Mwamba alipofika tume kuweka mambo sawa ya kisheriaHakuna kupotezea, Magu amekithiri mno kukiuka sheria, kanuni na hata Katiba ya nchi
PositivelyMagufuli alivyowanyoosha haitoshi, Lissu atanyoosha zaidi ya Magufuli?
Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma
Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mhe. Tundu Lissu, akiwa pamoja na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, muda huu wanaelekea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Uchaguzi House) jijini Dodoma kuwasilisha fomu zake za mapingamizi dhidi ya wagombea wengine katika nafasi ya Urais wa JMT, baada ya hapo atazungumza na Waandishi wa Habari Ofisi za Chadema, Kanda ya Kati, jijini Dodoma.
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Agosti 26, 2020
====
Tundu Lissu amewawekea Pingamizi Wagombea Wawili wa Urais. Amewawekea pingamizi Ibrahim Lipumba wa chama cha CUF na Dr. John Magufuli wa chama cha CCM.
Hadi muda unaisha, hakuna aliyemuwekea Pingamizi Tundu Lissu. Hivyo kaondoka na kuelekea Ofisi za CHADEMA za Kanda kuongea na Wanahabari.
Zaidi, soma:
Uchaguzi 2020 - NEC imemteua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mgombea wa Urais
Uchaguzi 2020 - NEC imemteua Dkt. John Pombe Magufuli kugombea Urais na Mama Samia Suluhu Umakamu wa Rais kupitia CCM
Uchaguzi 2020 - Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA
View attachment 1548762View attachment 1548764
Aingie kingi nani tena? Labda hao chadema and co. Maana naona wanaona kuweka pingamiz ni ushindi tayarTunawasubiri tu muingie King!!
Ni hasara sana kumkosa chenge kwenye systemBungeni siku ya report ya uchunguzi ya kina marehemu Deo Filikunjombe. Yaani hadi Lissu mwenyewe walikuwa wanamfuata Mtemi Chenge. Tena siku hiyo bunge lilikuwa live. Walijadili ila wote walikuwa wanamfuata Chenge ili kutafasiri na sheria.
Tatizo litabaki kuwa la tume that if kama kweli kuna tatizo...unakosea.
..TL hajavunja sheria yoyote ile ya uchaguzi.
..tume kupokea mapingamizi yake kunaiongezea sifa kuwa inatoa haki sawa kwa wagombea wote.
..tume lazima ionyeshe kwa vitendo kwamba wagombea wote ni sawa, na haipendelei mgombea yeyote.
..again, Magufuli siyo mungu kiasi kwamba ni dhambi au ubatili kum-challenge.
NB:
..tatizo la wana CCM ni kutaka ktk uchaguzi huu Jpm awe kama "Papa au Baba Mtakatifu", halafu wagombea wengine wawe sawa na Maaskofu.
Acha ubwege wako usifikiri watu ni wajinga kama wewe Tambua kuwa CCM na wapambe wake walimwekea Tundu pingamizi tokea jana na hiki unachokiona kwa Tundu ni kujihami dhidi ya mapingamizi ya CCM tokea janaAngewekewa pingamizi Lissu kungekuwa na povu humu jf kwamba wanamwogopa, leo Lissu kaweka pingamizi anaonekana shujaa. Subirini kidogo mtakuja kulialia Tena .
Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Kama matoke ni hayo basi chadema washachukua la ubungoMpaka sasa hivi ccm 22 chadema ya Lisu 0
Mpumbavu sana wewe dada! Lissu anapambana na Magufuli kama mgombea urais wa CCM si vinginevyo!Anauwa Chama chenu lakini, Magufuli ni Raisi wa JMTZ na mkuu wa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama, kuanzisha Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ ni ujuha, ni watu low IQ ndio wanaweza kufanya hivi, ...
Anamuengua mgombea wenu tulia usikilizie mziki mmezoea vya kunyonga vya kuchinja hamviwezi sasa mtajua mwamba huyu hapa sasaWatu wanajiandaa na campaign yeye anapekenyua forms za wenzake, vipi anaogopa ushindani au hana kingine cha kufanya.
Si alidai yeye ndio anaogopewa wenzake, sijui watanzania wapo nyuma yake sasa mbona anaangaika na watu ambao hawana muda na yeye.
Get the guy some help
Daaaa...... Watu mna maneno 🤣🤣🤣Hii ndiyo tofauti kubwa kati ya "mechanical approach" kwa kulinganisha ni "technical approach', wakati inahitaji matumizi ya maguvu tu pasipo kutumia akili, ya pili ni kinyume chake.
Ni kanuni mbili tu zinaweza kumfanya kiongozi apate kuungwa mkono na wananchi waliokuwa wengi.
Kanuni Na. 1
Tumia hekima na akili nyingi ili uweze kupata aridhio na kuziteka akili za unaowaongoza.
Kanuni Na. 2
Zingatia na kuishika vyema Kanuni Na.1
Mmekaa kishari shari sana, kama siyo chama cha siasa ni kikundi cha mauaji vile.Endeleeni kuchokoza tu.
Ndiyo mkuu nina maana saccos ya chadema!Aingie kingi nani tena? Labda hao chadema and co. Maana naona wanaona kuweka pingamiz ni ushindi tayar
Tena inatakiwa walinzi wa magufuli wapunguzwe kuokoa gharama kwenye pesa za walipa kodiMpumbavu sana wewe dada! Lissu anapambana na Magufuli kama mgombea urais wa CCM si vinginevyo!
Tatizo litabaki kuwa la tume tu kama watu walipeleka forms in advance zikaguliwe kama kuna makosa warekebishe na tume aikuona tatizo naamini itakuwa ivyo.
Issue hapa ni psychological issues the guy is crying for help, he is not emotionally stable yet, hilo ndio tatizo la msingi hapa.