Ee Mungu mkuu uzidiye mamlaka na uweza wote, uliyewahi kuyaangamiza majeshi ya wakuu walioaminika kuwa na mamlaka yasiyoweza kufanywa chochote, Ee Yesu ambaye kwa upendo mkuu ulikubali kuteseka, kuimwaga damu yako, na hata kufa msalabani, ambaye hatimaye uliyashinda mauti ya mwili na Roho, ukamshinda shetani na ufalme wake, ukapewa mamlaka yote Duniani na Mbinguni, kwa mkono wako wenye nguvu, umtazame mtumishi wako Tundu Lisu kwa jicho la huruma na ushindi, tunaomba umshirikishe katika ule ushindi wako dhidi ya mauti kama ulivyomfanyia hapo mwanzo dhidi ya yeyote anayepanga uovu wowote juu ya uhai wake. Kwa sababu ya ile sadaka aitoayo kwa watu wako, kwa kuunena uovu wa watawala wautendao dhidi ya watu wako wasio na uwezo wa kunena wala kujitetea, ukampe ulinzi wako usiopenyeka wala kwa risasi, sumu, kisu au kingine chochote. Na kwa mkono wakp wenye nguvu, hao waupangao huo uovu na waliopangwa kuwa watekelezaji wa uovu huo, matokeo ya uovu walioupanga, yakawarudie wenyewe na watu wao, na washiriki wao, hata mara 3 zaidi.
Yeyote atakaye ulinzi juu ya Lisu na adhabu dhidi ya waovu, kila siku baada ya kufanya toba jwa Bwana, aisali sala hii mfululuzo kwa siku 7 au 3. Kumbukeni kuwa 3 7 na 40 ni namba za ukamilifu.
NB: Sala siyo mbadala ya kutimiza wajibu wetu kama wanadamu kwa kutumia zile nguvu na mamlaka zote aluzotujalia. Wakati tukiomba mkono wenye nguvu wa Mungu dhidi ya waovu, tuendelee kupambana kupinga mifumo na matendo yoyote ya dhuluma dhidi yetu na wengine wote wanaoonewa na mifumo ya utawala na watawala.