Wewe endelea kuropoka ropoka tu
Wewe ni mjinga na ni mpumbavu kwa wakati mmoja..

Hii ndiyo sifa kuu uliyonayo (ya ujinga na upumbavu) na ni lazima uambiwe na ukemewe Ili roho ya shetani inayokusukuma kutetea umwagaji damu ikutoke, uokoke....

Hamwezi kuendelea kumwaga damu za watu halafu watu wanyamaze...

HAPANA...!!!!

This time ni turn yenu. Mipango hii ya uovu mnayopanga Ili kumlinnda mama yenu mwovu na CCM yake, itageuka kuwa mishale ya kuwaumiza na kuwaua wenyewe na watoto wenu, na familia zenu..

Mungu hataki tena kuona mnaendeleza roho ya uuaji mliyonayo. Mkono wa hukumu ya HAKI ya Bwana na uwe juu yenu...
 
MAHOJIANO NA CLOUDSMEDIA 17 DECEMBER 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=CWWzPw0Pv4Y
Habari kamili :
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu amesema Watu wasiojulikana wanapanga njama za kumuumiza kisha wamsingizie Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe huku akiwataka waache kufanya wanalopanga kwakuwa watamchafua zaidi Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda.

Kupitia kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) leo Desemba 16, 2024 Lissu ameandika “Enyi Watu wabaya mjulikanao kama Watu wasiojulikana, nimezisikia njama zenu, mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa Chama, Freeman Mbowe, ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe, ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17 na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao"

"Ndivyo mavyofanya kila mnapoua Watu wasio na hatia, mnasingizia Watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu, huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani, Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo Bungeni"

"Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda mtamchafua zaidi na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia" ameandika Lissu ambaye pia ni Mgombea Uenyekiti wa Chama hicho
 
niliwahi kuandika humu
Kwa hili tishio la usalama wa Tundu Lissu aliloshikwa sikio kuwa kuna njama zinapangwa kumshughulikia Tundu Lissu afunguka A-Z wasiojulikana kutaka kumuumiza!
kama ni kweli njama hizo zilikuwepo ila sasa hazita tekelezwa tena kwasababu tayari zimeisha kuwa exposed

Then hoja za bandiko hili TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! bado zina sadifu!。
P
 
Lisu unakuwa mgombea wa unyekiti. Mbona kama anashida katika kuhifadhi mambo nyeti. Yaani kama hana siri yeye lopolopo nimegunduwa wanataka kunizulu watakuzulukweli. Kuwa na kaba mw/ mtarajiwa unayo yaongea yawe na afya kwa chama.
 
Katika mahojiano yake na Clouds Tv hapo jana, Tundu Lissu aliulizwa swali na Masoud Kipanya kuhusu alivyo-tweet juu ya watu wanaotaka kumshambulia. Je alipata wapi taarifa?

Lissu akajibu, alipigiwa whatsapp call na mtu mmoja mzito na anayeshimika zaidi nchini na ambaye hayupo serikalini juu ya kumtaka kuchukua tahadhali maana kuna mipango miovu dhidi yake.

Masoud akamuuliza huyo mtu ni nani, Lissu akajibu kwasasa hawezi kumtaja jina. Ila huyo mtu mzito nae anapata taarifa kutoka kwa wakubwa waliopo serikalini.

Nikajiuliza huyo mtu mzito na anayeheshimiwa zaidi nchini na hayupo serikalini ni nani?

NB
Mahojiano hayo yapo youtube
 
Nilimdokeza

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…