Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuna upungufu wa kutisha wa fedha kwa ajili ya shughuli za Chama (CHADEMA), msiniulize nimekuta nini, jibu halitakuwa zuri!

Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuna upungufu wa kutisha wa fedha kwa ajili ya shughuli za Chama (CHADEMA), msiniulize nimekuta nini, jibu halitakuwa zuri!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu akiwa Kibamba akizungumzia urataibu wa kujiunga na Chama amesema kama Chama

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Nisiwadanganye, tunahitaji fedha kwenye Chama za kufanyia shughuli. Tuna upungufu wa kutisha wa fedha kwa ajili ya shughuli za Chama, wiki ijayo nimeambiwa tutafanya huo utaratibu wa namna ya kupata fedha za Chama. Msiniulize Mwenyekiti umekuta nini huko ulipoingia kwasababu sitajibu na sitajibu kwasababu jibu halitakuwa zuri sana"

Soma, Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%
 
Mbowe sahivi huko alipo.

6283808B-5EA4-4F4F-9072-4FA999DA676A.jpeg
 
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu akiwa Kibamba amesema "Tunaupungufu wakutisha wa fedha kwa ajili ya shughuli za Chama, usiulize nimekuta nini kwani majibu hayatakuwa mazuri"

si alisema pesa zinatumika vibaya, nae ataweka vizuri matumizi ya pesa za chama?

ziko wap hizo pesa sasa gentleman?🐒
 
Aache kutupigia makelele yake hapa. Naye atafute pesa zake za kuendeshea chama. Si aliona ni rahisi kuendesha chama? Hafahamu kuwa Mwamba alikuwa amejitoa na kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya CHADEMA? Na bado ipo siku atasema chama kimemshinda kukiendesha. Nipo pale 👉nimekaa naangalia mwisho wake
 
si alisema pesa zinatumika vibaya, nae ataweka vizuri matumizi ya pesa za chama?

ziko wap hizo pesa sasa gentleman?🐒
Sasa huwo utafiti wako ulikuwa unatafitia kitu gani hata kitu kidogo chenye kueleweka na wewe unaongea hoja ambayo hata haifanani na kilichoelezwa hapo.
 
K
Aache kutupigia makelele yake hapa. Naye atafute pesa zake za kuendeshea chama. Si aliona ni rahisi kuendesha chama? Hafahamu kuwa Mwamba alikuwa amejitoa na kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya CHADEMA? Na bado ipo siku atasema chama kimemshinda kukiendesha. Nipo pale 👉nimekaa naangalia mwisho wake
Kwani wewe kinachokuuma ni kitu gani mbona hamjui mnachokipigania hata huko ccm.
 
Lisu ana shida kama ya JPM. Hajui nini cha kuongea hadharani na kipi cha kuongea kwenye vikao vyao vya ndani. Atapoteza watu kwa hii style yake ya kuongea bila break. Asifikiri watu wanaipenda sana chadema. Ni vile hakuna chama mbadala kwa sasa wa kupambana na ccm.

Laiti wagombea binafsi wangekuwa wanaruhusiwa, ccm na chadema vingebaki na ofisi bila watu.
 
Yeye afanye kazi aache siasa za kulalamika,kama hakuna hela aseme chama hakina hela wanachama watachanga na siyo kulalamika kwamba hakukuta kitu wakati anajuwa fika Mwenyekiti mstaafu ndiyo alikuwa mfadhili wa Chama.
 
Sasa huwo utafiti wako ulikuwa unatafitia kitu gani hata kitu kidogo chenye kueleweka na wewe unaongea hoja ambayo hata haifanani na kilichoelezwa hapo.
unatuhumuje watu kua na matumizi ya pesa za chama hali ya kua hakuna hizo pesa?

watu walikua wanajitolea pesa zao mfukoni wewe unadai wanatumia pesa vibaya.

haya,
chama hicho hapo, wewe ndiyo kiongozi, panga basi matumizi mazuri ya chama.

Yaani kufanya retreat mbili tu dar na bagamoyo account ya chama inasoma zero?🤣
 
Aache kutupigia makelele yake hapa. Naye atafute pesa zake za kuendeshea chama. Si aliona ni rahisi kuendesha chama? Hafahamu kuwa Mwamba alikuwa amejitoa na kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya CHADEMA? Na bado ipo siku atasema chama kimemshinda kukiendesha. Nipo pale 👉nimekaa naangalia mwisho wake
yaani kafanya retreat mbili za kichama kwenye mahoteli ya maana huko bagamoyo,
account ya Chadema inasoma zero dah 🤣
 
Back
Top Bottom