Tunaunga mkono kwa kauli ya RC kurudisha mabasi yote katika stendi ya Magufuli Mbezi

Miji mingi duniani sio lazima uende mpaka stendi kuu bali unaweza kupandia au kushuka road bay kama una ticket yako

Makosa yalianza walipojenga stendi kubwa hivyo
Bora zingekuwa sehemu za kushushia watu hata pembeni mwa Barabara kama majiji makuu ya Ulaya
Traffic itakuwepo tu
 
Nikusaidie. Zamani stendi zilikuwa tatu. Kisutu, kariakoo na


Sio kisutu tu hata Kariakoor mabasi yalikuwa yanadhusha na kupakia.
Sawa ila Stand ya mkoa ilikuwa Kisutu,hapa hizi kelele ni sababu ya mazoea, mimi na amini hata mbezi tutazoea cha msingi abiria kuwa na nidhamu ya muda.
 
Mimi nakuambia waliobuni ubungo unaanza kuishambulia Mimi. Waliona ubungo ni meeting point nzuri ya mabasi. Kama unataka kawabishie hao. Ila hakuna justification ya kupeleka stendi Mbezi. Dar sio Mkuranga kwamba unapeleka nje ya mji ili mji ukue. Dar ilishakuwa na imejaa.
 
Na sisi uku Mwanza tunaomba Mkuu wa mkoa Mh Saidi Mtandao...tuondoshee hizi ofisi za mabasi apa NATA warudi Nyegezi kule kuliko na stendi kubwa iliyojengwa Kwa gharama kubwa pesa za Wananchi.
Sababu ya kwanza kuwaondosha apa NATA ni kupunguza jammm ya magari pamoja na Bajaji
Pili ni kurejesha na kutanua mji wa Mwanza kibihashara...hasa maeneo ya Nyegezi na Vitongoji vyake....
Tatu kufanya stendi ya mabasi Nyegezi kutengeneza mzunguko wa pesa na kuingizia mapato stendi pamoja wafanyabiashara maeneo ayo.
Lamwisho kabisa...kuzuia mabasi yasiingie mjini hasa NATA kutafanya biashara /mzunguko Kwa daladala pamoja bajaji /teksi kufanya biashara na mwisho wa siku kukuza huchumi wa mtu mojamoja.
 
Kwani waliobuni Ubungo na Waliobuni Mbezi wanautofauti gani? Hebu niambie wewe,maana unazunguka unarudi palepale, maana aliyebuni Kisutu ndio hao hao wamebuni Ubungo na baadae wakabuni Mbezi au wewe unaona walibuni watu tofauti?
 
Mbona zamani wote waliishia ubungo nini kinawafanya sasa hivi washindwe kuishia mbezi
 
Nyie ndio mnaofanya wanaolazimisha stand ibaki Mbezi waonekane wana hoja. Maana hamna hoja ya maana mnazubgukazunguka tu.
Nani kakataa stendi isiwe Mbezi?. Stendi iwepo ila mabasi yaruhusiwe kuwa na stendi binafsi za kushushia abiria wa mbali. Kajifunzeni Mwanza wanavyofanya.
 
naimani hata watangulizivwalio ruhusu izo ofisi wliliona hili mwanzo wakachukua hatu kupunguza usumbufu na kero za wakaazi wa dar ila naona tunataka kurudi kule kule tena dah😄
Mimi naona kuktaza stendi binafsi ndio kurudi kwenye tatizo. Dar Ina watu milioni tano na wilaya Tano halafu stendi ni Moja Tena nje ya mji.
 
Nata ni stendi inauotambulika. Mwanza stendi ni tatu, Nyegezi, Nata na Nyamhongolo. Ila Mwanza wanautaratibu mzuri basi lazima liingie stendi.
 
Advantage ya maBUS kuanzia stand kuu yanakaguliwa na Vehicle Inspectors na pia madereva hupimwa vilevi kabla ya kuondoka ,wakianzia huko madongo poromoka pasipo kuwa na supervision ni hatari.
 
Hakuna Sehemu yeyote yenye Changamoto ,Kigamboni kuna njia mbili Boti ni 24/7 na Darajani ni 24/7 ,Chamazi Pia ni Mtelezo tena kwa usiku ni Hakuna Foleni ndani ya 1hr ushafika Mbezo Magufuli.

Ukitoka Kigamboni Unapitia Darajani tu unakuja kuibuka Uhasibu ,Unanyoosha Unakuja kuibukia Kijazi Interchange - Unakula Kushoto ukishuka tu MAGUFULI TERMINAL HIYO....Same as Chamazi uwe unatoka Chamazi bamia ,gereji ,maliasili unafika Rangi Tatu hadi Machinjioni Uhasibu -Unakula Kushoto kuitafuta Mandela Road - Kijazi Interchange.
 
Nadhani mabus hayapark tu Bali kupakia abiria. Halafu tuangalie maslahi ya abiria pia.
Usalama kwanza mkuu ,kwenye maslahi vs Usalama ,cha kwanza kuanza ni Usalama.

MaBUS kuanzia huko vichochoroni ni risk ,hayakaguli ,madereva wapo keroro na wanaingia road MBIO MBIO.
 
KUna Option ya kupeleka moja kwa moja Magufuli kwa mizigo ambayo hahitaji purukushani na vipaseli unaweza ukapeleka urafiki/shekilango.
 
Kwa mabasi yaliyopo Magufuli stand haiwezi kutosha
Abood peke yake ana basi zaidi ya 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…