Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

Umenikumbusha mbali Ila nianze na hili la jiwe Fatuma.
Kuna mzee mmoja jirani alikua mlevi mlevi, Kuna siku amerudi home saa sita usiku wakati bado Yuko sebuleni anakula akasikia kwa nje wanahesabu moooojah. Fasta akafungua mlango na kuwaambia wale wezi, msinivunjie mlango wangu, chukueni mnachotaka halafu mzee akarudi mezani akaendelea na msosi wake. Basi wale wahuni wamesimama pale mlangoni tiivii chogo wanaiona, deki na redio lkn mzee anakata matonge ya ugali na kutoweza kwenye mchuzi mzito wa samaki.
Wale wahuni walianza kumtukana mzee kwamba Ni mwanga na kuondoka mmoja baada ya mwingine.
Mzee alipomaliza msosi alifunga mlango na kuingia chumbani.
Kesho yake mzee alipokua anahadithia alisema ujinga ule wa kilevi hatakaa aurudie Tena.
 
Enzi hizo ugonjwa mkubwa ulikuwa malaria na badae ukimwi lakini siku hizi ni mwendo wa sukari, presha, ini , figo, stroke.
Halafu kipindi kile kulikua hakuna swala la kukosa nguvu za kiume. Hata ofisa mzee akiamua anakanyagia kweli kweli.
Siku hizi vumbi la kongo na kwa wsheshimiwa Viagra .
 
umenikumbusha kipindi cha miaka 1994 buguruni kwa mnyamani na kile reli ilipokuwa inapita kulikuwa na nyumba za udongo sana.

miaka 2000 tabata,kisukuru,mabibo nyumba zilikuwa za kuhesabu tena mashamba ya mpunga huko tabata.

kwa wale tuliokulia sinza miaka 90 mnakumbuka ukuta wa posta kabla kuwa stendi ya elfu 2000.

maeneo ya chuo kikuu kulikuwa na mitaro yenye maji safi na unapata samaki wa kufuga.

maisha ukianza kukumbuka nyuma unaanza kulia maisha ya zamani yalivokuwa mazuri
 
Ila watanzania kwa uwongo na uzushi. Nakumbuka kabisa iyo ya pajero ilivypamba moto eti kuna katv kwenye dashboard jinsi unavyo geza spidi unaona jeneza ukizidi unaona watu wa nabeba jeneza wanaenda kuzika.

Halafu kuhusu popo Bawa yani uzushi tuu hadi tulikuwa tunaogopa kulala. Wakamsingizia hadi mzee ruksa.

Ishu ya wanyonya damu masinga singa walizushiwa
 
Usinikumbushe AFRAHA STADIUM, STAGS HEAD HOTEL NA SHULE YANGU MENENGAI . Ulishafika landipanya???
 
1. NGOMA YA MDUNDIKO
Kaka usiache nitoe machozi.
Kuna dogo mmoja mitaa ya Gongo la mboto aliingia chooni kujisaidia. Enzi zile madogo wakiingi chooni wanavua kabisa kaptura na kuiacha nje ya choo. Sasa dogo wakati anamalizia shughuli za chooni mdundiko ukapita. Dogo alipotoka nje alisahau kuvaa kaptura na kufuata mdundiko. Muda umekwenda Sasa mama dogo anamtafuta dogo. Kufika uani anakutana na kaptura ya dogo Ila dogo haonekani. Mama akajua dogo Kwisha tumbukia ndani ya shimo la choo. Muda wote huo dogo Yuko kwenye mdundiko.
Wazee wa mtaa wakaita gari ya faya. Yale makelele ya gari ya faya yakamstua dogo naye ikabidi akaangalie home kulikoni mbona wanavunja choo chetu.
Faya wakavunja choo ndani ya choo hakuna mtu.
Sasa mama mmoja akamuona dogo Hana kaptura akakuambia dogo akavae kaptura. Dogo wakati anaingia kuvaa ndio bi mkubwa akamuona yapata saa kumi na mbili na ushee. Alooh. Dogo alishushiwa kipigo Cha mbwa Koko aka muroto
 
6. KUMBI ZA STAREHE
Bonga Bar,

We kijana weeeh. Bonga bar uliijuaje?
Saa kumi na mbili na nusu kagiza kanaanza tu watu tunanawa na koni zinavyonzwa hadharani. Bar Ina mabarmaid wengi kuliko wateja.
Wee mwana wee.
Kumbe umeona mengi mweh.
Siku hizi ukipita Mboka unajichekea kikoyomoyo
 
Ilikua chupi unakuta nzima kabisa mara ghafla unaweza kuhisi pumbu ziko wazi kumbe kauzi keshakatika
πŸ˜€πŸ˜€ inaanza kupanda taratibu kuelekea tumboni...
 
Kitambo mno mkuu
 
Umenikumbusha ki luxury pugu Kariakoo,ubungo minazi,Kuna watu hawawezi kuelewa ukiwaambia pale ubungo lilipo jengo la Tanesco l,ilikuwa soko kubwa,enzi hizo panaitwa ubungo minazi.
Hivi watu wanajua kabla stend haijaamishiwa makumbusho ilikuwa mwenge!?
Vipi story ya mtu kugeuka chatu!!buguruni!!
Vijana wa leo wakiona mwendo Kasi,wanafikiri ni kitu kigeni kwa baba zao,miaka ya 90,zilikuwepo ikarusi(kumba kumba).
Kipindi hicho,kutoka ubungo kwenda Mbagara ni gari tatu!!
Ubungo buguruni,buguruni Temeke,Temeke Mbagara!!!
Aaaah tumetoka mbali sana.
Kipindi hicho nasoma darasa la tatu external nakaa liver side,natembea kwa miguu,ilipo mabibo hostel,ulikuwa uwanja tunachezea Mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…