Tundu Lissu: Tuna Rais Mzanzibari anayeweza kwenda Ngorongoro na kutoa Amri kwa Wanajeshi wafukuze wamasai wote

Spana na nyundo za Lissu ni hatari sana aisee kama mambo ndio hayo bora tugawane mbao. Tubaki na Tanganyika yetu wao wabaki na kisiwa chao kikizama watajijua wenyewe manake ukimya wetu sisi watanganyika wao wanatuona mazoba kumbe tunawa zoom tu!! Ashakum sio matusi.
 
Ndio mwanasiasa jasiri asiyeuma maneno.Nchi imepoteza uelekeo.Ila wale wanaokula na kusaza wanaendalea kutuhadaa kwamba mambo ni shwari.
 
Hapa kwa kweli Lissu amesema jambo. Amenikosha.
 
Kuna kesi wameshitakiwa Tanzania kwa ardhi iliyouzwa na wazanzibar, kwanza aliuziwa mwekezaji toka Mauritius halafu wakamnyang'anya wakauza kwa mwekezaji mwingine Ila anashtakiwa Tanzania.
Walipohisi Wana gesi Zanzibar wakaondoa kinyemela Tena kwa kuvunja katiba kwa maamuzi ya baraza la wawakilishi bila kupitia bungenla muungano.
Lakini baada ya kuapishwa rais Samia mkataba wa kwanza aliosaini ni wagesi na Kenya, amewaambia Zambia atawapa gesi na ardhi aliwapatia bure. Amegawa bandari, Loliondo, misitu, Kia na mwendokasi kwa waarabu.
Chadema wakitaka wapate sapoti kubwa wabebe ajenda ya Tanganyika .
 
Uzur wa CCM 2030 atakuja President mwingine atawaludisha Wamasai.
 
Angeweza kujadili hoja bila hizi kauli zake zenye ukakasi wa kikaburu! Huwezi kumzungumzia Rais wa nchi kirahisi hivi. Nchi hii inaundwa na Tanzania Bara na Zanzibar. Ndiyo maana pia, Rais wa nchi kutoka Bara ana mamlaka na nchi yote bila kujali kazaliwa Chato, Tanga, Mbeya au Gamboshi. #Lissu hana busara ya uongozi. πŸ™πŸ™πŸ™
 
Naona baada ya kutafuta wapi na nini watanzania wanataka, sasa umeshaelewa, kamatia hapohapo, awareness ifanyike, na hiyo ndio ticket yenu itakayo win mioyo ya wapigakura mwaka huu serikali za mtaa na mwakani.

Nawashauri kamatieni hapohapo, ukisikia mayowe jua jiwe limetua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…