Ukisikia mtu anawaita wasiokubalina naye kuwa ni wajinga, basi ujue ana matatizo makubwa sana ya kiakili.
Kama unawauzia wafanya biashara maarufu kwa mabilions usituletee hapa; wapelekee hao hao watu wako ambao hawafiki hata 0.001% ya hapa JF.
Wewe kama muuzaji unaonekana kuwa desparate kujaribu kuhalalisha bei yako badala ya kunyamaza kuacha soko lijipange. Kadri unavyopiga kelele hapa unaonyesha ufinyu wako kibiashra labda huwa unapata wateja kwa bahati tu na majibu yako hapa yatakuathiri hata wale wateja uliokuwa unapata kwa bahati ukawakosa kwani yanasababisha wapate information on the other side of the coin.
Kuna dalali (labda alikuwa wewe) alitaka kuniuzia kiwanja kwa milioni 80, lakini nikakipata kiwanja hicho hicho kwa milioni 5 tu kwa kufuata sheria za ubadilishaji wa umiliki wa viwanja, tena kwa mabishano sana kwani thamani halisi ilikuwa milioni tatu. Viwanja ambavyo havijaendelezwa bei zake zinajulikana kisheria; huwezi kuchukua kiwanja bure kutoka serikalini ukakihodhi kwa muda halafu baadaye ukakiuza kwa bei kubwa. Sheria zipo wazi kabisa; utakiuza baada ya kukiendeleza tu, na kuna kitu cha kuuza kwa bei unayopanga.