Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

Acha tu tulitembea na mdundiko kutoka Tandale mpaka Buguruni tuliporudi home tulichezea stiki na mzee mpaka mjumbe aliingilia kati ndo ikawa pona yetu

View attachment 1989651
Hahaha mkuu umenikumbusha mbali sana, mdundiko ulipita home nje Kijitonyama gafra nikawa katikati ya ule umati nikiufuata na kufurahia mauno na nyimbo za mdundiko. Kuja kushtuka jioni giza linaanza kuingia eneo silijui wala hakuna ninaemfahamu. Nikaanza kulia, wasamalia wema wakanipeleka msikitini kutanganzwa kuwa nimepotea.
Cha kushukuru Mungu nikaulizwa shule ya msingi nasoma wapi? Bila kusita nikiwa nalia nikataja shule yangu ni KITONYAMA PRIMARY SCHOOL so nikachukuliwa mpaka maeneo ya shule nikawaambia hapa ninapajua. Bhas nikangoza njia mpaka nyumbani pamoja na wale wazee wawili (mmoja akiwa ni balozi ) ikiwa ni usiku huku nyumbani nilishatafutwa sana mpaka taarifa polisi ilishatolewa na baba.
Eneo nililopetea ni MBURAHATI, now naijua vizuri tu
 
Umenikumbusha enzi ya ndaga bar magomeni kagera, kibisa friends corner hotel, cinema kwa ngawaiya manzese Argentina yalipokuwa makao makuu ya nccr mageuzi,, ukitaka kwenda kwetu uzaramoni stendi sokoni kariakoo basi isuzu tx nyuma
limeandikwa mchawi na mwizi mzuri nani,, lingine limeandikwa 'dikwembe dibanza ingoma '
 
Enzi ambayo mkila wali nyumbani utahakikisha kwenye chai unanawa mkono mmoja ili mwingine iwe ushahidi kwa masela wanuse hata kidogo viganja vyako
Hahaha uswahilini kulikuwa na vituko sana. Naikumbuka sana hii pamoja mkila kuku hunawi mkono ili masela wakajue dah
 
Disco kwa MBOWE huyuhuyu anaesumbuliwa na kima wa vijijini eti ni gaidi.
 
1.Nyama kwenye pick up ikipelekwa buchani huku na wanunuzi wakiwa wamepanda juu wakiikanyaga hiyo nyama.
2.watu wakivuta sigara ndani ya basi.huku basi likiwa limewekewa ashtray kabisa.hakuna abiria anaelalamika.

Mche wa sigara ulikuwa unavurumishwa hadi hospitalini bila kelele ya mtu!
 
Harbours Club Kurasini near mivinjeni ...Mzee Naido, Bugi service mapikipiki Uwanja wa Barafu kuwaona wakina Rozi Walele na kimini cha netball Mzee Mwishehe Dukani Magorafa ya customer kwakina Antonita bonge la pisi leupeee....haha Salvatory Edward tunacheza mpirapale shule ya vidudu tukiwafunga wanatufukuza na mawee...Bambino relini shimo la udogo bar mziki wa nyako nyako konyaaaa......meli ya Kishitobe bandalini .....Amina mento bonge la pisi kurasini kotaz
 
Bila kusahau kumbi za sinema kama Empire,Empress, Drive Inn,New Chox,Star Light,Odeon,Cameo.Kipindi hicho tunamuangalia Angela Mao,Churck Norris,James Bond,Bruce Lee halafu jumatatu tunakwenda kuhadithiana Shuleni[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Brother umeua! Brother umeua! πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚

Vichupi vilikuwa vinabana vile,yet wanaume kama wanaume tulikuwa na nguvu za kiume za kutosha.Sijui leo boxer ndo zinafanya watu wakose nguvu?

Zamani zile ukiona paja la mdada ngoma inasimama kinyama.Leo mtu umevaa boxer mdada mzuri anasimama mbele yako kwenye mwendokasi akiwa hajavaa kitu,mmebanana kinoma,ila bado mtambo hausimami.Boxer zilaaniwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…