Tundu Lissu: Watekaji wanataka wanimalize wamsingizie Mbowe
Galasa hilo.

Ameivuruga CHADEMA sasa analia mbwa mwitu.

Mtafaruku aliouibua ni mkubwa. Sasa kwa kuficha PTSD yake anataka kubadilisha Narrative

Eti wanataka kummaliza?

Hao anaodai walitaka kummaliza ni wao wenyewe. Karata zao wanazijua.

Ikumbukwe maneno haya anayasema baada tu ya kutia nia ya kugombea Uenyekiti- Uchaguzi ni wa CHADEMA, na hivyo basi maneno yake haya ameyalenga kwa wale Wana CHADEMA wanaopinga nia yake hiyo yani watekaji, wauwaji na wale wasiojulikana wa CHADEMA, itoshe ishasikika Wangwe aliondoshwa na HAO HAO baada ya kutia nia

Sasa Tundu anaogopa kucheza karata zao na watu wake wenyewe anatupa galasa X
 
Mwambie aweke ushahidi na siyo kuropoka ropoka tu bila ushahidi .anatafuta sifa tu baada ya kuona hauungwi mkono katika nia yake ya kutaka kugombea uwenyekiti
Muungwana hunyamaza. Mwehu hujibu lolote. Nimwambie alete ushahidi upi, na nimekuambia kabla hajashambuliwa alisema na kutoa taarifa polisi na namba ya gari iliyokuwa inamfuatilia. Mtanzania yeyote akifa unapata shs ngapi., unaijua siasa kuliko Mwl Nyerere au Mwinyi au Mkapa ? Uliwahi kusikia mtu kaokotwa katobolewa macho nk au ulikuwa hujazaliwa. Mropokaji ni wewe unayefurahia vifo vya watanzania wenzako. Nyamaza.
 
Kama kawaida yake ya kuropoka ropoka Hovyo hovyo bila ushahidi wa aina yoyote ile
Mkuu wewe na Lissu nani anaweza kuwa anaropoka bila ushahidi. Inaelekea unafahamu njama hizi ndio maana unataka kudown play tahadhari anayoitoa Lissu.

Kuna pattern isiyo poa jinsi unavyohandle taarifa za tahadhari za victims humu ndani.
 
Kelele za Lusu zitaisha baada ya kushindwa uchaguzi

Lisu ana ji over rate sio saizi ya Mbowe yuko chini sana Mbowe yuko juu mno kumshinda
 
Enyi watu wabaya mjulikanao kama 'watu wasiojulikana,' nimezisikia njama zenu. Mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa chama, Freeman Mbowe.

Ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe. Ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17. Na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao.

Ndivyo mnavyofanya kila mnapoua watu wasio na hatia. Mnasingizia watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu.

Huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani. Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo bungeni.

Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan. Badala ya kumlinda mtamchafua zaidi. Na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia.View attachment 3178142
Nategemea hawatakuwa wapumbavu kiasi hicho.

Na kama kweli ni wapumbavu wa aina hiyo, basi inabidi wajue hatma yao haina tofauti na madhalimu wote wajulikanao. Hakuna hata mmoja wao aliishi kwa furaha katika uhai wake.
 
Kelele za Lusu zitaisha baada ya kushindwa uchaguzi

Lisu ana ji over rate sio saizi ya Mbowe yuko chini sana Mbowe yuko juu mno kumshinda
Ungeishia kwenye mstari wa kwanza unge eleweka tu vizuri, lakini umeamua kuuchafua kwa kuongeza madoido yasiyo husika kabisa na huo mstari wa pili.
 
Wewe na RAIS TUNDU LISSU nani mwenye akili kuliko mwenzie???
 
Back
Top Bottom