Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Polisi Nyamongo wameshambulia msafara wetu kwa mabomu ya machozi wakizuia njia kuelekea kwenye mkutano wetu wa kampeni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Polisi Nyamongo wameshambulia msafara wetu kwa mabomu ya machozi wakizuia njia kuelekea kwenye mkutano wetu wa kampeni

Sababu mbona huweki?
Sababu inajulikana!
Dpmw-LYXUAAsrws.jpg
 
UPDATES

Polisi wamesalimu amri na kuondoka baada ya somo la Lissu kuwaingia. Mkutano unaendelea Nyamongo muda huu. Aidha baada ya raia kupigwa mabomu wamegoma kutawanyika.
Peeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeopleeees !!!!!!! Mbuya mbuyaa tataa
 
Watoa taarifa muwe mnajitahidi kuweka na sababu ya matukio kama haya ili kuepuka speculations na kusaidia wananchi kufanya judgement.

Kupiga mabovu tu bila sababu ya msingi inayohatarisha usalama wa raia na mali zao ndio chanzo chenyewe cha uvunjivu wa amani
 
Watanzania wenzangu na wanachadema wenzangu tusipo angalia vizuri huyu Tundu Lissu atatupeleka pabaya, tumeishi kwa amani na upendo kwa miaka mingi lkn sasa anataka kutuchonganisha sisi kwa sisi, hatutaki kabisaaa
 
UPDATES

Polisi wamesalimu amri na kuondoka baada ya somo la Lissu kuwaingia. Mkutano unaendelea Nyamongo muda huu. Aidha baada ya raia kupigwa mabomu wamegoma kutawanyika.
Usisahau kutuwekea picha picha na video za kutosha.
 
Binafsi siwalaumu Polisi najua wapo kwenye shinikizo kali Sana kuhusu utendaji wao.
Sasa wachague moja kuburuzwa the Hague kwa kutii maagizo ya mtu ambae arudi tena kuwatesa watz au waunge mkono mabadiliko
 
Ameyasema hayo Nyamongo akiwa anawaeleza viongozi wa Jeshi la Polisi waliozuia msafara wake.

Ameeleza yupo tayari kupingwa mabomu au risasi kama wanataka.

Kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi malalamiko yote ya ratiba na mchakato wa uchaguzi vinaratibiwa na tume ya uchaguzi huku kazi ya polisi ikiwa ni kusimamia ulinzi katika maeneo wanayofanya mikutani wagombea.

Leo Mhe. Magufuli amesimama maeneo mbalimbali akiwa anaelekea kwenye kampeni iringa na amezungumza na wananchi lakini hakuna polisi aliyemzuia.

Vivyo hivyo kwa Tundu lisu akiwa njiani kuelekea Serengeti na baadaye Arusha anayo haki yakuzungumza na wapiga kura. Huu ndio muda pekee wa wagombea kukutana wa wananchi na Ni muda sahihi wa Jeshi la Polisi kuonyesha ueledi na uvumilivu.

Tuheshimu na kufuata misingi ya malalamiko katika kampeni.
 
Watanzania wenzangu na wanachadema wenzangu tusipo angalia vizuri huyu Tundu Lissu atatupeleka pabaya, tumeishi kwa amani na upendo kwa miaka mingi lkn sasa anataka kutuchonganisha sisi kwa sisi, hatutaki kabisaaa
Msimzue tendeni haki kila kitu kiwe wazi hesabuni kura wazi kabisa ili isiwepo sababu ya kuzuia
 
Polisi kafyata Maskini, Kapewa hoja za nguvu kama kasimama kizimba Cha MAHAKAMA,

Kakosa hata Jibu la uongo, Kama Ingekuwa MAHAKAMANI Keshaenda Jela, Maana ni Kama alikuwa anasutwa, Amekuja Moto karudi Baridi.
 
Back
Top Bottom