Uchaguzi 2020 Tundu Lissu awawekea pingamizi wagombea wawili wa nafasi ya Urais wa Tanzania. John Magufuli (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu awawekea pingamizi wagombea wawili wa nafasi ya Urais wa Tanzania. John Magufuli (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)

Kumfukuza kazi siyo kiholela hivyo, [SUB]katiba imetoa sababu zinazoweza kutumika kumshitaki rais ya kwanza ni iwapo rais amevunja katiba au amevunja Sheria ya naadili ya viongozi wa umma, pili amefanya jambo linalokiuka Sheria ya vyama vya siasa, tatu ni iwapo Rais anamwenendo unaodhalilisha kiti cha urais[/SUB]
Sasa kuna rais amabae ni malaika?

Lazima akikosea tu wenzie wanapeleka mswada wana mngoa.

Sio Lisu akiwa rais wakati anategemewa kupata si zaidi ya asilimia 20 ya kura na wabunge wasiozidi 10
 
Watu wakisema huyu mtu anahitaji msaada wa kitaalamu ajatulia mnaona wanamnanga.

Kadri siku zinavyoenda ndio anazidi kuonekana kituko kwenye jamii yeye kila kitu anafanya tofauti na wenzake.
He is tall water, dont play with him. Anaonekana tofauti because he is far ahead of many
 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma

Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mhe. Tundu Lissu, akiwa pamoja na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, muda huu wanaelekea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Uchaguzi House) jijini Dodoma kuwasilisha fomu zake za mapingamizi dhidi ya wagombea wengine katika nafasi ya Urais wa JMT, baada ya hapo atazungumza na Waandishi wa Habari Ofisi za Chadema, Kanda ya Kati, jijini Dodoma.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Agosti 26, 2020

====

Tundu Lissu amewawekea Pingamizi Wagombea Wawili wa Urais. Amewawekea pingamizi Ibrahim Lipumba wa chama cha CUF na Dr. John Magufuli wa chama cha CCM.

Hadi muda unaisha, hakuna aliyemuwekea Pingamizi Tundu Lissu. Hivyo kaondoka na kuelekea Ofisi za CHADEMA za Kanda kuongea na Wanahabari.

Zaidi, soma:
Uchaguzi 2020 - NEC imemteua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mgombea wa Urais

Uchaguzi 2020 - NEC imemteua Dkt. John Pombe Magufuli kugombea Urais na Mama Samia Suluhu Umakamu wa Rais kupitia CCM

Uchaguzi 2020 - Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA
View attachment 1548762View attachment 1548764
 
Hilo bunge wabunge watakutania wapi? Ukishakuwa na nguvu ya kuamrisha vyombo vya dola, yeyote anayekwenda mahali kukusanyika bila ridhaa yako anapata kipigo. Hayo mambo Magufuli ndio kaonyesha miaka hii yote mitano, kuwa rais ndio anaamua atakavyo na wengine wote wanafuata. Mtengeneze precidence mbaya ya utii wa sheria na katiba, kisha mtegemee wengine watafuata?
Mkuu hivi Lisu awe rais na wabunge wake wasiozidi 20 unategemea nini kitatokea? Hata kama una nguvu za vgombo vya dola wabunge wa upande wa pili lazima wakutimue na uchavuzi kurudiwa
 
Sawa mkuu. Jiandae kulia 28.Shida nyinyi watu vichwa vyenu ni vizito sana.

Sio kwa kura boss. Kama tayari idadi ya wapiga kura ni ya kupika, unategemea matokeo yatakuwa ni ya kura? Watanzania tuko 59m+, inawezekana vipi watu 29m+ kuwa wapiga kura? Ukielewa hiyo huwezi kutamba eti ningoje tarehe 28.
 
Mkuu hivi Lisu awe rais na wabunge wake wasiozidi 20 unategemea nini kitatokea? Hata kama una nguvu za vgombo vya dola wabunge wa upande wa pili lazima wakutimue na uchavuzi kurudiwa

Narudia tena, ukiwa na nguvu ya kuagiza vyombo vya dola, unafanya lolote nchi hii. Bunge na mahakama ni uchafu kama uchafu mwingine.
 
Sasa kuna rais amabae ni malaika?

Lazima akikosea tu wenzie wanapeleka mswada wana mngoa.

Sio Lisu akiwa rais wakati anategemewa kupata si zaidi ya asilimia 20 ya kura na wabunge wasiozidi 10
Mimi nilikuwa nakukumbusha tu kwamba Rais hafukuzwi tu na bunge kiholela.
 
Sio kwa kura boss. Kama tayari idadi ya wapiga kura ni ya kupika, unategemea matokeo yatakuwa ni ya kura? Watanzania tuko 59m+, inawezekana vipi watu 29m+ kuwa wapiga kura? Ukielewa hiyo huwezi kutamba eti ningoje tarehe 28.
Wewe ukikuwa wa kwanza kuhamasisha wenzio wasiende kujiandikisha sasa ulitegemea nini?

Mbali na kura, huu uchaguzi ccm ina sehemu nyingi sana za kuwapigia
 
Wewe ukikuwa wa kwanza kuhamasisha wenzio wasiende kujiandikisha sasa ulitegemea nini?

Mbali na kura, huu uchaguzi ccm ina sehemu nyingi sana za kuwapigia

Ndio maana nashangaa watu 29m+ wametokea wapi? Kama nilihamasisha inakuwaje idadi imezidi watu wazima? Hapo unatetea au unaanika upuuzi wako? Kama mnaweza kupiga nje ya kura, kipi kinawafanya mtambe kuwa tarehe 28 mnashinda? Kwanini msiendelee na sherehe za ushindi?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Baada ya oktoba 28 mtapoteana humu,

Hivi mwenzio tayari ana mabao 22 wewe una 0 bado unaota ushindi?

Lisu atatia aibu sana mwaka huu
Tunazungumzia mtu kufungwa supa kwenye draft au kupigwa woshi kweny pool table ndio alichowafanyia Antipasi leo. Na ni aibu iliyo kuu.
 
Halafu utakuta hata hoja hii itaunganishwa na thread nyingine kufifisha hoja nzito kabisa ya elimu ya kweli ya kiuraia aliyotoa mgombea wetu kwa umma.

Kama hoja ya magufuli asichangishe hela ya ujenzi wa msikiti kanisani ilivyopotezwa kwa kuwa merged na nyingine!. Mods wetu sometimes hawasmeki!
 
Back
Top Bottom