Uchaguzi 2020 Tundu Lissu awawekea pingamizi wagombea wawili wa nafasi ya Urais wa Tanzania. John Magufuli (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)

Taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma

Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Tundu Lissu, akiwa pamoja na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, muda huu wanaelekea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Uchaguzi House) jijini Dodoma kuwasilisha fomu zake za mapingamizi dhidi ya wagombea wengine katika nafasi ya Urais wa JMT, baada ya hapo atazungumza na Waandishi wa Habari Ofisi za CHADEMA, Kanda ya Kati, jijini Dodoma.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Agosti 26, 2020
 
Kama umezaliwa mpenda haki, risasi haziwezi kukubalisha. Hata Nyerere naye alikuwa hivyo hivyo. Ndio maana leo akina Madaraka na Makongoro wako kama sisi. Ndio maana aliacha mshahara wake kama mwalimu Pugu akaingia kwenye mapambano ya uhuru, kazi ya kujitolea wakati huo. Wangapi wanaweza kuacha kazi ya kulipwa mshahara na kwenda kufanya kazi ya kujitolea ya kudai haki?
Uzuri wa Lissu watu wengi bado hawajamuelewa yeye siku zote uwa anapenda haki, sheria ifuatwe na haki itendeke.

Ujanja ujanja kwake no Ni kusimamia ukweli.
 
Zile saa nane ama yale masaa manane jana ya tar 25. August. 2020 ya kumsubirisha mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia saa sita mchana mpaka jioni ya saa moja na dk 40 yalikuwa ni faida tupu kwakwe.

Trust me wale wagombea wengine waliopewa kipaumbele na kuharibu ratiba wakaingia fasta wakapokelewa na kupitishwa haraka wamefanya makosa mengi ya kisheria na hili litawagharimu pakubwa
 
Wakati Lissu ameweka wazi kuwa ameweka pingamizi/mapingamizi, naomba nitabiri tu kuwa kitachotokea katika kuamua juu ya mapingamizi hayo, ni mapingamizi hayo ya Lissu na ya wagombea wengine (kama yatakuwepo), yote yatatupwa.

Lissu ni kioona mbali na anajua afanye nini katika wakati sahihi.

Mshindi hapa atakuwa ni nani, nakuachia msomaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…