Tundu Lissu kurejea nchini kabla ya tarehe 27 mwezi huu

Tundu Lissu kurejea nchini kabla ya tarehe 27 mwezi huu

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu amesema mwishoni mwa mwezi Julai, 2020 atarejea nchini kwa ajili ya kuendelea na shughuli za kisiasa.

Kuelekea Mkutano wa Baraza Kuu la chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Lissu amesema atahudhuria mkutano huo utaompitisha mgombea Urais wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020.

Kuelekea Mkutano wa Baraza Kuu la chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Lissu amesema atahudhuria mkutano huo utaompitisha mgombea Urais wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020.

Tundu Lissu ni mmoja wa watia nia waliojitokeza kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, wengine ni wakiwemo, Mwenykiti wa chama, Freeman Mbowe, Mbunge Peter Msigwa na mwanasiasa Lazaro Nyalandu.

Tangu alipopelekwa nje ya nchi kwa matibabu tangu Septemba mwaka 2017, Lissu hakuwahi kurudi nchini na hiyo itakuwa ni mara ya kwanza baada ya tukio la kushambuliwa na watu
Tunamsubiri kwa shangwe kubwa shujaa Lissu.
 
Vinavyotia shida Chadema kama vipo usivifiche , viweke wazi vitatuliwe , japo unaweza kuona kuna shida chadema kumbe labda hujaelewa tu yanayoendelea , chadema inabeba kila zuri kutoka kwa yeyote yule .

Ofisi ya Katibu Mkuu inakaribisha maoni ya kujenga
Kuna yaliyofichika mkuu, rafiki yangu Erythrocyte, kiasi kwamba hamtaki kuyaweka wazi watu wayajadili.

Kwa ujumla wake, ngoja nikudokeze: CHADEMA mpo karibu sana na 'version' ya Kikwete katika yale mabaya tuliyoyaona kwenye awamu ile.

Hapo ndipo panapotia shida.

Lakini hilo halizuii kwa sasa kutafuta njia za kuondoa balaa hili linalotuandama la CCM inayotufanya mateka.

Ni bora kuwa huru na kuwa na uwezo wa kupambana na adui yako kuliko adui aliyekuweka mateka moja kwa moja.

Sasa sijui kama utanielewa; lakini huo ndio wasiwasi wangu.
 
Mbona ufisadi upo sasa CCM ya sasa ina wizi kuliko CCM zote pesa trilion 1.5 imepigwa kwenye utawala huu huu ndipo wakamtoa kafara CAG kuficha Aibu zao, Ndungai katafuna bilion 12 peke yake akiwa India, 10% ununuzi wa Ndege,Ujenzi chato Airport, Reli, bwawa la umeme
Mkuu na mimi nikaribishe kwenye kijiwe chako unachokunywa kahawa!
 
Taarifa mbaya sana hizi kwa MATAGA wa ccm! maana huyu ndiye kiumbe pekee aliyeweza kum challenge Magufuli hadharani kiasi cha kushambuliwa mchana kweupe kule Dodoma na watu 'wasiojulikana'

Kwa mbali anafuatiwa na Zitto.
Zitto can hardly be trusted.
 
Huyo Lissu mtapitisha kama mgombea ama mna mhadaa babu wa watu aje alale lockup maana ana kesi nyingi za kujibu.
Tanzania nzima ingekuwa na wakina Lisu 100 tu, wangetosha sana kuiua na kuizika ccm , ifutike kabisa duniani.
 
Kumtupa segerea pekee yake ndio salama ya jiwe, na genge lake la ccm. Hiyo ya kumfunga kwa kesi za kubumba , ndio njia pekee iliyobaki ya kukibeba chama kichovu cha ccm.
Cyprian Musiba kawaanda wagonjwa wa corona ambao watapelekwa jela walale karibu ya Tundu lisu wamuambukize.
 
Hapa nauona mgongano wa kimasilahi kati ya chadema na Act wazalendo...

Chadema najua bila shaka Lissu atakua mgombea wao na Nyalandu mgombea mwenza ila sasa ACT watashindwa kusapoti Chadema maana wao wanamtaka Membe na Chadema sidhani kama watamuhitaji Membe.

Matumaini ya hivi vyama kushirikiana hayapo...

Mambo yasiwe Mengi na Mengi yasiwe mambo
Wapinzani kumchukua Membe ni sawa na kurudia ule upumbavu wa kumchukua Lowasa 2015.
 
Mh. Tundu Lisu, unakuja kwenye makucha ya Simba. Kwangu mimi nakushauri usije kama kuna International Security assurance or anything of that nature ( sijui kama ipo anyway). Short of that sioni your precious life to be in safe custody. Ujue unakuja kwenye makucha ya Idd Amin, alimuua hata Askofu Mkuu wa Anglican Church Janan Luwum
Anayekushauri anakushauri si vema
Magu ni katili kiasi hicho ?
 
Cha kwanza atakachokutana nacho ni harufu mbaya ya uchafu wa mji wa Dar.

Halafu atashangaa kuona watu wamekonda na kuchoka sana. Pia ataona barabara zimejaa bidhaa mbalimbali mpaka sehemu ya kupita hakuna.

Kiujumla ukitoka ulaya halafu ukafika airport Dar unatamani urudi na ndege iliyokuleta.
Mkuu
Exposure
Exposure ni elimu kubwa sana.

MATAGA wengi hawana exposure. Wakiona lile daraja la Ubungo wanahisi ndio wameimaliza dunia yote.
 
Rais mkapa alimaliza kipindi cha pili akiwa mlemavu na hata Rais mwai kibaki wa kenya alifanya kampeni akiwa kwenye while hair na alipoingia ikulu akawa ni mlemavu wa kudumu
Mkapa alipigwa stuli na nani vile ?
 
Na hiko ndo kitu kwa sasa Zitto anapigania yaani anarudi jambo lile lile mana nakumbuka hata 2015 Zitto hakuungana na ukawa badala yake yeye akawsimamisha Rais mama Anna Mgwira
Wapinzani kumchukua Membe ni sawa na kurudia ule upumbavu wa kumchukua Lowasa 2015.
 
Back
Top Bottom