Tundu Lissu: Watekaji wanataka wanimalize wamsingizie Mbowe
Samia kapewa maelekezo na waarabu ya kulinda ''uwekezaji'' wao. Wametoa fedha nyingi za kuhonga vyama vya upinzani ili visimpe upinzani na kuanika uovu wake na wakati wa uchaguzi visitoe upinzani kamili. Lissu pekee ndiye aliyekataa hii hongo ndiyo maana wanapanga njama za kumuumiza. Unakumbuka yule simba wa kwenye maonyesho ambaye Samia alisema ''hatulii kama Lissu'' hivyo aitwe Lissu? Alikuwa anamaanisha hatulii hata akipewa fedha!
Lugha kama hizi za kuchafua watu bila ushahidi ndio Huwa Zina wa cost mnaanza kulaumu wengine.

Unaweza tuwekea ushahidi?
 
Wajaribu tukinukishe, maana tumechoka!! Hii nchi ni yetu sote!!wasituchukulie poa!!kisa tuna vyeo vidogo jeshini! hao wanaowaumiza ni ndugu zetu!!
 
Usifikiri LISSU ni mwepesi kihivyo kama wewe mpuuzi kwa taarifa Yako Kuna watu wema ndani ya vyombo vya usalama wanampa LISSU taarifa sahihi ni watu wema wasiopenda upuuzi wa ccm walioko kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Mwambie aache kuropoka Hovyo hovyo pasipo ushahidi hapa.anatafuta sifa tu huyo na uropokaji wake.
 
Mdomo wake haujawahi kuwa na utulivu wala staha wala hekima wala umakini wala utaratibu.ukimwambia weka ushahidi anaanza kujiuma uma tu.ndio maana nimesema ya kuwa itakuwa ni Uwendawazimu na ukichaa kwa CHADEMA kumchagua Lissu kuwa mwenyekiti wake. Lissu hawezi kujiongoza hata yeye mwenyewe. Ndio maana anashindwa kuongoza hata kauli na Maneno yake.
Dogo naona zile kelele zenu za kuwa mbowe ameoverstay sasa kimya

Mnakubali kuwa cdm ni mwalimu wenu wa siasa
 
Je hamkumuua Ally Kibao? Uchunguzi ambao Samia aliagiza uko wapi?

Unaweza kuwa Unalipwa leo hivyo vihela vidogo lakini Tambua Shetani hana Rafiki, Mangula aliwekewa sumu lumumba
Unawafahamu waliomuua kibao? Unaweza kusaidia jeshi la polisi ?
 
2017 alipeleka ushahidi polisi mpaka namba za gari iliyokuwa inamfuatilia. Akifa utashangilia kwa sababu ulimi wako umezoea ladha ya damu ya watu. Ccm ni chama changu ila mtanzania yeyote akifa naumia, sababu huko tunao ndugu pia. Wewe ndiye unaropoka.
Mwambie aweke ushahidi na siyo kuropoka ropoka tu bila ushahidi .anatafuta sifa tu baada ya kuona hauungwi mkono katika nia yake ya kutaka kugombea uwenyekiti
 
Kutoka X Lissu anaandika,

Enyi watu wabaya mjulikanao kama 'watu wasiojulikana,' nimezisikia njama zenu. Mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa chama, Freeman Mbowe.

Ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe. Ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17. Na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao.

Ndivyo mnavyofanya kila mnapoua watu wasio na hatia. Mnasingizia watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu.

Huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani. Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo bungeni.

Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan. Badala ya kumlinda mtamchafua zaidi. Na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia.
Lissu , chomoka kwanza njoo siku ya uchaguzi, acha kambi yako iendelee kupambana ,
 
Usifikiri LISSU ni mwepesi kihivyo kama wewe mpuuzi kwa taarifa Yako Kuna watu wema ndani ya vyombo vya usalama wanampa LISSU taarifa sahihi ni watu wema wasiopenda upuuzi wa ccm walioko kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Huyu punguani anadhani Lisu ni mtupu kama alivyo yeye. Lisu anaungwa mkono na watu wengi wenye akili na wanaopenda nchi, ambao wapao hata ndanibya CCM na Serikali. Ndiyo maana hata hayati Magufuli alivyokuwa taabani na mara alipofariki, alipewa taarifa yeye kabla ya Watanzania tuliokuwepo nchini.
 
Duh hawatafanikiwa na hawatafanikiwa huu ujinga waliutumia kwa chacha wangwe hawatafanikiwa kamwe


We are watching them24/7 wakijaribu tunapindua kabisa serikali na ndio utakuwa mwisho wa CCM!!

Yaani safari hii wasifanye hayo. Watasababisha hali ya kiuchumi kuwa mbaya ghafla. Mabwanyenye watakacho tufanya si cha kawaida. Na ndo mwisho wa chama cha majani. Tafadhali kwa Jina la Yesu wasijaribu!!!! Wanafikiri Lissu ni wa kawaida.
 
Mbona umetahamaki sana mkuu? Unafahamiana na hao watu wabaya nini? Umenishtua kidogo.
Mwashambwa hafahamiani na hao wauaji. Na siamini kama naye ni miongoni mwa hao wauaji. Bali uropokaji wake ndio unaoweza kuwafanya watu wafikirie kuwa yeye ni miongoni mwa hao wauaji.

Aliye miongoni mwa hao wauaji ni Tlaatlaah, siyo Mwashambwa.
 
Enyi watu wabaya mjulikanao kama 'watu wasiojulikana,' nimezisikia njama zenu. Mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa chama, Freeman Mbowe.

Ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe. Ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17. Na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao.

Ndivyo mnavyofanya kila mnapoua watu wasio na hatia. Mnasingizia watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu.

Huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani. Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo bungeni.

Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan. Badala ya kumlinda mtamchafua zaidi. Na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia.View attachment 3178142
Wamuache bhana, washamtia ulemavu inatosha.
Hata huruma hawama????
Warmonger.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu ambaye pia ni Mgombea Uenyekiti wa Chama hicho, amesema Watu wasiojulikana wanapanga njama za kumuumiza kisha wamsingizie Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ambapo amewataka waache kufanya wanalopanga kwakuwa watamchafua zaidi Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda.
IMG_1694.jpeg

Kwenye taarifa yake aliyoitoa leo December 16,2024, kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Tundu ameandika yafuatayo "Enyi Watu wabaya mjulikanao kama 'Watu wasiojulikana,' nimezisikia njama zenu, mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa Chama, Freeman Mbowe, ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe, ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17 na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao"

"Ndivyo mavyofanya kila mnapoua Watu wasio na hatia, mnasingizia Watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu, huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani, Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo Bungeni"

"Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda mtamchafua zaidi na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia"
 
Back
Top Bottom