Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

MWAMBA KATEULIWA kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Sasa mjiandae na kupiga push-ups jukwaani... sasa tunasubiri kujibu mapingamizi (amblyopia tunajua yapo mengi tu kkutoka kwa watu waoga).. #TunduLissu2020 #nohatenofear @TunduALissu
Yes tuko hapa na ndo tunaelekea ofc zetu za kanda ...ni lissu ni lissu ni lissu
 
Wewe kama mimi Mkuu nina donge la hali ya juu sijui habari hii kama ni kweli au la!

Acha kuturusha roho, aisee hapa nilipo ni presha tuu.halafu kugomea ndio nini?
 
Yaaani nec wamejibaraguza ili iwe wote washaisha na tbc washaondolewa ndio wampitishe Lissu?
Ukweli hauwezi kufunikwa uvunguni usipohubiriwa hata juu ya paa.
Hongera zake Lissu kuteuliwa,
Tunasubiri mziki kuanza rasmi
 
jamaa atakuwa anaubao sana. tangu saa 6 tumbo halijapata chochote duuu
 
Ni dhahiri sasa kwamba kuna dalili ya kuchokwa kwa rais wangu Magufuli, wanaoonekana kumchoka ni watumishi na viongozi ndani ya serikali yake.
Kwa kuangalia namna ambavyo mgombea wa CHADEMA amekuwa handled hii inaonyesha ni mkakati wa kulazimisha kupandisha joto la kila mmoja ili kufuatilia kila hatia anayoipiga na kupitishwa Tundu Lissu.
Yote wayafanyayo yanaibua chuki na hasira ya malipizi dhidi ya serikali.
Tangu amerejea nchini, Tundu Lissu amebadili kabisa upepo wa siasa za nchini Tanzania ambazo zilitawaliwa na Chama tawala pekee. Sasa hivi CCM imejikuta kwa wingi, nguvu, ukubwa, uchumi, mtandao na mamlaka yake wanapambana na Tundu Lissu as individual.
Option pekee iliyobaki kwa CCM ni kutumia vichwa vyao ambavyo vipo mbali sana na mfumo ambavyo hata haijulikani kama wanavijua, nje ya hapo ni to pull the nuclear button.
 
Chadema wanacheza mchezo wa serikali, CCM na NEC toka siku Lisu anaingia TZ, lakini wao wanadhani kinyume chake. Kila wanachokitarajia kinakuja kinyume chake, itakwenda hivi hadi mshindi anatangazwa. Mda utaongea
 
Sasa mlikua mnalia lia nini. Magu hanaga ushamba ule wa kukata wapinzani wake
 
Reactions: BAK
Walichokifanya NEC leo wamemuongezea sana huyu jamaa attention.

Bila shaka hata kura zake pia zitakua zimeongezeka. NEC wanapaswa wafahamu siasa ni sayansi.
 
Enheee picha la kutisha linaanza sasa. Ngoja nivute popcorns mapemaaaaaaaaaaaa.

Kubwa la maadui kazi anayo.
 
ASANTE YESU, ASANTE MUNGU.[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kwa dhati kabisa nampongeza Tundu Lissu kwa Kuteuliwa kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kazi Kwetu wapiga kura kuchagua yupi bora baina yake na Rais Magufuli.

Sina Cha ziada cha kuongezea.
Umemaliza kudhikiri. Maana ulikiwa busy kupiga ramli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…