhaa viongozi, wanachama na waungaji mkono wa vyama vya upinzani.
Wapenzi na wanachama wa CUF wamewahi kuuawa na Polisi huko Zanzibar.
Wapenzi na wanachama wa CHADEMA wamewahi kuuawa a Polisi huko Morogoro na Arusha.
Wapenzi na wanachama wa ACT wamewahi kuuawa na Polisi huko Zanzibar.
Na hivyo vya vyote, wanachama, wapenzi na viongozi wake wamewahi kuteswa, kuwekwa mahabusu, hata kutekwa na kufungwa.
Lakini haijawahi kutokea hata mara moja, kiongozi, mwanachama au mpenzi wa CCM kuteswa au kuuawa na Polisi wakati akiwa kwenye harakati za kufanya siasa.
Mara zote Polisi hawajawahi kuviacha vyama vya upinzani vishindane na CCM, na hasa pale itakapoonekana CCM kuelemewa. Polisi wakiona kuna uelekeo wa CCM kuzidiwa na vyama vya siasa kwenye ushindani wa kisiasa, huingilia kati wakitumia nguvu za dola, ili kuilinda CCM. Kwa sasa Polisi, ni taasisi inayotegemewa sana na CCM kuliko taasisi nyingine zote. Jeshi la Polisi limekuwa idara muhimu sana ya CCM katika kuhakikisha CCM haizidiwi katika mashindano ya siasa.
Kijana Hamza alikuwa ni kada kindakinda na kiongozi mfia chama wa CCM. Imekuwaje huyu kada mwaminifu wa CCM hata akaenda kushambulia na kuua Polisi ambao ni makada zaidi ya makada katika kutetea maslahi ya chama? Imekuwaje wafia chama hata wakaanza kuuana wenyewe kwa wenyewe? Ni jambo la kufikirisha sana.
Kuna matukio mengine, yanayoendana na haya. Huko siku za nyuma ilikuwa ni kawaida sana Ndugai kuwafanyia harassment wabunge wa upinzani bungeni. Leo hawapo. Hivi karibuni Ndugai kawaita makada na wabunge wa CCM, Gwajima na Jerry kwenda bungeni kufanyiwa sawa na walivyokuwa wanafanyiwa wapinzani. Imekuwaje wafia chama kuanza kufanyiana harassment wenyewe kwa wenyewe kupitia Bunge? Inafikirisha sana.
Chini chini, ndani ya CCM na nje ya CCM, wapenzi, viongozi na wanachama wa CCM, wanafanyiana fitina za hali ya juu, huku baadhi wakimwunga mkono Rais wa sasa na wengine wakimpinga. Rais ambaye, hapo zamani angepingwa kwa baadhi ya mambo na wapinzani, sasa anapingwa kwa nguvu nyingi na wana-CCM wenzake. Inatikirisha sana.
Wakati nikiyafikiria haya, nikijatibu kuitafuta hekima, nikachukua kitabu changu kitakatiktu. Ndipo macho yangu yakaangukia kwenye kitabu cha Kut 17:8-15
Katika simulizi hii kwenye biblia, wana wa Israel walipoliitia jina la bwana ili kupigana na Waamaleki, Musa alipoinyanyua mikono yake, Waisrael walishinda.
Simulizi nyingine inasema maadui hata waliuana wenyewe kwa wenyewe. Hii maana yake ni kwamba Mungu anaweza kuwafanya muuane wenyewe kwa wenyewe.
Hiki kilichotokea jana kati ya Polisi ambayo ni taasisi yenye uaminifu mkubwa kwa CCM na kada na kiongosi mtiifu wa CCM, ni friendly fire, ni friendly war, ni friendly calamity, ni fruliendly disaster. Mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi was caught in fire but was not a target.
Wenye macho ya rohoni, ndani ya CCM, wanatakiwa kutafakari zaidi. Matukio makubwa na mabaya, hutanguliwa na matukio madogo, yanayoonekana ya kawaida.
Wenye kupuuza na wapuuze, maana kuupuuza ukweli hakupunguzi bali huongeza hatari.
Mwalimu aliwahi kunena, "mnasema wao Wazanzibari na sisi Watanganyika kwa sababu ya Muungano, bila Muungano itakuwa sisi wasukuma, sisi wangoni, sisi wachaga, n.k."
Nami ninasema, "Kukiwa na vyama vya siasa vya upinzani, kutakuwa na sisi na wapinzani. Lakini bila upinzani, kutakuwa sisi wana-CCM wa kawaida, CCM Polisi, CCM-wakristo, wana-CCM waislam, wana=CCM wa kanda ya Ziwa, wana-CCM kanda ya Kusini, wana-CCM tunaomwunga mkono Samia, wana-CCM wanaompinga Samia, n.k."
Ujumbe muhimu:
Tuzoee kutenda wema na haki kwa kila mtu hata kama tunatofautiana naye kifikra, kiitikadi, kiimani, kimtazamo au namna nyingine yoyote iwayo. Tukizoea kutenda uovu dhidi ya tunaotofautiana nao, siku wasipokuwepo, roho ya uovu ule ule tutaitumia dhidi yetu wenyewe.
"Moyo wangu wamtukuza Bwana, roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu. Kwa kuwa Mungu Mwenye Nguvu amenifanyia makuu, jina lake ni takatifu. Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi. Amefanya mambo makuu kwa mkono wake: Amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao; amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu.”