Kwamza wanajukwaa Nina wasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pili ninampongeza Mama Samia kwa hili la kumlipa stahiki zake ndugu yetu, mtanzania mwenzetu na makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo stahiki zake, ni Jambo jema na linapendeza pia ndio utanzania huu.
Tatu upinzani si kupinga,kukosoa, na kuchukia Kila kitu kinachofanywa na serikali ya ccm kwenye mazuri tuseme bila kupepesa macho, Tundu lissu aliumizwa, alidhulumiwa Sana na serikali ya awamu ya tano.
Nne Mama Samia ni kweli kabisa watanzania tunahitaji katiba mpya, week historia ya kudumu ulimwenguni Kama mwanamke aliyesaidia nchi yake kupata katiba mpya hicho utajivunia milele.
Tano, ninakuombea kwa Mungu akutangulie kutimiza majukumu yako ya uraisi maana ni magumu Sana na angalau unaonyesha nia njema na wewe ni tumaini jipya la watanzania kutokea CCM