Wakongwe kama wewe hawapaswi kuongea hivyo. Uongozi wa Mbowe uliweka wazi kuwa hakuna hela, na hata Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, wajumbe wa Kamati Kuu waligawana viwango vya fedha vya kutafuta kwa marafiki zao, hata Lissu aligawiwa ingawa hakuchangisha.
Sasa kama Mkutano wa mwisho tu wa awamu iliyomalizika haukuwa na fedha za chama za maandalizi, Lissu hakutegemea kukuta akaunti haina kitu au na hata kuikuta na madeni?
Unasema Mbowe ana kinyongo, sasa hicho kinyongo ni kipi, hataki kuchangia chama au ni vipi?