Wandugu;
Huu ucheleweshwaji na ukiukwaji wa ratiba ya wagombea kuwasilisha fomu zao uliofanywa na NEC, hauna afya kwa mustakabali wa taifa letu na uchaguzi wenyewe.
Hivi ikatokea mgombea wa CHADEMA akashambuliwa na wale watu wanaoitwa "wasio julikana" njiani akiwa njiani anarejea kwenye maskani yake baada ya kumalizana na NEC, nani atalaumiwa?
Siombei itokee hivyo lkn nawaza tu kwa sauti!
Hivi haitaonekana kwamba NEC iliujua mpango huo na ikatumiwa na hao "wasio julikana" kuufanikisha?
Ndio, ndivyo itakavyo someka kwa sababu watakuwa wamehusika kwa maksudi kufanya mgombea huyo aondoke NEC usiku.
Ni hayo tu wandugu.