1.Kwanini Wabunge wa Zanzibar huwa wanajadili bajeti za Wizara zisizo za Muungano, Kama Wizara ya Kilimo?
2. Kwanini kwenye Baraza la Wawakilishi hakuna Wabunge toka Tanganyika kulinda Maslahi ya Tanganyika?
3.Kwanini Wazanzibar wanakuwa Wakuu wa Wilaya Tanganyika ilihali Watanganyika hawawezi kuwa Znz,assumption kwamba TAMISeMI ipo nchi ya Rais?
4.Kwanini Rais wa Jamhuri akitaka kugawa eneo labda Mkoa au Wilaya,Tanganyika anagawa tu,ila Kwa Zanzaibar ni lazima ashauriane na rais wa Zanzibar?
5.Idadi kamili ya wapiga kura ilikupata Jimbo la Mbunge wa bunge la JMT ni ngapi?
6.Kwanini Sukari bei chini Znz?
7.Kwanini Leseni ya udereva ya Tanzania haikubaliki Znz?
8.Kwanini Mh Rais hakubinafsisha bandari za Znz?..Znz hawataki Ufanisi?
9.Kwanini Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hatambuliki Znz ilihali ni wa Tanzania nzima?
10.Kwanini Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halijawahi kuwa na Spika wala Naibu Spika toka Zanzibar?