Uchaguzi 2020 Tundu Lissu awawekea pingamizi wagombea wawili wa nafasi ya Urais wa Tanzania. John Magufuli (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu awawekea pingamizi wagombea wawili wa nafasi ya Urais wa Tanzania. John Magufuli (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)

Nadhani ili kusiwe na mizengwe na fomu za mapingamizi ziweze kufika salama ilitakiwa hii taarifa itolewe wakati Mheshimiwa Lissu akiwa ameshafika yupo ndani ofisi za tume.

Maelekezo hayachelewi kutolewa kwa wale vijana servicemen wa jkt pale getini wakiwa na incharge wao corporal wa Jw wamzuie mheshimiwa mpaka ikifika saa16:00 ndo wawaruhusu kuingia halafu wakishaingia wakaambiwe ndani muda umeisha wa kuweka mapingamizi
Bila shaka yoyote mchongo ndio ulivyokuwa umepangwa.
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA Mhe. Tundu Lissu tayari amemaliza kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wengine, sasa yupo njiani kwenda ofisi ndogo ya Makao Makuu Kanda ya Kati, kuzungumza na waandishi wa habari saa 11 jioni hii.

Mpaka inafika saa 10: 05 Mhe. Tundu Lissu alikuwa hajawekewa mapingamizi yoyote. Lissu amewasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wawili, Mosi mgombea kupitia chama cha Mapinduzi John Pombe Magufuli na pili Mgombea kupitia chama cha CUF Ibrahim Lipumba.

#NoLissuNoElection View attachment 1548779

Hii imekaa vizuri. Asante mwanataaluma Lissu. Saa ya ukombozi ni sasa. Nchi ilipoteza mwelekeo kabisa.
 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma

Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mhe. Tundu Lissu, akiwa pamoja na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, muda huu wanaelekea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Uchaguzi House) jijini Dodoma kuwasilisha fomu zake za mapingamizi dhidi ya wagombea wengine katika nafasi ya Urais wa JMT, baada ya hapo atazungumza na Waandishi wa Habari Ofisi za Chadema, Kanda ya Kati, jijini Dodoma.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Agosti 26, 2020

====

Tundu Lissu amewawekea Pingamizi Wagombea Wawili wa Urais. Amewawekea pingamizi Ibrahim Lipumba wa chama cha CUF na Dr. John Magufuli wa chama cha CCM.

Hadi muda unaisha, hakuna aliyemuwekea Pingamizi Tundu Lissu. Hivyo kaondoka na kuelekea Ofisi za CHADEMA za Kanda kuongea na Wanahabari.

Zaidi, soma:
Uchaguzi 2020 - NEC imemteua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mgombea wa Urais

Uchaguzi 2020 - NEC imemteua Dkt. John Pombe Magufuli kugombea Urais na Mama Samia Suluhu Umakamu wa Rais kupitia CCM

Uchaguzi 2020 - Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA
View attachment 1548762View attachment 1548764
Hili vibe la mwaka huu raha sana
 
Jamaa anatembea na misafara ya kihuni, utafikiri km sio rahisi mtarajiwa
 
Watu wakisema huyu mtu anahitaji msaada wa kitaalamu ajatulia mnaona wanamnanga.

Kadri siku zinavyoenda ndio anazidi kuonekana kituko kwenye jamii yeye kila kitu anafanya tofauti na wenzake.

Lissu is not fit for office
Unapokuwa tofauti na wenzako ni ishara pia unaweza kuwa upo ahead na uwezo mkubwa kuliko wao.
 
Wewe unaweza kuona Lissu anatumia haki zake lakini tatizo hapo kama unaelewa ‘psychology’ ya impact za kukutana na ‘life changing events’ kama tukio la Lissu side effects ni rebellion na kutokukubali ukweli.

Lissu anatakiwa akubali Magufuli ni raisi wa Tanzania na ana nguvu kubwa kutokana katiba yetu. Kwenda kutembea na ma body guards wanakimbiza gari yake kama na yeye mtu muhimu akumuweki on equal na raisi wa Tanzania.

Kukataa hadharani hakuna kitu Magufuli amefanya hayo mambo yamefanywa na wakoloni ya kujenga miundombinu etc.

Kudhamiria kushinda uchaguzi kwa sababu ya kumshinda Magufuli ukisikiliza speech zake badala ya kwenda kuwatumikia watanzania.

Barua zake za ovyo zenye empty threats na dilusions za international community nyuma yake kwenye uchaguzi.

Ushahidi ni mwingi mpaka sasa serikali inafanya kazi ya ‘baby sitting’ tu amalizane na emotional issues zake; hila he is becoming erratic as days go anahitaji intervention huyo mtu kumsaidia kimawazo.

Mimi mpiga kura nafahamu nani ametufikisha hapa tulipo right kama kungekuwa na utawala wa haki siyo kuoneana tusingefikia hapo lakini kwakuwa kuna kikundi cha wanaojiona wana haki ya kuonea wenzako ngoja twende sawa hivohivo hata Rais akiwa na polisi lakini bado hakuna sheria inayomruhusu kutumia hayo mamlaka aliyonayo kuvunja sheria za nchi kama kusema wapinzani wakishinda wasitangazwe ndiyo maana anapendwa na genge lake tu
 
Hata Mimi nikiwa Rais naweza Jenga sgr sio kazi ngumu .

Hata presidential decree unajenga unakaba huku na unakaba kule reli hio hapo .

Watu wanataka mkate wa kula njaa zinauma ndio hao wako nyuma ya lissu
Uongozi ni kubalansisha mambo. Kama baba unaacha za kula za kutosha nyumbani watoto washibe na zingine unajengea, simple economics!
 
1598450679390.png
 
Watu wakisema huyu mtu anahitaji msaada wa kitaalamu ajatulia mnaona wanamnanga.

Kadri siku zinavyoenda ndio anazidi kuonekana kituko kwenye jamii yeye kila kitu anafanya tofauti na wenzake.

Lissu is not fit for office
mbona hukusema kwenye utofauti wa kula mahindi barabara! Awamu ya kwanza, pili, tatu na nne hawakufanya hivyo. Co kila utofauti ni mbaya kuna utofauti mzuri
 
Inabidi BAVICHA TAIFA mfanye verification ya hii account yenu humu JF.
Iko verified that's why haijafutwa na hii ni matokeo ya kilio cha wengi kuyaka CHADEMA ijitanue mitandaoni
Kumbe ni account ya kitambo sana tangu 2013...lakini nadhani ilikuwa less active

CHADEMA, BAVICHA TAIFA please wekeni nembo ya chama kama DP
 
Back
Top Bottom