The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Ni kawaida yeye kutoa Miamala hata leo kule Morogoro ameshaagiza barabara ipanuliwe na pia watajengewa vibanda kama walivyoomba pale Dumila sasa mkaweke pingamizi nyingine hiyo nyinyi wanasaccos ya Chadema...
Pingamizi litawekwa ikilazimika kuwekwa.
Lakini this is very complicated.
Hili swala ni la ki - mgongano wa sheria na katiba yetu.
Kiuhalisia, haya mambo ndiyo yanapaswa kurekebishwa ktk katiba yetu. Hayaleti usawa katika uchaguzi. Yanambeba na kumpendelea mgombea anayegombea nafasi ya Urais huku aikwa bado na madaraka ya Urais.
Ni vyema sana katiba ingesema, aliyekuwa Rais akiteuliwa na chama chake kugombea muhula wa pili, atalazimika kuacha madaraka yake ya Urais miezi mitatu kabla ya uchaguzi.
Katiba yetu ingekuwa clear kwa kiwango hiki, kusingekuwa na shida.
Kwa sasa shida IPO. Likiwekwa pingamizi, aliyewkewa pingamizi ambaye bado ni Rais, atajibu kwa urahisi kabisa kuwa, yeye anatekeleza majukumu yake ya Urais!
Ngoja tuone. Labda ndiyo itakuwa mwanzo wa kuanza kuyatazama mambo kwa jicho tofauti maana hii kitu haijawahi kutokea....